This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/12/11 at 06:26
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Maswali yalioulizwa mara kwa mara

1. Ufuatiliaji wa Umiliki wa Vyombo vya Habari (MOM) ni nini?

Ufuatiliaji wa Umiliki wa Vyombo vya Habari (MOM) imetayarishwa kama zana ya ubainishaji  ili kuunda kanzidata inayopatikana kwa umma na inayohuishwa mara kwa mara yenye kuorodhesha wamiliki wa vyombo vya habari vya umma  muhimu vyote –  sekta za magazeti, redio, televisheni na vyombo vya kimtandao.

MOM inakusudia kutoa mwanga kuhusu hatari kwa wingi wa vyombo vya habari zinazisababishwa na wingi wa umiliki wa vyombo vya habari (kwa taarifa zaidi: Njia). Ili kuelewa sifa bainifu za kitaifa na kugundua vipengele vya uongezaji au upunguzaji hatari wa wingi wa vyombo vya habari, Ufuatiliaji wa Umiliki wa Vyombo vya Habari (MOM) pia inatathmini ubora wa hali ya soko na mazingira ya kisheria.

2. Je, muasisi wa MOM ni nani??

MOM imependekezwa na kuzinduliwa na Reporter ohne Grenzen e. V. – idara ya Ujerumani ya Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Maripota Wasio na Mipaka (Reporters sans frontières, RSF), linalokusudia kutetea uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupasha habari na kupata habari mahali popote duniani.

Katika kila nchi, RSF inashirikiana na shirika mbia la nchi. Nchini Tanzania, RSF limefanya kazi na Baraza la Habari Tanzania, MCT.Mradi unafadhiliwa na Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano ya Shirikisho la Ujerumani, BMZ.

3. Where can I download this report?

The website affords a PDF download containing all website content. The PDF is automatically generated and thus updated on a daily base. It exists for all website languages. In order to generate the PDF, scroll down to the website footer, choose your preferred language and “Download complete website as PDF”.

4. Kwa nini uwazi wa umiliki wa vyombo vya habari ni muhimu?

Wingi wa vyombo vya habari ni kipengele muhimu kwa jamii zenye demokrasia kuwa huru, zinazojitegemea na vyombo vya habari tofauti kuonesha maoni tofauti na kuruhusu ukosoaji kwa watu walio madarakani. Hatari ya mawazo mbalimbali husababishwa na wingi/mrundikano wa soko la vyombo vya habari, pale ambapo vyombo vya habari vichache vinatumia ushawishi mkubwa kwa maoni ya umma na kuweka vikwazo vya kuingia kwa vyombo vingine vya habari  na mitazamo (wingi wa umiliki wa vyombo vya habari). Kikwazo kikubwa cha kupambana nacho ni ukosefu wa uwazi wa umiliki wa vyombo vya habari: Je, watu wanawezaje kutathmini kuaminika kwa taarifa, iwapo hawajui ni nani anayetoa taarifa hiyo? Je, waandishi wa habari watawezaje kufanyakazi vizuri iwapo hawajui ni nani anadhibiti kampuni wanayoifanyia kazi? Je mamlaka ya vyombo vya habari yanawezaje kukabili wingi wa vyombo vya habari uliokithiri, iwapo hawajui ni nani anayeongoza vyombo vya habari?

Kwa hiyo, MOM inakusudia kujenga uwazi na kujibu swali la “ni nani hatimaye anadhibiti mauthui ya vyombo vya habari? Ili kuongeza uelewa wa umma, msingi wa ukweli kwa ajili ya uraghibishiili kuwawajibisha wanasiasa na wachumi kuhusu hali iliyopo sasa.  

Wakati tunapozingatia uwazi kama sharti la lazima la kuimarisha wingi wa vyombo vya habari, tunaandika kuhusu uwazi wa kampuni za vyombo vyahabari kutoa taarifa za muundo wa umiliki wao. Kutokana na majibu yao, tunatofautisha viwango mbalimbali vya uwazi vinavyooneshwa kwa kila aina ya chombo cha habari na kampuni yake kwenye wasifu wao.

Sababu ya wamiliki wa vyombo vya habari kuendelea kuficha au hata kudanganya uwekezaji wao inaweza kutofautiana kutoka kuwa halali hadi kutokuwa halali na kung’ang’ania sababu za kibinafsi za kisheria au za kibiashara; au mchanganyiko kwa sababu zote zilizotajwa, na katika baadhi ya matukio hujumuisha makosa ya jinai kama vile kukwepa kodi na kuvunja sheria dhidi ya uaminifu.

