This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/07/18 at 14:24
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Viashiria Hatarishi kwa Vyombo Habari

Wingi wa hadhira ya vyombo vya habari

Kiashirio hiki kinapima wingi wa hadhira na usomaji kwenye vyombo vya habari vyote kulingana na kiasi cha hadhira. Wingi huo unapimwa kwa kutumia wamiliki wakubwa wanne kitaifa kwenye soko.

Matokeo:
HATARI YA KIWANGO CHA JUU (ISIPOKUWA MTANDAONI)

Kwa nini?
Kutokana na wingi wa soko la utangazaji na magazeti, na kiasi kidogo cha wingi wa vyombo vya habari kwenye sekta ya mtandaoni , wingi wa hadhira ya vyombo vya habari unaweka HATARI YA KIWANGO CHA JUU kwa aina na wingi wa vyombo vya habari nchini Tanzania.

Soko la magazeti linaonyesha kiwango kikubwa cha wingi wa hadhira. Tuliangalia Kampuni kubwa 4 za juu kwenye soko la magazeti yanayolenga habari; Mwananchi Comunication Limited (MCL) (chini ya umiliki wa Nation Media Group XX.XXX%), IPP Media Group, (XX.XXX%), New Habari (2006), Ltd, (XX.XXX%), na gazeti la Serikali la Tanzania Standard Newspaper (TSN XX.XXX%). Usambazaji wao wa habari kwa magazeti kwa jumla ina XX.XXX% ya wasomaji MCL linamilikiwa na kampuni binafsi na kuendeshwa na Nation Media Group, iliyopo Kenya na kugharamiwa na The Aga Khan Development Fund. IPP Media Group, ni kampuni binafsi, inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu aliyefanikiwa, Dkt. Reginald Mengi. New Habari (2006) Ltd, inahusishwa na mwanasiasa na mfanya biashara Rostam Aziz hali ya kuwa wenye hisa hawafahamiki vizuri ingawa tetesi za kuhusishwa na Aziz. Wingi unazumgumzia hali ya soko la Habari za magazeti isipokuwa magazeti ya michezo, hata hivyo washiriki wa kuu ni walewale hata kama uaingiza magazeti ya michezo.

Soko la TV lina kiwango kikubwa, kutokana na kampuni kubwa nne (IPP: XX.XXX%, Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) inayomilikiwa na Serikali: XX.XXX, Azam Media Limited: XX.XXX% na Clouds Entertainment Ltd: XX.XXX%, kwa jumla zina soko la XX.XXX%. IPP Media Group inamilikiwa na mjasiriamali maarufu wa vyombo vya Habari Reginald Mengi, TBC ni mtangazaji wa umma kwenye karatasi na kuendeshwa na taifa, kwa vitendo inamiliki Azam Media Limited iliyopo kwenye kundi kubwa la Kampuni za Bakhresa Group linaloendesha biashara mbalimbali kuanzia vyakula hadi boti za usafiri. Joseph Kusaga, aliyeanzisha Clouds Fm na kuikuza na kuwa maarufu, ana miliki hisa nyingi za kampuni wakati baadhi ya wanafamili yake wanamiliki hisa zilizobaki.

Soko la RADIO nalo ni mchanganyiko zaidi na linaongoza katika soko na kutofautiana kutoka mkoa mmoja hadi mwingine. Nayo Clouds Entertainment Lt: XX.XXX%, IPP (XX.XXX%), Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) inayoendeshwa na Taifa: XX.XXX%, kama ilivyo kwenye TV- zina idadi kubwa ya soko na kila mmoja ikiendesha vituo, yenye vituo vingi vya redio na TV inafuata kwa soko la XX.XXX% ya hadhira. Hakuna taarifa rasmi za kampuni kwenye masjala ya Biashara ya BRELA. Taarifa zinamtaja Dkt. Anthony Diallo, Mwanasiasa na Mbunge wa zamani, mwasisi, Ofisa mtendaji mkuu na mmiliki wa kampuni ya Diallo pia huwakilisha vyombo vya habari kwenye matukio ya umma. Soko la redio linaonyesha kuwa, kuwango cha wastani cha wingi wa juu kama ilivyo kwa kampuni 4 za juu hufikia wasikilizaji XXX.XX%. Kuhusu soko la mtandaono, MCT ilifanya utafiti wa haraka haraka, kuhusu tovuti maarufu sana. Tovuti maarufu sana ya habari ukiondoa mitandao ya kijamii ni blogu huru. Hazihusiani na chombo cha habari chochote cha asili hata hivyo inakuwa mtoa habari mbadala na uwanja wa majadiliano. Kuna wingi wa kiwango kidogo cha hadhira kwa sababu watumiaji wake wanataja blogi mbalimbali za habari mtandaoni. Kampuni 4 za vyombo vya habari mtandaoni zilizotajwa zaidi kama vynzo vya habari kwa XX.XXX% ya watu waliofanyiwa utafiti, tuliyowachangua.

Wamiliki wake walianza kama waendesha blogi, na wajasiriamali wa kidigitali na wanaooonyesha kutokana shughuli nyingine zozote za biashara na siasa. Jamii Forum, iliyoanzishwa na Max Melo, na Mike Mushi, ni blogi maarufu na inayotumiwa sana (XX.XXX%). Millard Ayo, alianzisha blogi yenye jina lake (XX.XXX%) pamoja na Isa Michuzi (XX.XXX%), Muungwana Blog, ni miongoni pia mwa blogi zinazotajwa sana imeanzishwa na kumilikiwa na Muungwana na Rashid Malik Said ambaye hajioneshi.

UPUNGUFU:
Kiwango cha hadhira ya TV na Redio kinatokana na utafiti wa GeoPoll war oho mwaka ya pili ya 2018. Matumizi ya magazeti na mtandao yalitokana na utafiti wa haraka haraka GeoPoll kwa kutumia nyimbo mfupi (arafa) uliyofanywa kwa siku mbili mwezi Agosti / September. GeoPoll inasemekana kuwa Shirika la kuaminioka, hata hivyo, kimbinu, watanzania, wenye simu za za mkononi tu ambao ni vijana, wanaume na wanaoishi mjini kuliko watanzania wa kawaida.

KIWANGO CHA CHINIWASTANI
KIWANGO CHA JUU
Wingi wa hadhira katika TV (baina ya TV) 

Asilimia:

Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wako 4 (4 wa Juu) wana hadhira ya chini ya 25%  Iwapo ndani ya ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wa juu) wa hadhira ya kati ya 25% na 49%.   Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wa juu) wana hadhira ya zaidi ya 50%.  
Wingi wa hadhira katika redio (baina ya redio).  

Asilimia: 

Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wa juu)wanahadhira ya chini ya 25%.   Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wa juu) wanahadhira ya kati ya 25% na 49%.   Iwapo ndani ya nchi moja, wamiliki wakuu 4 (4 wa juu) wana hadhira ya zaidi ya 50%. 
Wingi wa wasomaji wa magazeti (baina ya magazeti)  

Asilimia:

Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wa juu) wana wasomaji nchini ya 25%. Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wa juu) wana wasomaji kati ya 25% na 49%.  Iwapo ndani ya nchi moja, wamiliki wakuu 4 wana wasomaji zaidi ya 50%. 
Wingi wa hadhira katika Intanet (baina ya intanet) 
Asilimia:
Iwapo ndani ya nchi moja wa miliki wakuu 4 (4 wa juu) wanahadhira ya chini ya 25%. Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wa juu) wanahadhira ya kati ya 25%.  Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wa kuu 4 (4 wa juu) wana hadhira ya zaidi ya 50%. 

Wingi wa soko la vyombo vya habari

Kiashirio hiki kinakusudia kupima wingi wa umiliki baina ya vyombo vya habari kwa mujibu wa hisa ya soko inayodhihirisha uwezo wa fedha wa kampuni / makundi ya kampuni. Wingi unapimwa kwa kila sekta ya chombo cha habari kwa kuomgeza hisa za soko za wamiliki.

