Kanzi data ya Binafsi
Mambo mawili yanafurahisha sana unapoangalia wamiliki wa hisa mmoja mmoja, waasisi, mameneja wa vyombo vya habari; Wakati Watanzania matajiri wanawakilishwa zaidi, idadi ya wamiliki wanawake na mameneja wa vyombo vya habari ni takriban sifuri.
Wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania wanabiashara nyingine nyingi
Hazinadata ya wamiliki inaonesha wamiliki watatu ambao pia wametokea kwenye orodha ya “The Forbes Top 5 of richest Tanzanians:
- Rostam Aziz – bilionea wa kwanza kutoka Tanzania mwenye biashara za Kampuni za simu, Uchimbaji madini na usafirishaji kwa meli. Bado ana hisa Vodacom Tanzania na anahusika na New Habari (2006). Aliwahi kuchaguliwa mbunge mwaka 1993 na kuwa mbunge vipindi viwili. Aliacha siasa mwaka 2011 kuzingatia biashara.
- Said Salim Bakhresa – ni milionea aliyejitengeneza kwa kuanzisha kampuni ya kutengeneza nafaka na utengenezaji vyakula, ameunda umaarufu wa Bakharesa Group. Alizindua Azam TV na huduma za kulipia TV, Afrika Mashariki. Hivi sasa Bakharesa Group ni miongoni mwa mkusanyiko mkubwa wa kampuni, Afrika Mashariki, anayeajiri zaidi ya wafanyakazi 5000 na uzalishaji wa vyakula na vinywaji baridi, ufungashaji, huduma za boti za usafiri na biashara ya mafuta.
- Dr. Reginald Mengi – alikuwa mhasibu ambaye ameanzisha na sasa ni mwenyekiti wa IPP Group inaendesha magazeti 10 ya kitaifa na vituo 2 maarufi vya Televisheni Afrika Mashariki (EATV na ITV), na kiasi cha vituo 10 vya redio. Biashara zake pia zinajumuisha utiaji vinywaji kwenye chupa na uchimbaji dhahabu.
Utajiri unaohusiana na umiliki wa vyombo vya habari si lazima uwe ni tatizo. Hata hivyo kuna hatari kwamba wamiliki wa vyombo vya habari wenye ajenda za biashara wanaweza kutumia vibaya chaneli zao kwa lengo la kukuza na kuwezesha kampuni nyingine kwa kisingizio cha maudhui yanayofaa kwa jamii.
Jinsia na Vyombo vya Habari – a mada iliyopuuzwa kisiasa
Utafiti unaunga mkono jamii ya kiraia kile ambacho imekuwa ikilalamikia kwa muda mrefu: wamiliki hisa wanawake wa vyombo vya habari na mameneja hawawakilishwi vyakutosha:
- Kwa mwanamke mmoja mwenye hisa nyingi – Dkt. Lilian Mtei mwenye hisa 75% kwenye Freeman Media. Anafanyakazi ya udaktari na mke wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
- Kuna wamiliki sita wa hisa chache. Watano kati yao wanahusiana na JosephKusaga: Judith Violet Kusaga, Sheba Martha Kusaga, Joyce Alex Kusaga, Alex Justine Kusaga, Prisca Mkama Kusaga ambao wote wana hisa chache kwenye Clouds Entertainment. Justina Antoine Ciza ni mmiliki mwenza wa E-FM Company Limited.
Data zilizopo haziruhusu matamko yenye uhakika kuhusu uwiano wa mwanamke kwa mwanaume kwa wajumbe wa bodi au hata maripota wenye uwiano wa wanaume kwa mwanamke kwenye vyumba vya habari. Hii inahitaji utafiti zaidi na uwazi kwa vyombo vya habari kusaidia utafiti wa aina hiyo. Data zilizopo hata hivyo zinaonesha hatua inahitajika kuchukuliwa kubadili hali hiyo. Mpaka sasa, utashi wa kisiasa bado ni mdogo. MCT pamoja na wadau wengine wa vyombo vya habari wamependekeza hatua ya sera kuhusu usawa wa jinsia kwenye vyombo vya habari tangu 2001. Ilikuwa miongoni mwa mapendekezo 18 – na moja kati ya matatu tu, ambayo watayarisha sera hawakuyachukua. Inaelekea mpaka sasa kuna hali ya kutokuwa tayari kushughulikia suala hilo.