This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/28 at 13:43
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Historia

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili zilizokuwa huru – Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ulioanza rasmi Aprili 26, 1964. Muungano huo mwanzoni uliitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini ilipofika Aprili 29, 1964, muungano ulipewa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tanzania bara ilipata uhuru Desemba 9, 1961 chini ya Tanganyika African National Union (TANU) kilichoongoza harakati za uhuru. Zanzibar ilipata uhuru moja kwa moja kutoka kwa utawala wa Mwingereza Desemba 10, 1963 chini ya Sultani wa Kiarabu. Hata hivyo, mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 yalimpindua Sultani wa Kiarabu na kutoa mamlaka kwa Waafrika walio wengi chini ya  Afro-Shiraz Party (ASP). TANU na ASP vilivunjika  kwa hiari na kuunda Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari 5, 1977

Mfumo unaokinzana

Vyombo vya habari Tanzania bara kati ya Desemba 1961 wakati nchi ilipopata uhuru na 1965 wakati nchi ilipokuwa chini ya chama kimoja, vilifanyakazi katika mfumo unaokinzana. Serikali ya Waalendo ilitaka kutumia vyombo vya habari kuimarisha ujenzi wa taifa lakini wakati huo huo magazeti yote maarufu, ya kiingereza na kiswahili yalimilikiwa na wajasiriamali binafsi hali ya kuwa Shirika la Utangazaji la Tanganyika (TBC) lilikuwa shirika la umma. Katika kipindi hiki hakukuwa na sera rasmi ya vyombo vya habari ingawa takribani vyombo vya habari vyote vilitumikia maslahi ya tabaka tawala.

 “Vyombo vya habari kwa Wananchi”- Vyombo vya utumishi wa umma

Hata hivyo, baada ya kupitishwa Azimio la Arusha Februari 5, 1967 lililokuwa waraka rasmi wa sera ya serikali kuhusu ujamaa na kujitegemea, kazi kuu ya vyombo vya habari ilikuwa kuimarisha juhudi za TANU na serikali yake katika kuandaa watu ili washiriki kwa ukamilifu katika kujenga nchi ya ujamaa na kujitegemea na kutangaza sera ya ujamaa na kujitegemea. Sera hii ya vyo vya habari iliongezwa uzito zaidi Februari 5, 1970 wakati serikali ilipotaifisha The Standard (Tanzania) na rais Nyerere aliandika maoni ya kwanza ya mhariri iliyojulikana kuwa ni tamko la rahisi na ilijulikana kuwa “Gazeti la Kijamaa kwa Wananchi”. Ingawa tamko hilo lililenga zaidi gazeti moja mahususi, kanuni zilizowekwa na miongozo iliyotolewa ilikuja kueleweka kuwa ni sera ya jumla ya vyombo vya habari kwa vya umma nchini.

Mambo muhimu ya tamko hili ni kwamba, vyombo vya habari vilikuwa ni vyombo vya utumishi wa umma; vitaunga mkono itikadi ya Tanzania kama ilivyoelezwa katika Azimio la Arusha; vitadumisha mjadala wa uma wa wazi na huru na ukosoaji unaojenga kwa chama na serikali; vitakuwa huru kukosoa utekelezaji wa sera zilizokubaliwa; vitatoa mawasiliano ya pande mbili baina ya serikali na watu;   na vitajizatiti kitaaluma kusimamia kweli. Hata hivyo, wakosoaji wa tamko hilo walisema kwamba, kwa kweli sera mpya ya vyombo vya habari ndani ya tamko ilikusudiwa kuvifanya vyombo vya habari kuwajibika na kuwa tayari kwa ajili ya walio madarakani kwa gharama yoyote.