Matokeo:
Wingi wa soko la chombo cha ahbari kwa mujibu wa hisa za soko haukuweza kufa nyiwa hesabu. Wakati wakala ya usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inaruhusu kuingia kwenye baadhi ya data za umiliki, data za fedha ( mapato, mapatangazo n.k) hazikuwepo a) kwa kampuni ya vyombo vya habari b) kama hisa ya soko na c) kwa kila sekta ya vyombo vya habari.


Alama: 

ChiniKatiJuu
Wingi wa umiliki wa televisheni (baina ya TV): Mashirio hiki kinakusudia kupima wingi wa umiliki ndani ya sekta ya TV.  
Asilimia:  Haikupimwa
Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanasoko chini ya 25%.   Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wana soko kati ya 25% na 49%. Iwapo ndani na nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanasoko zaidi ya 50%. 
Wingi wa umiliki wa redio (baina ya redio): Kiashirio hiki kinakusudia kupima wingi na umiliki ndani ya sekta ya redio.    
Asilimia:  Haikupimwa
Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira chini ya 25%.  Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira kati ya 25% na 49%. Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira zaidi ya 50%.  
Wingi wa umiliki wa magazeti (baina ya magazeti): kiashirio anakusudia kupima wingi wa umiliki ndani ya sekta ya magazeti.
Asilimia:  Haikupimwa
Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira chini ya 25%. Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira kati ya 25% na 49%.  Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira zaidi ya 50%. 
Wingi wa umiliki katika watoa huduma za maudhui ya Intanet.
Asilimia:  Haikupimwa
Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira chini ya 25%.   Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira kati ya 25% na 49%. Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki 4 wakuu (4 wa juu) wanahadhira zaidi ya 50%.   

Kanuni za usimamizi: Wingi wa umiliki wa vyombo vya habari (baina ya vyombo vya habari)

Kiashiria hiki kinapimia kuwapo na utekelezaji wenye ufanisi wa kanuni za usimamizi ? (Zinazohusu sekta na au sharia ya ushindani) dhidi ya wingi wa kiwango cha juu cha umiliki na/au udhibiti katika vyombo vya habari tofauti.

Matokeo:
HATARI/YA KIWANGO CHA JUU

Kwa nini?

 • Masharti muhimu ya katiba haya jumuishi vifungu au aya zozote zinazokusudia kuzuia wingi na ukiritimba wa vyombo vya habari. Sheria mbili za vyombo vya habari zilizotungwa hivi karibuni – The media services Act na The Access to Information Act – hazishughulikii suala la wingi wa vyombo vya habari na suala hilo linaelekea kutokuwa kwenye ajenda kwa watunga sharia na watayarishaji sera hivi sasa.
 • Kuna kikomo kimoja tu kwa umiliki wa vyombo vya habari, umiliki wa mgeni kwenye vyombo vya habri usizidi 49% kwa mujibu kwa Information and Broadcoas ting policy, 2003 pamoja na media Services Regulations, 2017.
 • Utoaji lessen kwa sekta ya vielelezo vya kuona na kusikia kutegemea kuwapo kwa masafa. Vyombo vya habari vya kielektroniki nchini Tanzania vinasimamiwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), sheria lililoanzishwa kwa mujibu wa sharia ya Tanzania communications Regulatory Authority Act, 2003. TCRA inatoa, inaongeza muda na kufuta leseni. Mamlaka ya chombo hicho hata hivyo, kuhusu utoajai au ubatilishaji wa leseni, kwa kipindi mahususi au majukumu ya huduma kwa wote, au kuwa na kipindi cha miaka mitano au zaidi haiwezi kutekelezwa bila ya kushauriana kabla na waziri na Waziri anayehusika na sekta.
 • Katika sekta ya mmagazeti, The Media Services Act, 2016, ilibatilishwa Newspapers A ct ya 1976 iliyopingwa sana iliyompa Waziri wa habari mamlaka ya kupiga marufuku uchapishaji wa gazeti na kushughulikia kashfa au kuchafua sifa au jina la mtu, ambayo inachukuliwa kuwa ni kosa la raia, ni kosa la jinai, linalostahili hukumu ya kifungo.
 • Kwa mujibu wa sharia mpya mkurugenzi wa idara ya habari (maelezo) anatoa leseni kwa magazeti na ana mamlaka ya kukataa au kubatilisha leseni iwapo maombi hayatimizi masharti au aliyepewa leseni anakiuka mashrti ya leseni.
 • Kwa mujibu wa The Electronic and postal Communications (online content) Regulations, 2018, waendesha blogi, kama ilivyo redio ya mtandaoni na tovuti za TV, wanatakiwa kupewa leseni na TCRA, waendesha blogi wanatakiwa kulipa ada ya maombi ya 100,000/= ada ya awali ya leseni ya 1,000,000/= na ada ya kuongeza muda wa leseni 100,000/=, wakati leseni ya televisheni na radio (kuingiza maudhui kwenye intaneti) watalipia ada ya maombi ya 50,000/=, ada ya awali ya 200,000/= na ada ya kuongeza muda wa leseni ya 200,00/=.
 • Kanuni mahususi za vyombo vya habari na kuzuia uunganishaji au ununuzi hazipo. Pia hakuna chombo cha ushindani kitakachozuia uunganishaji na ununuzi.


Alama za kanuni za usimamizi:
0 kati ya 20 – hatari ya kiwango cha juu (0%).
1 = kanuni/mamlaka mashususi ya vyombo vya habari
0.5= kanuni/mamlaka inayohusiana na ushindani

  JEDWALI HILI LINATOA MUHTASARI WA TV/RADIO/ONLINE/NA GAZETI    MaelezoNdiyoHapanaNAMD
  Je, sharia ya vyombo vya habari ina ukomo au vikomo mahususi vinatokana na vigezo visivyo na upendeleo (kwa mfano idadi ya leseni, kiasi cha hadhira, usambazaji wa hisa au haki za kipiga kura mapato maduhuli kuzuia kiwango cha juu cha wamiliki baina ya vyombo vya habari na au udhibiti kwenye sekta hii?     Swali hili linakusudia kupimia kuwapo kwa kanuni za usimamizi (za sekta) dhidi ya kiwango cha juu cha wingi wa umiliki baina ya vyombo vya habari na/au udhibitisho wa SEKTA YA TELEVISHENI/RADIO.     

   

    X

   

  Je, kua mamlaka ya utawala au chombo cha mahakama kinachofuatilia kwa ukamilifu ufuasi wa ukomo kwenye sekta ya magazeti na /au kusikiliza malalamiko? (kwa mfano vyombo vya habari na/au mamlakaya ushindani)?     Kigezo kinakusudia kupimia iwapo sharia kanuni inafanya ufuatiliaji unaostahili na mfumo wa kuruhusu kanuni kwa wingi wa vyombo vya habari vya kusikiliza na kuona.     

   

    X
  Je, sheria inakipa chombo hiki mamlaka ya utekelezaji wa sharia ili kutoa tahadhari zinazostahili (za kitabia na kimuundo) iwapo hutakuwa na kutoheshimiwa kwa ukomo?     

  Kigezo kinakusudia kupimia iwapo sharia vikwazo kwa kwa kanuni ya kisekta kama vile.

  • Kukataa kutoa leseni ya ziada
  • Kuzuia uunganishaji au ununuzi
  • Jukumu la kutenga madirisha ya program za chombo cha tatu,
  • Jukumu la kuacha kutoa leseni/ shughuli kwenye sekta nyingine za vyombo vya habari
  • Kuondolea madaraka    
   

    X

    

  Je, mamlaka haya ya kuruhusu /kuhimiza sharia yanatumiwa kwa ukamilifu?     Kiashirio hiki kinakusudia kupimia utekelezaji kwa ufanisi wa tahadhari za kisekta dhidi ya kiwango cha juu cha umiliki baina ya sekta na/au udhibiti katika televisheni.     