Baadhi ya sababu hizi ni pamoja na:

  • Katika nchi nyingi, umiliki wa vyombo vya habari unadhibitiwa na sheria ili kuepuka wingi wa vyombo vya habari. Kwa hiyo iwapo mtu mmoja anataka kupanua wingo wa vyombo vyake vya habari zaidi ya ukomo uliyowekwa, wamiliki wasio wa moja kwa moja au kampuni zilizosajiliwa nchi za nje zinazofanyakazi nchini au hata kampuni zilizosajiliwa nchini zinazofanyakazi nchi za nje hutumiwa mara kwa mara.
  • Wakati mwingine, wamiliki wa vyombo vya habari wanapata vitisho binafsi au wanakabiliwa na hatari nyingine ama kutoka serikalini au kwa kampuni shindani na kwa hiyo huamua kubaki kutofahamika ili kujilinda wenyewe.
  • Mara nyingi, umiliki wa vyombo vya habari umefungamana na mslahi ya kisiasa au kiuchumi yaliyokithiri, na wakati mwingine watu wanaohusika ni viongozi wa serikali wasiotaka kueleza mgongano huo wa kimaslahi.
  • Kwa nadra sana, udanganyifu wa umiliki wa vyombo vya habari hutokea pasipo kukusudia kwa sababu kadri muda unavyopita na kupitia uunganishaji na ununuaji, miundo ya shirika imekuwa tata kiasi cha kushindwa kutambua ni nani hasa mmiliki halali.
  • Mwisho lakini si kwa umuhimu, kuna sababu za “kawaida” – yaani zisizohusiana na vyombo vya habari kwa wamiliki kuficha, kama vile ukwepaji kodi

5. Je, aina gani ya sheria ya wingi wa vyombo vya habari ambazo MOM inapendekeza?

MOM haitoi matamko sanifu – haupendekezi jinsi ya kusimamia umiliki wa vyombo vya habari. Mfumo wa usimamizi wa wingi wa vyombo vya habari unaoweza kufanya kazi, hutegemea muktadha wa nchi, sheria zilizopo na hali ya soko na mandhari ya umiliki. 

MOM inatoa zana ya uwazi kuhimiza majadiliano ya kidemokrasia kuhusu suala hilo pamoja na uamuzi wa utawala bora, huenda ikawa ya hali ya juu na kuweza zaidi kuonesha mahitaji na matakwa ya watu iwapo wanapata taarifa za kutosha na ushauriano mpana, wenye maoni na mapendekezo yanayotolewa kwa uhuru.

6. Je, taarifa na takwimu zinakusanywaje na kuhalalishwa?

Kwa kawaida, vyanzo vya taarifa na takwimu rasmi, na au vyanzo vyenye kiwango cha juu cha kuaminika na kuaminika vinatumika. Pale ambapo taarifa hazipatikani kwa urahisi, taarifa hizo huombwa na kampuni za vyombo vya habari kutoka kwa wawakilishi wa kisiasa na taasisi za utafiti. Vyanzo vyote vya habari huandikwa na kuhifadhiwa kwa makini maktaba. Taarifa zaidi zinapatikana MCT iwapo zitaombwa.

Taarifa na takwimu za magazeti, TV na Redio, MOM imeshirikiana na GeoPoll Tanzania Audience DataRadio/TV, Q2 2018; Online/Print, Sep 2018). GeoPoll ni shirika kubwa la utafiti kwa njia mtandao duniani, lenye zaidi ya watumiaji 200 milioni barani Afrika na Asia. MOM ilinunua taarifa na takwimu kwa bei nafuu ya shirika lisilo la kiserikali.

Kwa taarifa kuhusu kampuni za vyombo vya habari, inayopatikana kwa umma ilitolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),ambako vyombo vya utangazaji na mtandaoni  vinapaswa kusajiliwa. Wakati mwingine, wanahisa wa vyombo hivyo vya habari walisajiliwa huko.

Taarifa kuhusu wanahisa, wamiliki n.k, ziliombwa kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji Leseni (BRELA) baada ya kulipia ada ya (sh. 22,000/ca. 10$)

Ili kuhakikisha na kuhakiki lengo la tathmini, MOM ilishirikiana na kikundi cha ushauri kilichotoa maoni na kushauriana kupitia mchakato wa utafiti. Kikundi hicho kiliundwa na wataalamu wa kitaifa wenye maarifa ya kutosha na uzoefu katika Nyanja za vyombo vya habari na mawasiliano. Miongoni mwa wataalamu hao, wafuatao walifuatilia mchakato wa utafiti:

7. Je, “chombo cha habari kinachohusika zaidi” ni chombo cha aina gani?

Swali muhimu ni kwamba: ni chombo gani cha habari kinachoshawishi mchakato wa kuunda maoni? Ili kuchuja vyombo vyote vya habari vinavyohusika, tulijumuisha aina ya vyombo vya habari vilivyozoeleka (magazeti, redio, TV na mitandaoni). Vyombo hivi vilichaguliwa kulingana na vigezo vifuatavyo:

