Uwingi wa Vyombo vya Habari
Je, mandhari ya vyombo vya habari vya Tanzania yanaonesha wingi na iwapo ndiyo, ni imara kiasi gani? Je, sheria ya sasa inalinda vizuri kiasi gani wingi wa vyombo vya habari? Je, ni hatari gani kubwa kwa mkusanyiko wa vyombo mbalimbali vya habari vinavyojumuisha sauti zote, maoni yote, ikiwemo kuwalaumu watu waliyoko madarakani? Viashirio hivi kumi vinatoa baadhi ya mwanga kuhusu hatari zinazokabiliwa na vyombo vya habari huru na zinazoweza kuweka wingi wa vyombo vya habari vya Tanzania hatarini.