  Hatari ya kiwango chajuu (0)

  Jumla  

  0

   

  UUNGANISHIJI VYOMBO VYA HABARIMaelezoNdiyoHapanaNAMD
  Je, kiwango cha juu cha wingi wa umiliki baina ya vyombo vya habari na/au adhibiti katika sekta ya vyombo vya habari unaweza kuzuiwa kupia udhibiti wa uunganishaji/kanuni za ushindani zinazozingatia umahususi wa sekta ya chombo cha habari?     

  Swali hili linakusudia kupima kuwapo kwa kanuni za kusimamia (za kisekta na /au sharia ya ushindani) dhidi ya kiwango cha juu cha wingi wa umiliki baina ya vyombo vya habari katika sekta ya vyombo vya habari kupitia shughuli za uunganishaji. kwa mfano sharia haina budi kuzuia wingi katika shughuli za uunganishaji. Kwa kuzuia masharti mahusussi ya vyombo vya habari yanayoweka ukomo mkali zaidi kuliko kwenye sekta nyingine Uingiliaji kati wa kisheria wa mamlaka ya vyombo vya habari katika matukio ya uunganishaji na uumimizi kwa mfano wajibu wa mamlaka ya ushindani kuomba ushauri wa mamlaka ya vyombo vya habari. Uwezekano wa kubatilisha kuidhinisha wingi na mamlaka ya mawasiliano kwa sababu ya wingi wa vyombo vyombo vya habari kwa maslahi ya umma kwa jumla ambao hata kama hauna masharti mahususi ya vyombo vya habari havizuii sekta ya vyombo vya habari kutoka kwenye mawanda yao ya maombi.

    X
  Je, kuna mamalaka ya utawala au chombo cha mahakama kinachofuatilia kwa ukamilifu ufuasi wa sharia za uunganishaji na/au kusikiliza malalamiko? (kwa mfano vyombo vya habari na/au mamalaka ya ushindani.     Kigezo hiki kinakusudia kupimia iwapo sharia/kanuni inatoa mfumo wa ufuatiliaji na kuruhusu unaostahiki.           X
  Je, sheria inatupatia chombo hiki mamlaka ya kuruhusu /kuhimiza sharia ili kuweka fahadhari zinazostahili ( kitabia na /au kinamuundo) iwapo kutakuwa na kutoheshimiwa wa vikono?     

  Kigezo hiki kinakusudia kupimia iwapo sharia inatoa mfumo unaostahili wa vikwazo kwa kanuni mahususi za sekta, kama vile.

  • Kuzuia uunganishaji au ununuzi
  • Jukumu la kutenga madirisha ya program za chombo cha habari
  • Jukumu la kuacha kutoa leseni/shughuli kwenye sekta nyingine vya vyombo vya habari
  • Kuondolea madaraka
        X
  Je, mamlaka haya ya kuruhusu/kuhimiza sharia yanatumiwa kwa ukamilifu?      Kiashirio hiki kinakusudia kupimia utekelezaji kwa ufanisi wa tahadhari za kisekta dhidi ya kiwango cha juu cha umiliki baina ya sekta na/au udhibiti katika televisheni.     Hatari ya kiwango cha juu (0)
  Jumla0 ya 3

Wingi wa umiliki wa vyombo vya Habari

Kiashirio hiki kinapania wingi wa umiliki kwenye sekta mbalimbali-TV, magazeti, vya kusikiliza, na chombo cha habari kingine chochote chenye umuhimu- cha tasnia ya vyombo vya habari. Wingi wa vyombo vya habari mtambuko hupimwa kwa kuongeza viwango vya soko vya Topmedia Companies.

Matokeo:
HAKUNA DATA/HATARI YA KIWANGO CHA JUU

Kwanini?

 • Wingi wa vyombo vya habari mtambuko hupimwa kwa kuzingatia uwezo wa soko. Hata hivyo kiwango cha soko, hakikupatikana kama ilivyokuwa kwa data za fedha kwa ujumla. Wakala wa mienendo ya umiliki wa vyombo vya habari mtambuko kwa kuzingatia viwango vya hadhira havikuweza kubainishwa pia, kwa sababu data za tabia za utumiaji – muhimu kwa kutambua umuhimu wa kila sekta ya magazeti, TV, redio na mtandao zimepitwa na wakati. Data za mwisho za kuaminika zilizopatikana zinaonyesha ni za 2014.
 • Kukosekana kwa vidokezo vya data kwa hatari ya kiwango cha juu, kwa sekta ya vyombo vya habari kwa kuwa kanuni za usimamizi wa vyombo vya habari zenye ufanisi hazikutayarishwa na kutekelezwa. Katika hali ya sasa mamlaka za usimamizi zisingechukua uamuzi wenye uthibitisho wa hoja na hatua za sera.
 • Jitihada za kuanzisha kanuni za kusimamia vyombo vya habari mtambuko zimechelewa kutayarishwa. Wakati wadau wa vyombo vya habari vimeweka mada hiyo kwenye ajenda mapema zaidi mwanzoni mwa milenia, serikali imesita. Hali hii imeruhusu kampuni za vyombo vya habari mtambuko, kuenea zaidi- kama vile IPP Media Ltd, ambayo hivi sasa ni miongoni mwa kampuni kubwa za vyombo vya habari Afrika Mashariki, inaendesha magazeti na utangazaji, na hivi karibuni imejisajili kama mtoa maudhui mtandaoni. Kampuni hizo zina uwezekano mkubwa wa kuwaondoa washindani, hali hiyo ina uwezekano wa kuhatarisha wingi wa vyombo vya habari nchini. Hata hivyo wingi halisi wa vyombo vya habari mtambuko, haukuweza kutathminiwa.

Alama:

KIDOGOWASTANIKIWANGO CHA JUU

Asilimia: Hakuna data zilizopatikana

Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wajuu) wana soko la chini ya 50% kwenye sekta mbalimbali za vyombo vya habari  Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wajuu) wanahudhuria kati ya 50% na 89% kwenye sekta mbalimbali za vyombi vya habari. Iwapo ndani ya nchi moja wamiliki wakuu 4 (4 wajuu) wana soko zaidi ya 70% kwenye sekta mbalimbali za vyombo vya habari.  

Kanuni za usimamizi: Wingi wa umiliki mtambuko wa vyombo vya habari

Kiashirio hiki kinapima kuwapo na ufanisi wa utekelezaji wa kanuni (zinazohusu sekta na/ au sheria ya ushindani) dhidi ya wingi wa kiwango cha juu cha umiliki tambuka baina ya vyombo vya habari kuteka aina ya vyombo vya habari tofauti (magazeti, TV, Radio, Intaneti).

Matokeo:
HATARI YA KIWANGO CHA JUU


Kwa nini?

