Uhusiano wa Kisiasa
Uhusiano wa kisiasa wa wamiliki wa vyombo vya habari na kampuni za vyombo vya habari uko wazi zaidi nchini Tanzania. Serikali imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na miongoni mwa wamiliki wakubwa wa vyombo vya habari vya utangazaji na magazeti. Chama tawala cha CCM nacho kina miliki kampuni ya vyombo vya habari pia. Viongozi wengi maarufu wa siasa wanajihusisha na uendeshaj9i wa vyombo vya habari – na kuna majadiliano machache ya umma kuhusu jambo hilo.
Uhusiano wa kisasa maana yake chombo cha habari au kampuni inamilikiwa na chama, kikundi cha wazalendo, kiongozi wa chama au mzalendo tu.. Kujihusisha sana kisiasa na kujitoa zaidi kunaweza kusababisha mgongano wa kimaslahi kwa watu wanaojishughulisha na kutayarisha kipindi au waliyopo kwenye majukumu na matukio, masuala ya kisiasa au sera ya umma.
Hii haina maana ya moja kwa moja kuwa kila uhusiano wa kisiasa unaathiri maudhurioo ya chombo cha habari - lakini kuna hatari hiyo. Kuna hatari – hasa inapotokea mada nyeti au nyakati za mjadala mkali wa kisiasa – uenezaji wa habari unaweza kuwa wa upendeleo.
Je, migongano ya maslahi ni nini na kwa nini ni muhimu?
Vipengele vitatu ni muhimu zaidi
- Je, ni kiwango gani au aina ya kujihusisha kisiasa? Kuna tofauti baina ya uanachama wa kimyakimya, kuwa mgombea wa chama, kuwa kiongozi wa umma, na kuzungumza hadharani au kuandikia mambo yenye utata wa kisiasa.
- Wafanyakazi wa vyombo vya habari:Je, mfanyakazi huyo anafanya kazi gani? Wahariri wa habari au vipindi vya matukio wenye uhusiano wa kisiasa ndiyo wenye mgongano mkuwa wa maslahi. Kwa aina nyingine za maudhui, ikiwamo mtindo wa maisha, burudani na utashi maalumu kama vile michezo, gari au kupika, mgongano wa maslahi bila shaka utakuwa si muhimu kabisa.
- Wamiliki wa vyombo vya habari:Je kuna ushiriki gani katika uamuzi wa wahariri sera ya kipindi au chombo cha habari. Wakati haja ya kutokuwa na upendeleo au upande wowote kwa wale wanaofanya kazi zaidi katika uandishi wa habari au katika nafasi nyingine nyeti za uhariri ni muhimu, ushirikishaji wa wamiliki wa vyombo vya habari katika kipindi au sera ya uhariri unatofautiana. Kimsingi “Ukuta mkuu wa china”baina ya chumba cha habari na chumba cha bodi ya wakurugenzi unaweza kuwezesha uhuru wa utoaji wa maudhui kutoka kwenye msimamo wa kisiasa wa mmiliki.
Je, kuna masharti gani ya kisheria nchini Tanzania?
Hakuna sheria inayomzuia mtanzania yeyote, wakiwemo watu wenye uhusiano wa kisisa, kutoendesha chombo cha habari, kisheria. Hakuna mipango yoyote ya kisheria na usimamizi kushughulikia suala hili.
Uhusiano wa kisiasa wa vyombo vya habari vya Tanzania.
Miongoni mwa vyombo vya habari vilivyofuatiliwa, theluthi moja vina wamiliki wa hisa, wenye uhusiano wa kisiasa, au kumilikiwa na taifa ukiangalia kampuni za vyombo vya habari , miongoni mwa kampuni 21, zilizofanyiwa uchanganuzi, tumebaini kampuni tano zenye wamiliki wenye uhusiano wa kisiasa au umiliki wa taifa: Tanzania Briadcasting corporation, Tanzania Standard Newspaper, Free Media Limited ,New Habari (2006) na Uhuru Media Limited. Wakati idadi kamili inatia wasiwasi, hatari inayosababishwa na udhibiti wa umiliki iko katika kiwango kinachoweza kusimamiwa. Vyombo vya habari vilivyoathiriwa havipendwi na hadhira, na hivyo kupunguza ushawishi wao kwa maoni ya umma.
