Mambo ya Umiliki wa Vyombo vya Habari
Vyombo vya habari vya umma vinashawishi namna haja zinavyoonekana na kujadiliwa katika jamii. Uhuru wa wingi wa vyombo vya habari, maoni ya umma na mawazo – ikiwemo kuwakosoa watu waliyoko madarakani ni kanuni za usimamizi wa demokrasia kamali. Ufuatiliaji na uhakikishaji umiliki wa vyombo vya habari ni hatua ya kwanza kupata uhuru na kujichagulia, Je, watu watatathmini vipi kuaminika kwa taarifa iwapo hawajui ni nani anayetoa taarifa hiyo? Je, waandishi wa habari wanawezaje kufanyakazi kwa usahihi iwapo hawajui nin nani anayedhibiti kampuni husika wanayoifanyia kazi? Je, mamlaka za vyombo vya habari zinawezaje kushughulikia wingi wa kupindukia wa vyombo vya habari, iwapo hawajui ni nani hasa wanaoongoza chombo hicho?
Muundo wa umiliki unaweza kuathiri pia namna tasnia ya vyombo vya habari inavyosimamia rasilimali zake. Inajenga nguvu ya kiuchumi na ufanisi wa sekta ya vyombo vya habari, ambayo ni muhimu zaidi kwa wawekezaji.
KANUSHO: Kuzuia upatikanaji wa data
Kama ilivyo kwa nchi nyingi za mradi MOM imekusanya, kuthibitisha na kuchanganua seti kubwa ya data za soko la vyombo vya habari Tanzania ambalo tovuti hii inazingatia. Hata hivyo sheria ya kipekee ya Tanzania inasimamia uchapishaji wa data za kitakwimu na kulazimisha kupata idhini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kabla ya kuchapisha. Tumeomba idhini hiyo kuelekea mwisho wa utafiti. Mpaka sasa hatukupata jibu kutoka NBS. Kwa hiyo, tumelazimika kutochapisha data mahususi za hadhira. Tutatoa data kama tulivyofanya katika miradi mingine ya MOM zaidi ya 15 ya nchi mara tu NBS itakapotushauri kuhusu jambo hili.
Tabia hiyo ya ukiritimba na udhibiti wa ubadilishanaji wa wazi wa data za utafiti husababisha hatari ya kiwango cha hali ya juu kwa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, inazuia utafiti wa kisayansi na uandishi wa habari za data wa kitaalamu.