 • Hakuna mamlaka inayofuatilia kwa ukamilifu umiliki mtambuko wa vyombo vya habari. Hakuna uelewa wa kisiasa au kisheria kwa hali hiyo ya wingi wa vyombo vya habari katika soko la vyombo vya habari Tanzania.
 •  Mwaka 2009 Serikali ilipendekeza marekebisho ya sera ya Habari na utangazaji kwa lengo la kuondoa kasoro zilizopo kwenye sera iliyoanza kutumika mwaka 2003. Kulipendekezwa marekebisho mengi kwenye sera ya vyombo vya habari . Miongoni mwa marekebisho hayo lilikuwa suala la umiliki wa vyombo vya habari. Marekebisho yaliyopendekezwa yameitaka serikali kukataza umiliki mtambuko wa vyombo vya habari wa mtu mmoja. Kama marekebisho hayo yange pitishwa wamiliki wa vyombo vya habari wangeruhusiwa ama kuendesha magazeti au vyombo vya elektroniki, lakini sio vyote . Kwa wale wanaomiliki vyote rasimu ya sera imependekeza wapewe miaka mitano kuamia aina moja ya vyombo vya habari. Sababu ya serikali kuzuia umiliki mtambuko ni kufuatilia na kudhibiti matumizi mabaya ya wamiliki kutumia vyombo vya vya habari kwa manufaa ya biashara zao au maslahi ya kisiasa.
 • Hata hivyo pendekezo la Serikali lilikataliwa na wadau wa vyombo vya habari wakisema kuwa kuzuia umiliki wa vyombo vya habari kunakiuka uhuru wa vyombo hivyo na hakuendani na uchumi wa soko huria. wamesema kwamba. Suala la umiliki wa vyombo vya habari liachwe kwenye nguvu za soko na si kisimamiwa na Serikali – na hivyo kuwa mwisho wa mchakato wa kurekebisha sera.
 • Kutoana na kukosekana kwa kanuni, wamiliki mtambuko wakubwa wa vyombo vya habari kama IPP wasingeendelea. Pia wanaendesha baadhi ya aina kubwa zaidi za bidhaa kwenye televisheni na tasnia ya vyombo vya mtandao.


Alama za Sheria na kanuni:

0 kati ya 8 - Hatari ya kiwango cha juu (Kanuni: 0%)

UMILIKI MTAMBUKO WA VYOMBO VYA HABARI MaelezoNdiyoHapanaNAMD
Je, sheria ya vyombo vya habari, imeweka ukomo wowote kuhusiana na vigezo visivyo na upendeleo, kama vile iadi ya leseni, hadhira, usambazaji, ugawaji hisa ya mtaji au haki za kupiga kura mapato/ maduhuli, kuzua kiwango cha juu cha umiliki mtambuko baina ya vyombo vya habari tofauti      Kiashirio hiki kinakusudia kupima kuwapo kwa kanuni za usimamizi (zinazohusu sekta na / au sheria ya ushindani) dhidi ya wingi wa kiwango cha juu cha umiliki mtambuko baina ya sekta za vyombo vya habari tofauti.      X
Je, kuna mamlaka ya utawala au chombo cha mahakama kinachofuatilia kwa ukaribu ufuasi wa ukomo huo na/ au kusikiliza malalamiko (kwa mfano mamlaka ya vyombo vya habari = 1, mamlaka ya ushindani = 0,5)     Kigezo hiki kinakusudia kupima iwapo sheria / kanuni inatoa ufuatiliaji na mfumo wa kuiruhusu kanuni kwa wingi wa vyombo vya habari vya vielelezo vya kusikia na kuona.      X
Je, sheria inakipatia chambo kinachoruhusu mamlaka ya uhimizaji sheria ili kuweka tahadhari zinazofaa (za tabia na / au muundo) iwapo kutatokea kutoheshimiwa kwa ukomo?    

Kigezo hiki kinakusudia kupima iwapo inatoa mfumo wa vikwazo vinavyotakiwa kwenye kanuni za kisekta, kama vile:

 • Kukataliwa leseni za ziada.
 • Kuzuia uunganishaji au ununuzi,
 • Jukumu la kutenga madirisha ya ziada kwa ajili ya programu za chombo cha tatu.
 • Jukumu la kusitisha leseni/ shughuli kwenye sekta nyingine za vyombo vya habari.
 •  Kuondoa madaraka.
  X
Je, mamlaka haya ya kuruhusu/ kuhimiza sheria yanatumiwa ipasavyo?    

Mamlaka inayohusika haitumii kabisa uwezo wa kuziua. Swali linakusudia kupima ufanisi wa tahadhari zilizotolewa na kanuni.     

  X
Je, kiwango cha juu cha umiliki mtambuko baina ya vyombo vya habari tofauti kizuiwe kwa njia ya udhibiti wa uunganishaji/ sheria za ushindani zinazozingatia umahususi wa sekta ya vyombo vya habari?    

Kwa mfano, umiliki mtambuko unaweza kuziwa kwa kutumia sheria ya ushindani.

- Kwa uingiliaji ,kati wa kisheria wa mamlaka ya vyombo vya habari katika matukio ya M+A ( kwa mfano jukumu la mamlaka ya ushindani kuomba ushauri kwa mamlaka ya vyombo vya habari.

- Kwa uwezekano wa kubatilisha uidhinishaji wingi na mamlaka ya ushindani kwa sababu ya wingi na aina za vyombo vya habari (maslahi ya umma kwa jumla).

- Ingawa sheria haina masharti mahususi ya vyombo vya habari katika sekta ya vyombo vya habari mawanda yake ya matumizi.

  X
Je, kuna mamlaka ya utawala au chombo cha mahakama kinachofuatilia kwa ukamilifu ufuasi wa kanuni/ sheria hizi na / au kusikiliza malalamiko?( Kwa mfano vyombo vya habari na/ au mamlaka ya ushindani)?     Kigezo hiki kinakusudia kupima iwapo sheria / kanuni inatoa ufuatiliaji inaotakiwa na mfumo wa kuruhusu kwa ajili ya kanuni dhidi ya kiwango cha juu cha umiliki mtambuko kwenye sekta mbalimbali za vyombo vya habari kupitia udhibiti wa uunganishaji/sheria za ushindani    
Je, sheria inakipatia chombo kinachoruhusu mamlaka ya uhimizaji sheria ili kuweka tahadhari zinazofaa (za tabia na/ au miundo iwapo kutokea kutoheshimiwa kwa ukomo.    

Mfano ya mamlaka ya kuhuruhusu/ uhimizaji sheria na tahadhari.

- Kuzuia uunganishaji na ununuzi.

- Jukumu la kutenga madirisha kwa programu za chombo cha tatu.

- Lazima kutekeleza jukumu la kusitisha utoaji leseni/ shughuli kwenye sekta vyingine za vyombo vya habari.

- Kuondoa madaraka.  

X
Je, kuna mamlaka za kuruhusu/ uhimizaji sheria zinazotuhumiwa kwa ufanisi?    Swali hili lina kusudia kupima ufanisi wa tahadhari za kanuni.    Hapana
Jumla (ya viashirio vidogo vya wastani wa L.e na L. i   0 kati ya 8

Uwazi wa umiliki

Kiashirio hiki kinapima uwazi wa data kuhusu uhusiano wa kisiasa na wamiliki wa vyombo vya habari kwa sababu uwazi wa umiliki ni sharti muhimu la awali kuhimiza wingi wa vyombo vya habari.

Matokeo:
WASTANI


Kwa nini?

 • Kampuni zinatakiwa kujisajili wakala ya usajili wa Biashara ya leseni (BRELA) ambako zinatakiwa angalau zijaze fomu ya kampuni na wanahisa. Taarifa hii inapatikana kwa bei ya Tshs. 22,000 sawa na USD 10. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) umetoa baadhi ya taarifa za umiliki kuhusu watoa mahudhuio kwenye mtandao. Kuhusu magazeti, taarifa za umiliki ziko kinadharia, Idara ya Habari – MAELEZO: Orodha ya hivi karibuni kutoka MAELEZO haikujumuisha data za wenye hisa wala umiliki.
 • Ili kukamilisha data zilizokosekana ambazo hazikupatikana mtandaoni au nje ya mtandao, vyombo vyote vya habari (36) wakati mwingine viliulizwa moja kwa moja kwenye kampuni zao kwa kutumia dodoso.
 • Hakukuwa na kampuni ya chombo cha habari chochote Tanzania vilivyokuwa na uwazi kabisa. Hii inamaanisha kwamba hakuna kampuni ya chombo cha habari iliyochapisha taarifa kwenye tovuti zao au kwenye taarifa za kutangaza shughuli zao iliyoweza kupatikana. Ni Nation Media Group tu iliyoko nchini Kenya inayoendesha kampuni tanzu tu nchini Tanzania, umechapishwa wajumbe wake na menejimenti na bodi ya ushauri kwenye tovuti.
 • Uwazi wa kimya kimya pia ulikuwa wa kiwango: ni kampuni tatu tu, zenye jumla ya vyombo vya habari vinane zilirudisha madodoso ya maswali: Kampuni hizi ni pamoja na kampuni zinazomilikiwa na Serikali za Tanzania Broadcasting Corporation na Tanzania Communication Limited (MCL) (22%).
 • Kwa vyombo vya habari vingi, data zilizopatikana bila kificho za vyombo hivyo (64%) kutoka Idara ya Msajili Mkuu. Hata hibyo ubora wa taarifa rasmi za kampuni haukuwa mzuri na kulikuwa na taarifa ambazo hazikujazwa. Kusema kweli data zilikuwa za zamani, zimepitwa na wakati, na mabadilio ya umiliki haya kuandikwa.
 • Kwa 15% ya vyombo vya habari, data hazikupatikana BRELA ingawa na wajibu, kisheria kusajili kampuni. Huki ingawa tulilipia kupata taarifa za kampuni
 • Hakuna kampuni iliyodanganya kabisa.
KIDOGOWASTANIKIWANGO CHA JUU

