This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/12/09 at 07:48
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Siasa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Jamhuri yenye raisi mtendaji. Nchi hii ina mfumo wa vyama vingi vya siasa ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa madarakani tangu 1961, wakati Tanzania ilipopata uhuru wake. Dr John Joseph Magufuli alishinda uchaguzi wa rais wa Oktoba 2015 kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi na kuapishwa Novemba 5, 2015. Utawala wa rais Magufuli umelenga zaidi kutokomeza rushwa serikalini na kusimamia matumizi bora ya mapato ya serikali, na kuongeza udhibiti wa vyombo vya habari.

Wimbi la mabadiliko... lenye kuleta hali mbaya zaidi

Ongezeko la uhuru  wa vyombo vya habari linaloonekana katika mwongo uliyopita wa tangu 1992 hivi sasa umo katika mtanziko kutokana na kutungwa na kutekelezwa kwa sheria kali na uamuzi wa serikali tangu utawala wa awamu ya tano uwe madarakani kwanzia Novemba 2015. Sheria zinazokiuka uhuru wa vyombo vya habari na wa kujieleza nchini zinajumuisha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya mwaka 2015(Cybercrime Act, 2015), Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Upataji wa Taarifa ya mwaka 2016. Sheria ya Upataji wa Taarifa ilionekana kuwa ni hatua chanya lakini pia ina upungufu mkubwa unaozuia uhuru wa vyombo vya habari. Kwa jumla, utawala uliyopo hivi sasa unaelekea kuwa na wasiwasi wa kukoselewa na kudhamiria kuanzisha vyombo vya habari visivyojiamini.  Hatua na uamuzi wake unakinza jitihada za kuendeleza uhuru mkubwa wa vyombo vya habari nchini Tanzania, ambao ni muhimu kwa kuzidisha demokrasia

Njia zenye hila za kuzuia uhuru wa kupata habari

Mifano ya uamuzi wa utawala wa ahamu ya tano iliyoathiri vibaya uhuru wa vyombo vya habari nchini ni kupigwa marufuku kwa matangazo mubashara ya shughuli za bunge na kufuta usajili wa magazeti na majarida 473.

Kufutwa kwa usajili wa magazeti na majarida hayo kumepunguza idadi ya machapisho yanayoendeshwa kisheria katika soko la Tanzania kwa zaidi ya 50%. Uamuzi wa serikali kufuta usajili wa idadi kubwa ya magazeti imewaogopesha wawekezaji wapya katika tasnia ya uchapishaji kwa sababu baada ya hatua ya kufuta usajili huo, idadi ya machapisho yaliyosajiliwa imepungua sana.

Matangazo mubashara ya shughuli za bunge yalianza katikati ya miaka ya 2005 na yalijikusanyia umaarufu mkubwa wakati wa utawala wa awamu ya nne. Matangazo haya yalikuwa muhimu kwa sababu kutokana na umuhimu wa majadiliano ya bungeni kwa wananchi na umuhimu wake katika kuhimiza siasa za mawazo mbalimbali. Hata hivyo, serikali imefuta matangazo mubashara ya shughuli za tangu Aprili 2016 na badala yake mfumo mpya umeanzishwa ambapo maripota na watangazaji wote walikabidhiwa taarifa zilizo haririwa sana kuhusu mijadala ya bunge.

Sources

Worldatlas (2018). What Type Of Government Does Tanzania Have?. Accessed on 22 October 2018.

G. Chisseo (2017). Assessing Public Opinion on the ban of live parliamentary Broadcast in Tanzania: Case of Ilala District. MA Dissertation, St. Augustine University of Tanzania.
J. Ulimwengu (2000). The Role of Mass Media in the Promotion of Good Governance. A paer presented at a conference in Dar es Salaam, 24-25 February 2000.
Martin Sturmer (1998). The Media History of Tanzania. Ndanda Press, Songea.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