This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/10/13 at 15:52
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Televisheni

Kanzi data ya Televisheni

Idadi ya vituo vya TV haijaongezeka tangu mwaka 2012- bodi ni vituo 48 kwa mujibu wa TCRA. Idadi ya vituo vya “Free-To-Air” imeongezeka kufikia chaneli 27 ambavyo ni miongoni mwa vinavyoangaliwa zaidi kwa ujumla, matumizi ya TV kwa muda mrefu yamekuwa yanakabiliwa na vikwazo, hasa kumudu gharama na upataji. Baada ya kuingia kwa mfumo wa kidijitali, hali hiyo imebadilika: Taarifa ya hali ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 vimetaja kuenea kwa vituo vya Televisheni katika sehemu mbalimbali za nchi yakiwemo maeneo ya pembezoni, ambako kutokana na kukosekana na miundombinu inayofaa ikiwemo umeme, upataji wa TV imeonesha maendeleo makubwa.

Matumizi ya TV

Bado matumizi ya TV yanaonekana si chanzo muhimu cha habari kama ilivyo redio, asilimia 47 ya Watanzania wanatumia T V kama chanzo cha taarifa angalau mara moja kwa mwezi, hata hivyo, haifiki hata robo ya watanzania wanaotumia kila siku. Idadi kubwa zaidi (39%) hawatumii TV kabisa kupata habari.

Umiliki wa wingi wa hadhira

Soko la TV lina wingi mkubwa kwa kuwa kampuni kuu 4, Tanzania Broadcasting Corporation inayomilikiwa na taifa (TBC), Azam Media Limited, na Clouds Entertainment Limited zinawakilisha hadhira ya XX.XXX%  IPP Group, inamilikiwa na mjasiriamali wa vyombo vya habari, Dkt Reginald A Mengi. TBC kwenye karatasi ni mtangazaji wa umma na kuendeshwa na serikali kwa vitendo. Familia ya Bakhresa inamiliki Azam Media Limited, mali ya kampuni yao kubwa ya Bakhresa Group inayoendesha biashara kuanzia vyakula hadi boti za usafiri. Joseph Kusaga, aliyeanzisha Clouds Fm na kuikuza na kuiendeleza, pia anamiliki hisa nyingi za kampuni- hali ya kuwa wanafamilia yake wengi wanamiliki hisa zilizobaki.

Kupungua kwa matangazo ya Biashara kama changamoto.

Kupungua kwa matangazo ya biashara kwa upande mmoja kumesababishwa na msimamo wa serikali wa kuzuia matangazo ya biashara na kubana matumizi miongoni mwa mashirika na watangazaji wakubwa, kwa upande mwingine ni kutokana na maendeleo ya mawasiliano kimtandao. Kampuni za utangazaji zimechukua hatua nyingi kushughulikia hali hii, kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya vyombo vya Habari ya MCT, 2016.

Hata hivyo, miongoni mwa nyingine ni pamoja na njia mpya za kusambaza maudhui ya habari kwa kutumia vifaa vya kidijitali. Hatua nyingine ni mkakati wa sasa ambapo baadhi ya vituo vya redio na TV vimekua vinashirikiana  na kampuni za simu za mkononi kupitisha maudhui ya habari zao kupitia vifaa vya mtandao ambapo raia (watumiaji simu za mkononi) wanalipia kwa baadhi ya maudhui ya habari kutoka kwenye vituo vyao kwa viwango maalumi. Katika juhudi hizo hizo za kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia, vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini vimeanzisha, ukutanishaji wa simu za mkononi – kwenda –redio/televisheni ambapo wasikilizaji au watazamaji wanatumia simu zao za mkononi wanapiga simu studio na kushiriki kwa ukamilifu kwenye kipindi kinachoendelea hewani. Utaratibu huu unasemekana umeongeza umaarufu wa vituo hivyo pamoja na kupanua wigo.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