Je, ungepimaje uwazi na upataji wa data kuhusu umiliki wa vyombo vya habari?

Data kuhusu wamiliki wa vyombo vya habari na uhusiano wao wa siasa inapatikana na kwa uwazi.

Jaza iwapo inafaa kwa >75% ya sampuli.

 

Data kuhusu wamiliki wa vyombo vya habari na uhusiano wa siasa zimepatikana kwa njia ya taarifa ya uchunguzi za waandishi wa habari wa wanaharakati wa vyombo vya habari au baada ya kuomba.

(uwazi wa kimya kimya data zimepatikana kwa uwazi)

Jaza iwapo inafaa kwa > 50% ya sampuli)  

Data kuhusu uhusiano wa siasa wa wamiliki wa vyombo vya habari hazipatikani kwa urahisi kwa wananchi na waandishi wa habari za uchunguzi na wanaharakati hawakufanikiwa kueleza data hizi (Data hazipo udanganyifu mkubwa).

Jaza iwapo data imepatikana kwa <50% ya sampuli.

Kanuni za usimamizi: Uwazi wa umiliki

Kiashiria hiki kinakusudia kupima kuwepo na utekelezaji wa uwazi kwa ufanisi na masharti kuhusiana na mumiliki wa vyombo vya habari/au udhibiti.

Matokeo:
HATARI ZA WASTANI

Kwa nini?

 • Ingawa hakuna sharia mahususi kuhusu uwazi wa umiliki, kanuni za uwazi wa kawaida pia zinatumika pia kwa sekta ya vyombo vya habari (TV, Radio, magazeti, mtandaoni) kuanzisha kampuni kunahitaji usajili katika wakala ya usajili wa biashara na leseni ( BRELA), ambako taarifa kama vile wanahisa, wakurugenzi, fomu ya kisheria tarehe za kusajiliwa n.k zitaorodheshwa taarifa ni lazima zihusishwe kila mwaka.
 • Zaidi ya hayo, taarifa kuhusu kampuni za magazeti zinaweza kupatikana hivyo MAELEZO, inayotoa leseni za magazeti. Hata hivyo inaorodhesha mwenye leseni tu ambaye anaweza kuwa mtu binafsi au kampuni. Si lazima sana kuorodhesha wenye hisa. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA). Inaorodhesha kampuni hizo na baadhi ya wenye hisa kwa watoa huduma za maudhui mtandaoni.
 • Wakati ni rahisi kupata taarifa kutoka MAELEZO na TCRA, katika BRELA, mchakato wa kupata taarifa ni mrefu sana, uleo taratibu sana na zuizi. Ili mtu apate taarifa za wamiliki inatakiwa kuomba mtandaoni na kulipa ada inayotakiwa ya (22000/=) Tsh/ USD kwa taarifa ya kampuni). mfumo wa maombi mtandaoni yako wazii tu kwa wale wenye kitambulisho cha taifa mchakato wa maombi umechukua hadi wiki sita. Baadhi ya taarifa za kampuni hazikujazwa, na baadhi ya majalada hayakuwapo.
 • Vikwazo kwa kutoheshimu wajibu wa kutoa taarifa vinaweza kuwekwa kinadharia na kufikirishwa mahakamani – hata hivyo hakujatokea kesi ya namna hiyo. Kampuni nyingi hazijajaza taarifa zao za karibuni kwa miaka mingi mfululizo – kama inavyoonekana kwa maelezo ya kampuni yaliyopatikana BRELA.

 

Alama za kanuni za usimamizi:

14 kwa 20 - hatari ya wastani (70%). Jedwali linaonesha muhtasari wa TV, redi, magazeti na mtandaoni. Alama za juu kabisa ni 5 kwa sekta.

Masharti uwazi (muhtasari wa TV, redia, magazeti, mtandaoni – alama za juu ni 5 kwa sekta) MaelezoNdiyoHapanaNAMD
Je sharia ya taifa (vyombo vya habari, kampuni, kodi ina masharti ya uwazi na utoaji taarifa kulazimisha kampuni za vyombo vya habari kuchapisha miundo yao ya uwazi kwenye tovuti zao au kwenye kumbuukumbu / nyaraka zinazopatikana kwa umma?     Lengo la wwali hili ni kukagua kanuni za usimamizi kwa ajili ya uwazi kwa raia, watu kiraji umma kwa jumla    X
Je, sharia ya taifa (vyombo vya habari kampuni kodi...) ina masharti ya uwazi na utoaji taarifa Kulazimisha kampuni za vyombo vya habari kutoa taarifa (mabadiliko ) ya miundo ya umiliki kwa mamlaka za umma (kama vile mamllka ya vyombo vya habari)?      Lengo la swali hili ni kukagua kanuni za usimamizi kwa uwajibikaji na uwazi kwa mamlaka ya umma.       X
Je, kama jukumu la sharia ya taifakutoa taarifa muhimu baada ya kulabaddiliko kwenye muundo wa umiliki?     Lengo la swali hili ni kupima iwapo sharia inatoa kanuni kwa upatikanaji data sahihi na za hivi karibuni kuhusu umiliki wa vyyombo vya habari. Hivi ni sharti la uwazi wenye ufaanisi.       X
Je, kuna vikwazo vyoyote iwapo hutatokea kutoheshimu jukumu la utoajai taarifa?     Swali hili linakusudia kupima iwapo sharia sharia kuhusu uwazi wa umuliki wa vyombo vya habari inaweza kusimamiwa kwa kutumia vikwazo.     X
Je, majukumu yanahaki kisha kuwa umma unafahamu ni mtu gani kisheria au wa kawaida anamiliki kwa ukamilifu au anadhibiti kampuni ya vyombo vya habari?     Swali hili linakusudia kupima ufanisi wa sharia zinazoshughulikia uwazi wa umili wa vyombo vya habari na iwapo sharia hizo zimefanikiwa kutoa taarifa za wamiliki sahihi wa vyombo vya habari.    Wastani baadhi ya wamiliki bado hawafamiki (= 0,5)
Total14 kati ya 20

Marejeo:

- Legal Assessment

Udhibiti (wa kisiasa) kwa vyombo vya habari mitandao ya usambazaji

Kiashirio hiki kinapima hatari ya vyombo vinavyohusiana kisiasa na udhibiti wa vyombo vya habari na mitandao ya usambazaji , Pia inapima kiwango cha ubaguzi wa mitandao ya usambazaji ya vyombo vya habari vinavyohusiana kisiasa. Kwa mfano hatua za kiubaguzi ni pamoja na bei ndogo na kuweka vipingamizi kwa vyombo vya habari kufikia chanels za usambazaji. Vyombo vinavyohusiana kisiasa ni kwamba chombo cha habari au kampuni ni mali ya chama, kampuni ni ya kizalendo , kiongozi wa chama au ni mzalendo tu.

