Jamii
Tanzania inajivunia kuwa na zaidi ya makabila 130, kila moja likiwa na utamaduni na lugha yake. Watanzania wawili kati ya watatu katika takribani watu 57.3 milioni ni Wakristo, wakati kila mtu wa tatu ni Muislamu. Kwa dini za matambiko, ni asilimia 1.8 tu ndio wanaoabudu siku hizi. Ingawa zaidi ya 70% ya watu wanaishi maeneo ya vijijini, vyombo vya habari vipo Dar es salaa, kitovu cha siasa na uchumi. Magazeti yanasambazwa zaidi maeneo ya mijini lakini redio ndizo zinazosikika mikoani. Hali hii pamoja na kiwango cha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu cha takribani 78% kinachangia jinsi Watanzania wanavyotumia habari: wengi wao wanafikia redio, baadhi yao wanamudu na kufikia TV, na wachache ndio wanaoweza kupata magazeti.
Vyombo vya Habari hutumia Kiingereza na Kiswahili
Ingawa zaidi ya lugha 100 zipo nchini, serikali ya Tanzania inatumia sera ya lugha inayowezesha Kiingereza na Kiswahili zote kuwa lugha rasmi, wakati Kiswahili ni lugha ya taifa. Kiswahili kinatumika katika utawala, elimu (elimu ya msingi) na mawasiliano ya umma. Hadhi ya Kiswahili inamisingi ya kiistoria kwa sababu Kiswahili ni nyenzo ya mshikamano; imekusudiwa kuunganisha na kuwa utambulisho wan chi yenye makabila mbalimbali. Hivi sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache katika kusini mwa Jangwa la Sahara, magazeti mengi yanachapishwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo wasomaji wote wanajua kusoma na kuandika. Katika nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, hasa magazeti bado yanatumia lugha za kikoloni – Kiingereza, Kifaransa au Kireno. Vipindi vingi maarufu vya redio na TV vinatayarishwa kwa Kiswahili pia.
Kudhoofisha kuungwa mkono kwa vyombo vya habari na umma
Mwaka 2013, theluthi mbili ya za watu wanajitambulisha kuwa wanapenda sana habari na wanaelewa waziwazi kwamba vyombo vya habari vya Tanzania vimekuwa bora. Kwa upande mwingine wanakosoa utaalamu na wingi wa maudhui yaliyopokewa kuwa ni dhaifu katika aina zote tatu za vyombo vya habari. Hata hivyo, kwa mujibu wa utafiti wa Ipsos/ TMF Tanzania Media Fund, Watanzania wanafurahia nafasi ya vyombo vya habari kusimamia mwenendo wa serikali: wanaamini kwamba vyombo vya habari ni lazima viiwajibishe serikali kwa kuwafahamisha serikali inafanya nini. Uungwaji mkono huu wa wananchi unaelekea kudhoofika.
Katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano iliyopita, idadi ya watu wanaofikiria kuwa vyombo vya habari vina haki ya kuchapisha maoni na mawazo yoyote bila kudhibitiwa na serikali inazidi kupungua siku hadi siku. Kwa mujibu wa Afrobarometer 2017, hali ni tofauti: 56% wamekubaliana au kukubaliana sana kuwa “serikali inayo haki ya kuzuia vyombo vya habari visichapishe mambo inayoona kuwa yanaathiri jamii.” Wakati huo huo, wananchi wachache (46%) wanahisi kuwa huru kutoa maoni yao.
Kwa kuangalia bara la Afrika kwa jumla, hata hivyo imani kwa vyombo vya habari inaonesha kuzidi imani ya vyombo vya habari katika nchi zilizoendelea zenye viwanda na demokrasia, na ni sawa au inazidi kidogo imani kwa taasisi nyingine za taifa. Tafiti mbalimbali zimebaini kuwa uthibitisho kwa ajili ya hali hii – kwa kuzingatia tafiti hizo inaweza kulinganishwa kwa tahadhari tu hali ya kuwa wanaonesha tofauti kwa jinsi swali lilivyoandikwa na vipindi vya utafiti.
Chanzo
The World Bank. Population, total, Tanzania. Accessed 20.08.2018
Martin Sturmer (2008). The Media History Of Tanzania. p.1. Ndanda Press, Songea.
Press Reference (2018). Tanzania. Accessed on 22 October 2018.
Afrobarometer (2018). Do East Africans still want a free media?. Accessed on 22 October 2018.
Quartz (2015). Tanzania dumps English as its official language in schools, opts for Kiswahili. Accessed on 22 October 2018.
Naunihal Singh, Devra C. Moehler (2011). Whose News Do You Trust? Explaining Trust in Private versus Public Media in Africa.
CIA (2018). The World Facebook Tanzania. Accessed on 20 August 2018.
TMF Tanzania Media Fund (2013). Ipsos - Baseline community and decision maker media perception survey. February 2013. Dar es Salaam: Tanzania Media Fund.