Kusema kweli, uhusiano wa kisiasa nchini Tanzania haujifichi na wala haujadiliwi sana.
- Tanzania Broadcasting Coorporation (TBC), Tanzania Standard Newspaper (TSN); humilikiwa na taifa.
- Freeman Media Limited: inamilikiwa na chama tawala CCM.
- Uhuru Publication Limited: mwenye hisa nyingi ni Dkt Lilian Mtei, binti wa mwasisi wa CHADEMA na mke wa Mwenyekiti wa CHADEMA; Freeman Mbowe.
- Sahara MEDIA Group Limited: inahusishwa na Dkt. Anthony Diallo, ambaye hivi sasa ni mwenyekiti wa mkoa wa chama tawala cha CCM. Aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mwanza, mwaka 1995 HADI oktoba, 2010, alipopoteza na kuchukuliwa na upunzani. Ametumikia byadhifa mbalimbali kwenye baraza la mawaziri kuanzia 2000 mpaka 2008. Alikuwa Naibu waziri wa viwanda na Biashara, Naibu waziri wa maji na mifugo na waziri wa maliasili na utalii.
- New Habari (2006) Ltd: Rostam Aziz alikuwa kiongozi wa CCM wa ngazi za juu, lakini alijiuzulu nafasi zake zote rasmi mpaka leo. Alikuwa madarakani wakati alipoanzisha Mwananchi Communication Limited (MCL) pamoja na aliyekuwa Balozi Ferdinand Kamuntu Ruhinda. Wote waliiuza MCL, mwaka 2014.
Uchaguzi unaonyesha kilele cha utoaji taarifa kizalendo
Has nyakati za uchaguzi, tabia za kisisas za kampuni za vyombo vya habari zinadhihirika. Ripoti ya MCT “Watching dogs “Imetoa mwanga kuhusu mwenendo wa utoaji taarifa za kisiasa wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015. Ripoti inaonyesha mwelekeo wa vyombo vya habari baina ya vile vinavyoungamkono chama tawala, kuhusiana na umiliki wao.
Hali kadhalika vyombo vya habari, vinavyomilikiwa na Taifa na chama tawala vimejitokeza kivyao kuunga mokono serikalo, chama tawala cha CCM nacho kilipata kutangazwa zaidi kwenye vyombo vya habari vya kielectroniki ikilinganishwa na vyama vya upinzani. Waandishi wa habai walioambatana na timu za kampuni za wagoombea urais walikuwa wakitoa taarifa na kutopendelea upande wowote. Isipokuwa kwa Star TV na RFA, vya Sahara Media Group vinavyohusishwa na Dkt. Anthony Diallo, Mbunge wa CCM – vyombo vya kielectroniki vya binafsi havikuwa na upendeleo.
Ripoti pia imebaini kuwa New Habari (2006) Ltd na magazeti yake ya Mtanzania Rai, Dimba na The African yaliunga mkono upinzani. Hali hii ilistaajabishwa sana, kwa sababu New Habari imeungana mkono chama tawala na Serikali yake kwenye uchaguzi uliyopita. Sababu za mabadiliko haya: Mmiliki Rostam Aziz – aliyekuwa mwanasisa wa ngazi ya juu wa chama tawala – alikuwa na uhusiano wa karibu na mgombea wa upinzani Edward Lowasa.
Lowasa alienguliwa katika mbio za kugombea urais kwa chama tawala na hivyo kuwa mgombea urais wa upinzani. Ghafla, New Habari (2006) Ltd ikageuka “kutaka mabadiliko”na kumuunga mkono Lowassa.