Matokeo:
KIWANGO CHA CHINI

Kwa nini?

 • Kati ya vyombo vya habari vinavyofatiliwa 936) 13 vina wenye hisa na kampuni zenye uhusiano wa kisiasa au vinamilikiwa na Serikali. Kwa kuangalia kampuni 21 zilizochanganuliwa, tulibaini kampuni tano zenye wamiliki wenye uhusiano wa kisiasa au umiliki wa Serikali. Tanzania Broadcasting Corporation, Tanzania Standard Nespaper, Free Media Limited, New Habari (2006) na uhuru Media Limited.
 • Kwa jumla kuna kiwango cha chini cha hatari kwa kuzingatia udhibiti wa kisiasa kwenye umiliki kwa vyombo vya habari vilivyo fuatiliwa kwa kuwa vyombo vya habari vyenye uhusiano wa kisiasa havitumiwi sana na hivyo kupunguza ushauwishi wao kwa maoni ya umma. Wakati huohuo, udhibiti wa vyombo vya habari kwa njia nyingine – kama vile kanuni kandamizi – kutokea kwa kiwango kikubwa.
 • Wakati kuna idadi kubwa kiasi ya kampuni za vyombo vya habari na vyombo vyenyewe vinavyomilikiwa na wadau wa kisiasa, hadhira yao ni ndogo.

- Kwa kuangalia magazeti, magazeti ya Serikali kwa pamoja hufikia  XX.XXX%  ya hadhira kwenye soko la habari, uhuru Publication linalomilikiwa na CCM ni  XX.XXX%  na Tanzania Daima inayohusiana na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ni  XX.XXX% ya hadhira

- Kwa soko la habari la TV; TBC inakiwango kikubwa cha hadhira ( XX.XXX%) pamoja na Sahara media Group ( XX.XXX%).

- Kwa soko la redio, hasa TBC ( XX.XXX%) na kubwa. Uhuru FM ni hadhira ndogo zaidi ( XX.XXX%).

- Tovuti maarufu za mtandaoni ni blogi na majukwa huru.

Wamiliki wa vyombo vya habari wenye uhusiano wa kisiasa.

KIWANGO CHA CHINIWASTANIKIWANGO CHA JUU
KUINGIZA SASA KWENYE VYOMBO VYA HABARI     
Je, ni kiasi gani cha TV/Redio/Mtandao/Magazeti kinachomilikiwa na kampuni zenye uhusiano wa kisisasa?
Vyombo vya habari vyenye hadhira <30% vinamilikiwa (kudhibitiwa) na chama cha siasa, mwana siasa au vikundi vya siasa au na wamiliki wa chombo cha kisiasa.     Vyombo vya habari vyenye hadhira <50% - >30% vinamilikiwa (kudhibitiwa) na chama cha siasa, mwana siasa au vikundi vya siasa au na wamiliki wa chombo cha kisiasa. Vyombo vya habari vyenye hadhira >50% vinamilikiwa (kudhibitiwa) na chama cha siasa, mwana siasa au vikundi vya siasa au na wamiliki wa chombo cha kisiasa.    

 Udhibiti wa kisiasa kwa mitandao ya vyombo vya Habari ya usambazaji.

Kiwango cha jumla cha udhibiti wa kisiasa kwa vyombo vya habari na mitandao ya usambazaji kilipimwa kama hatari ya wastani kwenye wingi wa vyombo vya habari. Mtandao wa usambazaji maarufu ni mtandao wenye zaidi ya 15% ya soko la taifa.

Matokeo:
KIWANGO CHA CHINI


Kwa nini?
Udhibiti wa kisiasa kwa mitandao ya usambazaji inayoongoza inatofautiana baina ya sekta ya vyombo vay habari na sekta ya vyombo vya habari.

 • Vyombo vya uchapishaji vinasambaza machapisho vyenyewe kwa gari, ambavyo havilaumu kwa uthibiti wa kisiasa.
 • TV ilichelewa kuanza Tanzania (matangazo ya kwanza mwaka 1994), na kuongozwa na utangazaji wa terrestrial (24% ya wananchi ). Matangazo ya dijitali yalianza (2011) na kuzima analojia (2012) yameunda mtandao wa usambazaji TV wa sasa . Leseni mbalimbali ziliyolewa mwaka 2010 kwa star Media Tanzania, Agape Media na Basic Transmission. Kampuni mbili za mwisho zinamilikiwa na watanzania na kuhusiana na chaneli za TV zilizopo, wakati star media ni ubia baina ya star times ya china (inayomiliki 65 %) na TBC. Watoa huduma bado wapo sokoni.
 • Baadhi ya watazamaji walipoteza upataji wa TV baaa ya kuzimwa kwa analojia wanakadiriwa kuanza 20% hadi 50%, Dar es salaam nap engine idadi ndogo kwenye maeneo ambako usimaji ulitokea baadaye. Kwa mujibu wa kamati ya ushauri ya MOM, watazamaji waliongezeka lakini hawakufikia kiwango cha kabla ya kuzima dijitali.
 • Wakati TCRA inasimamia kuhakikisha ubora wa huduma, haifanyi hatua za ubaguzi zinazotokea dhidi ya baadhi ya vyombo vya habari. Hata hivyo, kamati ya ushauri ya MOM imebaini kuwa utazamaji TV, hasa habari za ndani, umepungua. Kwa mujibu wa taarifa zao, mtu anaweza kupata TBC tu inayomilikiwa na Serikali na visimbuzi baadaye. Hawakuto maelezo.
 • TCRA pia inasimamia mtandao wa redio kwa mujibu wa kamati ya ushauri, mpangilio huu si muhimu kwa udhibiti wa kisias.
KIWANGO CHA CHINIWASTANIKIWANGO CHA JUU
Je, utapimaje mwenendo wa mitandao maarufu ya usambazaji kwa magazeti? 
Mitandao maarufu ya usambazaji haihusiani kisiasa au havichukui hatua za kibaguzi.     Angalau moja ya mitandao maarufu ya usambazaji inauhusiano wa kisiasa au inachukua hatua za kibaguzi. Mitandao yote maarufu ya usambazaji ina uhusiano wa kisiasa na inarikodi ya hatua za kibaguzi za mara kwa mara.     
Je, utapimaje mwenendo wa mitandao maarufu ya usambazaji kwa redio? 
Mitandao maarufu ya usambazaji haihusiani kisiasa au haichukui hatua za kibaguzi.  Angalau mtandao mmoja maarufu ya usambazaji inauhusiano wa kisiasa au inachukua hatua za kibaguzi.     Mitandao yote maarufu ya usambazaji ina uhusiano wa kisiasa na inarikodi ya hatua za kibaguzi za mara kwa mara.    
Je, utapimaje mwenendo wa mitandao maarufu ya usambazaji kwa Televisheni? 
Mitandao maarufu ya usambazaji haihusiani kisiasa au haichukui hatua za kibaguzi.Angalau mtandao mmoja maarufu ya usambazaji inauhusiano wa kisiasa au hachukui hatua za kibaguzi.  Mitandao yote maarufu ya usambazaji ina uhusiano wa kisiasa na inarikodi ya hatua za kibaguzi za mara kwa mara. 
Je, utapimaje mwenendo wa mitandao maarufu ya usambazaji kwa Intanet? 
Mitandao maarufu ya usambazaji haihusiani kisiasa au haichukui hatua za kibaguzi. Angalau mtandao mmoja maarufu ya usambazaji inauhusiano wa kisiasa au hachukui hatua za kibaguzi.   Mitandao yote maarufu ya usambazaji ina uhusiano wa kisiasa na inarikodi ya hatua za kibaguzi za mara kwa mara.   