Mfumo wa chama kimoja, upashaji habari wa aina moja

Baada ya Azimio la Arusha vyombo vya habari nchini vilikuwa vinatoa taarifa za chama na serikali yake tu kwa sababu vilikuwa vikitumiwa zaidi na chama na serikali kuwafikia wananchi kuliko kutumiwa na wananchi kukifikia chama na serikali kinyume na Tamko la rais. Vyombo vya habari vilijibainisha na matarajio ya watu tu kwa kiasi fulani hali ya kuwa vilikuwa vikituniwa kuzungumzia maslahi ya chama cha taifa na wafanyakazi wa vyombo vya habari walikuwa kama vyombo vya viongozi wa chama dhidi ya matarajio ya watu. Vyombo vya habari vilidhibitiwa serikalini kupitia Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970 na Sheria ya Magazeti ya 1976, ni miongoni mwa sheria hizi; na utaratibu kama vile Kamati ya Vyombo vya Habari ya Chama, kuwapiga siasa waandishi wa habari kwa kuhudhuria vyuo vya itikadi ya chama na kuwafanya wawe wanachama na baadhi yao kuwa watumishi wa serikali.

Mwandishi wa habari mkongwe aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Radio Tanzania, Ng’wanakilala alitoa hitimisho halisi la hali ya vyombo vya habari nchini Tanzania enzi za mfumo wa chama kimoja wakati alipoandika mwanzoni mwa miaka ya 1980; Ni haki kuhitimisha kuwa katika hali ambapo chama na serikali vinahudumia maslahi yao wakati huo huo vikidai kwamba vinahudumia wananchi, na wakati vyombo vya habari vinamilikiwa na serikali, vyombo vya habari vitatoa utetezi unaotakiwa kwa hiari au bila ya hiari na kulinda maslahi, pia, kwa kisingizio cha wa wananchi. Kwa hiyo, pale ambapo vyombo vya habari vinashawishiwa na viongozi wa chama na serikali na pale ambapo maendeleo ya vyombo vya habari vya umma yanapuuzwa, vyombo vya habari vitakuwa chombo cha ukandamizaji licha ya kuwa vyombo vyenyewe vinakandamizwa.

Baada ya 1992: anuwai na aina mbalimbali

Mageuzi ya kisiasa yaliyoanzishwa nchini Tanzania 1992  na kubadilisha sheria ya vyombo vya habari baada ya hapo vimesababisha kuwepo kwa utaratibu mpya wa vyombo vya habari nchini utakaohakikisha kuwapo kwa uhuru zaidi wa vyombo vya habari. Uliibuka utitiri wa vyombo vya habari na baada ya muda mfupi nchi ilijikuta imejaa magazeti, redio na televisheni vilivyobadilisha soko la namna umma wa Tanzania unavyopashwa habari. Haikuwa rahisi tena kuzuia taarifa kwa kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali haviwezi kutoa taarifa hiyo. Kwa hiyo hakukuwa na uanuwai wa kutosha na aina mbalimbali za maoni kwenye vyombo mbalimbali vya habari na msimamo ulikuwa miongoni mwa misimamo mingi iliyoonekana na umma ulikuwa na fursa ya kuchagua nini cha kusoma, kutizama na kusikiliza.  Kwa hali hii vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu masuala mengi yenye maslahi ya umma na ya kitaifa.

Wimbi la mabadiliko, lakini...

Hata hivyo ongezeko hilo lililoonekana katika uhuru wa vyombo vya habari hivi sasa liko katika mtanziko baada ya kutungwa na kutekelezwa kwa sheria kandamizi na uamuzi wa serikali tangu utawala wa awamu ya tano ulipokuwa madarakani Novemba, 2015.

Chanzo

Condon, J (1967). Nation-Building and Image Building in the Tanzanian Press. Journal of Modern African Studies, Vol. 5, p. 334-335.
Konde, H (1984). Press Freedom in Tanzania. East African Publishing House.
Mboya, F, Mkwawa J, Kilimwiko, L (1982). The Functions and Role of the Press in Tanzania; A case study. Diploma Thesis, Tanzania School of Journalism.
Mwaffisi, M (1985). Broadcasting in Tanzania: Case study of Broadcasting System. MA Thesis, University of Washington, Seattle, USA
Mwaffisi, M ( 2013). Editorial Independence in Public Broadcasting in Africa: Case of Tanzania Broadcasting Corporation During Multi-party Presidential Elections, 1995-2010. PhD Thesis, University of Dar es Salaam.
Mytton, G, (1976). The Role of Mass Media in Nation-Building in Tanzania. PhD Thesis, Manchester.
Ng’wanakilala, N (1981). Mass Communication and Development of Socialism in Tanzania. Tanzania Publishing House.
Sturmer, M (1998). The Media History of Tanzania. Ndanda Press, Songea.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