  • MOM ilizingatia zaidi chombo cha habari kinachofikika zaidi, kwa kuangalia wingi wa hadhira. Msingi wa uchaguzi ulikuwa taarifa na takwimu za hadhira kwa kipindi cha hivi karibuni zilizopo na zilizotolewa na GeoPoll(Radio & TV:Q2 2018; Online & Print: Sep 2018).
  • Umuhimu wa habari na maudhui ya maoni. Utafiti unalenga taarifa ya jumla inayozingatia zaidi taifa. Kwa hali hiyo, chombo cha habari kinacholenga maeneo mahususi (muziki na michezo), mitandao ya kijamii, watafiti na matangazo havikuhusishwa.
  • Uchaguzi wa vigezo hivyo kimsingi kwa kuanzia vilihusu wastani wa vyombo vya habari kumi kwa kila aina (TV, magazeti, mtandaoni). Kwa kutoa mwanga kwa vyombo vya habari hivi vinavyohusika zaidi, tayari kuna ruhusu tabia bayana katika wingi wa vyombo vya habari. Vyombo vya habari vingi zaidi vitaongezwa – kama vitathibitisha kuhusika kwa mujibu wa umiliki au ushawishi wao kwa maoni ya umma (soma zaidi kuhusu – “Je, vyombo vya habari vinavyochaguliwaje?”)

8. Je, vyombo vya habari vinachaguliwaje?

Vituo vya TV vilichaguliwa kutokana na ufikiaji wao wa hadhira nchini kote, kwa mujibu wa GeoPoll (Q2 2018). GeoPoll ni mtoaji mkubwa wa viwango vya habari usiku kucha barani Afrika, ikitoa utambuzi wa taarifa na takwimu wa kila siku, siku 356 kwa mwaka. Huduma ya Upimaji wa vyombo vya habari hutumia utafiti kwa simu za mkononi kwa njia jopo kukusanya taarifa na takwimu za hadhira kwa sampuli ya watu 2000 kwa nchi kwa siku, vikiwemo vituo vya TV vya kitaifa na vya kidijiti pamoja na vituo vya TV vya kimataifa.

Vituo vya redio vilichaguliwa kwa kutumia ukusanyaji taarifa na takwimu wa GeoPoll (Q2 2018). Ni vituo vya redio vyenye usikilizwaji muhimu pekee nchi nzima ndivyo vilivyohusishwa. Vituo vya redio vya mikoa pia vilijumuishwa kwa kuwa vinamilikiwa na mwenye mtandao nchi nzima wa vituo vya mikoa ambavyo kwa pamoja hufikia hadhira muhimu.   

Kwa Magazeti na Vyombo vya mtandao, GeoPoll ilitoa utafiti kwa simu (Agosti 30 – Septemba 1, 2018) kwa MOM, ikiomba iwapo ndivyo, ni magazeti au tovuti zipi zilitumika siku 30 za mwisho. Utafiti ulipokewa zaidi maeneo ya mijini, kutoka kwa wanaume zaidi na watu wa umri wa kati. Taarifa hii ilikokotolewa na viwango vya Alexa na utafiti wa des...

Kwa uchaguzi wa magazeti, tulitoa yale magazeti yaliyokuwa yakiripoti habari za michezo michezo au burudani tu (kwa mfano, Mwanaspoti, Championi, Dimba n.k). Kwa soko la mtandaoni hasa tovuti za habari na mijadala ziliangaliwa kwa sababu zilijengenga maoni ya umma. Mitandao ya kijamii (mfano. facebook, Instagram), vibanda vya mtandao na tovuti za matangazo (kwa mfano Tovuti ya Ajira) havikujumuishwa, kwa kuwa havikuwa na uhusiano unapangalia maudhui ya uhariri na umiliki. 

9. Kwanini Tanzania?

Mbia imara wa nchini kama Baraza la Habari la Tanzania (MCT) ndilo msingi wa mafanikio ya utekelezaji na vigezo vya uchaguzi vinavyohusika zaidi. 