Udhibiti (wa kisiasa) kwa Ugharimiaji Vyombo vya Habari

Kiashirio hiki kinapima ushawishi wa serikali kuhusu ufanyajikazi wa soko la vyombo vya habari kwa kuzingatia hasa hatari ya ubaguzi katika usambazaji wa matangazo ya Serikali/ugharimiaji. Ubaguzi unaweza kuonekana katika upendeleo kwa vyama vya siasa au vinavyohusiana na vyama vya siasa serikalini, au katika kutoa adhabu kwa vyombo vya habari vinavyolaumu serikali. Matangazo ya serikali ni matangazo yoyote yanayolipwa na Serikali (kitaifa, kimkoa, serikali ya mtaa) na taasisi za umma au kampuni.

Matokeo:
HATARI YA WASTANI/ YA KIWANGO CHA JUU

Kwa nini?

 • Kabla ya Media Services Act, idaraya Serikali, Wizara na nyinginezo zilifanya uamuzi wa matangazo kwa uhuru. Hapakuwa na sheria wala kanuni zilizowekwa kuongeza uamuzi wao kuhusu namna ya kusambaza matangazo yao.
 • Hivi sasa, kwa mujibu wa Media Services Act, 2016, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ana jukumu la kuratibu matangazo ya Serikali. Hii inamaana yake na kawaida, mtu mmoja aliyeteuliwa na Rais, ana mamlaka ya kutoa uamuzi kuhusu namna matangazo hayo yatakavyowekwa. Sheria haisemi ni vigezo gani au taratibu zitakazoelekeza uamuzi huo. Jinsi Mkurugenzi wa Maelezo anayofanya uamuzi wa uwekaji wa matangazo hayo ya Serikali, unakosa uwazi, na hivyo kuonesha kuwa ni HATARI YA KIWANGO CHA JU.
 • Kamati ya Ushauri ya MOM, kulingana na uzoefu wao, wamesema kuwa matangazo yamekuwa yanatolewa na bado yanasambazwa kwa upendeleo (kwa upande wa kiwango cha hadhira) kwa vyombo vya habari. Vyombo vya habari vya umma/serikalini au vya CCM vitapewa matangazo mengi ingawa hadhira yao, ikilinganishwa na vyombo vya habari vya binafsi na ndogo.

Alama:

KIWANGO CHA CHINIWASTANIKIWANGO CHA JUU
Je, matangazo ya Serikali/ugharimiaji unatolewa kwa vyombo vya habari unawiana na kiwango cha hadhira yao?  
Matangazo ya serikali yanatasambazwa kwa vyombo vya habari kwa uwiano kiasi kwa kiwango cha hadhira ya chombo husika. Matangazo ya Serikali yanatolewa kwa upendeleo (kwa upande wa kiwango cha hadhira) kwa vyombo vya habari. Matangazo ya Serikali yanayotolewa kwa vyombo vya habari vichache tu; na hivyo kutohusisha vyombo vya habari vikuu nchini.  
Je, utaipimaje sheria na kanuni za usambazaji wa matangazo ya Serikali?     
Matangazo ya Serikali yanayotolewa kwa vyombo vya habari kwa mujibu wa kanuni na sheria na wazi.     Matangazo ya Serikali yanatolewa kwa vyombo vya habari kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo ingawa haifahamiki iwapo ni wazi kiasi gani.     Hakuna sheria au kanuni kuhusiana na matangazo ya Serikali yanavyotolewa kwenye vyombo vya habari.   
UMUHIMU WA MATANGAZO YA SERIKALI     

Je, nini kiwango cha matangazo ya serikali kama sehemu ya soko la matangazo la jumla la TV/Redio/Magazeti na mtandaoni? 

KIWANGO: Hakuna data kuhusu kiwango cha matangazo ya serikali kwenye soko.

Kiasi cha matangazo ya Serikali ni <5% ya soko lote.   Kiasi cha matangazo ya Serikali ni 5% - 10% ya soko lote.     Kiasi cha matangazo ya Serikali ni >10% ya soko lote.·  

Marejeo:
- Legal Assessment
- The 2017 Budget Statement and Economic Policy

Kanuni za Usimamizi: Kutokuwa na upande wowote kabisa

Kutokuwa na upande wowote kabisa ni kanuni ambayo data zote kwenye mitandao ni lazima zishughulikiwe kwa usawa bila kubagua au kutozwa tofauti kwa watumiaji maudhui tovuti, maeneo au mifumo tumizi. Kulinda kutokuwa na upande wowote kabisa ni muhimu kwa kusimamia wingi na aina mbalimbali za vyombo vya habari kwa sababu inahakikisha uwezo sawa wa kupata na kusambaza taarifa, maoni, mitazamo n.k mtandaoni, ambayo ni muhimu kwa wingi na aina za vyombo vya habari. Kiashirio hiki kinaeleza madhara ya kanuni ya kisheria ya kutokuwa na upande wowote kabisa pamoja na taratiibu za usimamizi zinazoshughulikia kutokuwa na upande wowote mahususi.

Matokeo:
HATARI YA KIWANGO CHA JUU

Kwa nini?

 • Dhama ya kutokuwa na upande wowote kabisa, hakukuelezwa kwenye sharia za Tanzania, na kutokana na hali hiyo, kaishughulikiwi kabisa hakuna sera au mswada wa sheria inayosubiri kuhusu suala hilo ili kulinda. Kukosekana kwa kanuni za usimamizi kabisa tayari kunasababisha HATARI ya kiwango cha juu kwenye wingi wa vyombo vya habari. Kama ilivyo nchini Tanzania , hakuna sharia rasmi inayolinda kutokuwa na upande wowote kabisa, thabitim halafu tunazungumzia kuhusu jinsi kanuni za kutokuwa na upande wowote kabisa zinavyoshughulikiwa.
 • Wakati kutokuwa na upande wowote kabisa hakulindwi, hata kinyume chache Kunaendelea: fukwa la mtandaoni linaathimiwa na kanuni zilizotekelezwa hivi karibuni (machi 2018) miongoni mwa kanuni mpya na zenye vikwazo, waendesha bligi na “ watengenezaji maudhui mtandaoni hivi sasa wanatakiwa kulipa ada ya leseni ya mwaka ya takribani #930. Kiasi hicho ni cha juu kuliko “GDP per capita” ambayo ilikuwa takribani kiasi hichohicho mwaka 2017 kwa mujibu wa benki ya Dunia.
 • Kanuni hizi zinaatofautiana na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu kwa ajili ya kulinda haki za uhuru wa kujieleza mtandaoni, MCT imesema. Wanazuia zaidi uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza kwa jumla kupitia udhibiti usio wa lazima, kukatazwa kutaja jina, masharti ya usajili wa waendesha blogi na majukwaa ya mtandaoni, maudhui ya mambo mbalimbali yaliyopigwa marufuku, na kutolewa kwa mamlaka ya usubihishi kuingilia hati uhuru wa raia kujieleza pale kanuni hiyo inapotumika kwa lengo la kupunguza hotuba ya kisiasa na jamii – majukwa ya mtandao, yalifungwa, kanuni za NN kama njia ya kumalizia, kwamba athari ni za kero zaidi.
 • Wakati huo huo, kiwango sifuri ni jambo la kawaida na ndani ya mfumo wa sharia kiwango sifuri maana yake ni sera ya kupanga beiambapo watoa huduma za intaneti (ISP) wanatoa maudhui mbalimbali kwa (hasa simu) watumi9aji wa intanet bila ya kutoza data zilizotumika au kuhesabu dhidi ya mpango uliyowekwa kwa mfumo hii ni hali iliyo nchini Tanzania, waliati kampuni kubwa za simu kama Tigo au Vodacom Facebook, Instagramu, na Google bila kutumia data. Millicom – imemiliki Tigo Tanzania ,ilianza mapema na kutangaza upataji wa Facebook bure kwa walipaji wake wa tangu 2014. Siku hizi. kampuni zote maarufu za simu za mkononi zinatoa aina hizo za ofa.
 • Kwa nini nini kiwango sifuri ni tatizo? upataji bure wa huduma zako uzipendazo inakuwa kama ndoto, hasa hivyo, kiwango cha zero kinaweza kutoa manufaa ya upendeleo kwa kuwa inawafatisha watumiaji kwenye maudhui na huduma za kiwango cha zero kwa gharama za mibadala zisizo na kiwango cha zero. Hatua hii inaharibu ushindani wa kufanya biashara kuwa ngumu kwa wanaoingia soko jipya. Kutokana na mtazamo wa maelezo ya umma, kiwango zero, kinaweza kupunguza uzoefu Intaneti, kwa kuwa kuna motisha ndogo kwa watumiaji kujaribu zaidi ya huduma zinazotolewa bure – watakaozoea Intaneti kama “ bustani yenye wigo” mwisho kiwango zero kinasaidia kubadili intaneti kutoka mazingira yasiyo na ruhusa – ambapo aina zote za waendelezaji wanatayarisha ubunifu kulingana na jinsi intanet inavyowafanyia watu na vifurushi vya kuanzia kama kampuni kubwa zinavyofanya – kuwa ile ambayo waendelezaji wanahitaji kwa ufanisi kushirikiana na ISP kanla ya kutumia teknolojia zao mpya. ISP hugeuka walinzi. Hivi ni vipengele vilivyoletwa na Electonic Frontiner Foundatio.
 • Hali tofauti hujitokeza wakati mtoa huduma za maudhui analipia gharama za data ambazo zingeghalimiwa na mtumiaji wa mwisho (data zilizodhaminiwa) ambayo haifahamiki Tanzania aidha, watumiaji wa huduma kuwakubali kwa kiasi huduma ya kiwango cha chini kwa baadhi ya maudhui (kuzuia) kwa kubadilishana na data zisizohesabiwa.

