This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/12/11 at 07:24
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Redio

Kanzi data ya Redio

Redio ni maarufu zaidi nchini kote. Asilimia 45 ya Wananchi wanatumia redio kama chanzo cha habari za kila siku. Watu 4 kati ya 5 wanatumia redio angalau kila mwezi kupata habari mpya. Hali hii ilioneshwa na 2017 Afrobarometer. Vituo vya Redio vinavyorusha matangazo yao kwa Kiswahili vina wasikilizaji wengi zaidi kwa Kiswahili vina wasikilizaji wengi zaidi.

Mahitaji yanatimiza Ugavi.

Mahitaji yanatimiza ugavi unaoendelea kukua: katika kipindi cha miaka michache iliyopita, idadi na kuenea vituo vya redio vinavyoendeshwa katika sehemu mbalimbali za nchi zimeongezeka haraka,ikiwemo kwenye maeneo yenye shida ya kupata magazeti na TV. Takwimu kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa kuanzia leseni za redio 86 mwaka 2012, idadi hiyo takribani imeongezeka maradufu mwaka 2017. Maendeleo kutoka kituo cha redio pekee kinacho milikiwa na Taifa na kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na serikali kabla ya kuingia kwa vyama vingi katikati ya miaka ya 1990, hadi kufikia 156 vingi vyao ni vya biashara imeonekana kuwa ni mchakato wa kupigiwa mfano uliofanywa na asasi za kiraia.

Umiliki wa wingi wa Vyombo vya Habari.

Soko la redio linalinganishwa na magazeti na TV lina mambo mbalimbali zaidi lakini bado inaonesha wingi wa wastani na wa juu wa hadhira kwa kuwa kampuni 4 za redio za juu zinawafikia wasikilizaji XX.XXX%. kama ilivyo TV, Clouds Entertainment Ltd, IPP Media Ltd na Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) inayoendeshwa na serikali, zina msimamo mzuri kwenye soko, na kila moja inaendesha vituo vingi. Sahara Medio Group Ltd, kutokea Mwanza, yenye vituo vingi vya redio na TV, inafuatia kwa upande wa kusikika na kufikia hadhira. Hakuna taarifa rasmi ya kampuni kwenye masjala ya BRELA. Taarifa zinamtaja Dkt. Anthony Diallo mwanasiasa na mbunge wa zamani, na mwasisi, na Ofisa Mtendaji Mkuu na mmliki wa kampuni hiyo.

Changamoto: Vifaa vya kiufundi na Watumishi.

Ukosefu wa uwezo wa kiufundi, ikiwemo vifaa vya Studio vya kuaminika, ni miongoni mwa changamoto kuu inayokabili utangazaji kwa redio nchini Tanzania. Hasa redio za wananchi ambazo mara nyingi huwategemea watu wanaofanya kazi kwa utaratibu wa kujitolea kwa sababu hawawezi kumudu kuajiri watumishi wa kudumu kutokana na changamoto ya kifedha. Kwa hali hizo, mara nyingi DJ wa redio wanachukua jukumu la mtayarishaji na mtangazaji, hali iliyotokana na utoaji taarifa juu juu na mziki mwingi badala ya vipindi makini vyenye maudhui, maswala yanayo wagusa wanajamii inayotarajiwa kushughulikia - kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Vyombo vya Vyombo vya Habari ya MCT, mwaka 2016.

Hii inaweza imesababisha kile ambacho utafiti wa ubora wa vyombo vya habari ya mwaka 2017, inapendekeza: habari za redio ubora wake ni wa chini ikilinganishwa na habari za magazeti na TV. Wasiwasi mkubwa ni kwamba habari za redio zinasikilizwa na sehemu kubwa ya watu.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