Tanzania ni ya 93 (kati ya nchi 180) kwenye Faharasa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, 2018 iliyochapishwa na Reporter Without Borders, inayopanga mataifa kulingana na viashirio kama vile Uhuru wa Vyombo vya Habari, kujidhibiti, kutii sheria, uwazi na ukiukaji wa maadili. Tangu rais Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015, Tanzania imeshuka kwa nafasi 18 kutokana na sababu kama vile wimbi la sheria mpya zilizosababisha ukandamizaji wa vituo vya redio na magazeti binafsi. Utafiti kama vile wa FES Media Barometer Africa Tanzania (2015) umeeleza kuwa waandishi wa habari wa Tanzania  wanajiskia kukandamizwa na sheria za vyombo vya habari pamoja na maslahi yenye nguvu ya wamiliki wa vyombo vya habari mbalimbali, view vinaendeshwa na watu binafsi au serikali. Hakuna sheria yoyote inayozuia wingi wa vyombo vya habari na ukiritimba au umiliki mtambuko nchini Tanzania. Yote haya yanafanya umiliki wa vyombo vya habari kuwa mada muhimu sana ya kuangaliwa nchini Tanzania. 

10. Je, MOM ipo nchini Tanzania tu?

MOM iliundwa kama njia ya msingi inayoweza kutumika kokote duniani na itabaki kuwa hivyo. Bila kujali kuwa mienendo ya wingi wa vyombo vya habari inaonekana duniani kote; utekelezaji na uchambuzi utaanza kwanza katika nchi zinazoendelea.  MOM imekuwa inatekelezwa katika nchi zaidi ya 20 duniani katika kipindi cha miaka mitatu. Miradi yote ya nchi inaweza kupatikana kwenye global website.

11. Je, kuna changamoto gani kuu za utafiti huu?

  • Hakuna taarifa na takwimu za kiuchumi: Wingi wa soko zinazotokana na kiasi cha soko haziwezi kukokotolewa kwa sababu hakukua na idadi kamili na inayoaminika kwa umma. Baadhi ya magazeti yamezieleza baada ya kuombwa ambazo kwa kweli zimeoneshwa kwenye wasifu wa chombo chao wa habari.
  • Hakuna taarifa na takwimu rasmi za hadhira zinazopatikana kwa umma – zinauzwa na kampuni za utafiti
  • Ingawa taarifa na takwimu kwa ajili ya umiliki wa shirika zipo BRELA, upataji wake unaweza kuwa ghali na wenye usumbumbu

12. Je, tunamlenga nani?

Kanzi data

  • Humwezesha kila raia kufahamishwa kuhusu mfumo wa vyombo vya habari kwa jumla.
  • Hujenga msingi wa ukweli kwa juhudi za uraghibishi wa jamii kuzidi kuhamasisha uelewa wa umma kuhusu umiliki na wingi wa vyombo vya habari;
  • Huwa kama mahali pa marejeo kwa ajili ya kushauriana na mamlaka za ushindani au vyombo vya serikali wakati wa kuanzisha hatua za usimamizi wa kisheria zinazofaa kulinda wingi wa vyombo vya habari 

13. Je, nini kinafuata?

Kanzi data hutoa picha ya hali ya sasa yenye maudhui ya ukweli wa kihistoria. Itahuishwa mara kwa mara na Baraza la Habari la Tanzania (MCT).

14. Je, kuna miradi mingine?

MOM inachochewa zaidi na miradi mingine  miwili. Hasa viashirio vya viwango vya baadae hutegemea zaidi  Media Pluralism Monitor inayofadhiliwa na EU ya Centre for Media Pluralism and Media Freedom (CMPF) katika European University Institute (EUI, Florence). Vile vile Media Pedia, kanzi data ya umiliki iliyotayarishwa na waandishi wa habari za uchunguzi nchini Macedonia imekuwa kama kichocheo cha MOM.  Muhtasari wa miradi mingine unaweza kupatikana kwenye jedwali lifuatalo:

ORGANIZATION

DESCRIPTION

Access Info 

A Spanish NGO that works in the field of media ownership transparency in several European countries.

Article 19

An NGO which works in the field of press freedom. It implements media concentration projects.

Deutsche Welle

The Media Freedom Navigator of Deutsche Welle provides an overview of different media freedom indices. 

European Audiovisual Observatory

A database of television and audiovisual services in Europe.

European Journalism Center

 

The Website provides a summary and analysis of the state of the media in Europe and neighbouring countries.

European University Institute in Florence

The Media Pluralism Monitor assesses risks for media pluralism in the EU Member States.

IFEX

The network provides information of the state of the media in many countries.

IREX

The Media Sustainability Index (MSI) provides analyses of the conditions for independent media in 80 countries.

mediaUk

The Website provides information about media ownership in Great Britain.

Pew Research Center

The organisation publishes an interactive database about media in the United States.

SEENPM

Monitors media ownership and the impact on media pluralism in southeastern Europe and EU member states.

The Columbia Institute for Tele-Information at Columbia Business School

A research that works with authors from 30 countries in the world about media concentration using a common methodology.

The Institute for Media and Communication Policy

A database of international corporations of the world´s biggest media.

UNESCO

Media Development Indicators - A framework for assessing media development.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