Alama:

0 kwa 11:

KUTOKUWA NA UPENDELEO WOWOTE KABISA MaelezoNdiyoHapanaNAMD
Je, sharia ya Taifa inashughulikia kutokuwa na upendeleo wowote kabisa? Lengo la swali hili ni kutambua iwapo kutokuwa na upendeleo wowote kabisa kunasimamiwa na sharia ya ndani kwa namna yoyote, pia inakusudia kuonesha makubaliano yoyote baina ya nchi, kama ilivyo kwenye EU, nan chi ambazo ni sehemu ya baraza la ulaya.X
Je, sharia za nchi zina kanuni zinazokataza kuzuia tovuti au maudhui mtandaoni?Swali hilo linatambua kiwango ambacho kanuni za kutokuwa na kanuni za kutokuwa na upendeleo kabisa kuzuia kukinga miongoni mwa sehemu muhimu za mfumo uliostawi wa kutokuwa na upendeleo wowote kabisa.X
Je, sheria ya taifa ina kanuni zinazokataza kuzuia huduma au maudhui yanayotolewa mtandaoni?Swahili linatambua kiwango ambacho kanuni za kutokuwa na kanuni za upendeleo kabisa kuzuia kukinga miongonini mwa sehemu muhimu za mfumo ulistawi wa kutokuwa na upendeleo wowote kabisa.X
Je sheria ya taifa ina kanuni zinazokataza kiwango zero na/au kipaumbele kilicholipiwa? Swali hili linatamkwa kiwango ambacho kanuni za nchi za kutokuwa na upendeleo wowote kabisa kuzuia kiwango ziro (ambacho kipaumbele kilicholipiwa ni mtindo wa kawaida) miongoni mwa sehemu muhimu za mfumo uliostawi wa kutokuwa na upendeleo wowote kabisa. X
Pale ambapo kutokuwa na upendeleo wowote kaboisa kunalindwa kisheria, je mfumo wa sheria unatambua jamb la kipekee kwa mfano kwa usimamizi wa mtandao unaofaa? Swali hili linaonesha ni wakati gani upungufu unaofaa unawekwa kwenye kulinda kutokuwa na upendeleo wowote kabisa ikilinganishwa na upungufu mwingine unaoweza kuzuia ufanisi wake.X
Kanuni zinazokataza au kuzuia kiwango ziro zinatekelezwa kwa mafanikio kipaumbele kinacholipiwa hakujafanyika.Swali hili linakusudia kuongeza upeo ambao hutokea kipaumbele kilicholpiwa licha yakukatazwa kisheria idadi ya nchi zenye kutuhumiwa kuwa na kinga ya kiwango ziro thabiti inayopata hali hii kiashirio hiki kinaweza kutoa mwanga kuhusu kiwango cha tofauti baina ya sheria na desturi zilizopo.X
Kanuni zinazokataza au kuzuia kiwango ziro zinatekelezwa kwa mafanikio hakuna aina nyingine za kiwango ziro zinazofanyika.Swali hili linakusudia kuongeza upeo ambao hutokea kipaumbele kilicholpiwa licha yakukatazwa kisheria idadi ya nchi zenye kutuhumiwa kuwa na kinga ya kiwango ziro thabiti inayopata hali hii kiashirio hiki kinaweza kutoa mwanga kuhusu kiwango cha tofauti baina ya sheria na desturi zilizopo.X
Kanuni zinatekelezwa kwa mafanikio kuzuia au kukatazwa hakufanyik. Swali hili linataka kutambua jinsi mfumo wa sheria uliyopo kulinda kutokuwa na upande wowote kabisa unavyofanyakazi kwa vitendo kuhusiana na kuzuia au kukatazwa. X
Je, kuna vyombo vya usimamizi au vingine vyenye jukumu lakufuatilia na kuhimiza ulinzi wa kutokuwa na upande wowote kabisa? Swali hili linaeleza kwa muhtasari iwapo kuna mamlaka yenye jukumu la kuhimiza ulinzi wa kutokuwa na upande wowote kabisa. X
Je, vikwazo vimewekwa kwa ukiukaji ulinzi wa kutokuwa na upande wowote kabisam pale zinapokuwep? Swali hili linaweza kuonesha kiwango ambacho ukiukaji wa kanuni za kutokuwaupande wowote kabisa zinachukuliwa kwa dhati kama suala la sheria na utashi wa kisias. X
Je, taratibu za uhimizaji sheria zipo kubainisha na kushughulikia ukiukaji wa kutokuwa na upande wowote kabisa zinazoonekana kama zenye ufanis? Swali hili linaonesha kiwango ambacho kanuni za kutokuwa na upande wowote kabisa kutimiza malengo yao? X
Jumla

Marejeo:

- Legal Assessment

- https://www.iafrikan.com/2018/03/23/tigo-tanzania-has-zero-rated-uber-for-its-subscribers/

- https://www.eff.org/de/node/90420

- https://www.berec.europa.eu/eng/netneutrality/zero_rating/

Chanzo

Media Ownership Monitor Tanzania (2018). Legal Assessment
The United Republic of Tanzania (2017). Media Service Regulations.
The United Republic of Tanzania (2016). Media Services Act
The United Republic of Tanzania (1976). Newspaper Act of 1976
The United Republic of Tanzania (2018). Electronic and Postal Communications Act.
The United Republic of Tanzania (2003). Tanzania Communications Regulatory Authority Act.
The United Republic of Tanzania (2017). The 2017 Budget Statement and Economic Policy.
Berec (2018). What is zero-rating? Accessed on 14 November 2018.
Tobor (2018). Tigo Tanzania has zero-rated Uber for its subscribers. Accessed on 14 November 2018.
Mc Sherry, Malcolm & Walsh (2016). Zero Rating: What it is and why you should care. Accessed on 14 November 2018.

 • Project by
  Media Council of Tanzania
 •  
  Global Media Registry
 • Funded by
  BMZ