Star TV

Star TV ni kituo cha TV cha binafsi kilichopo Mwanza na kinamilikiwa na Sahara Media Group inayoendesha pia vituo viwili vya redio.
Star TV ilianzishwa mwaka 2000 na hivi sasa inawatazamaji wengi hasa katika kanda ya nyanda za juu kusini. Pia ina mtandao mkubwa wa soko na gari la OB linalowezesha kutangaza mubashara vipindi vya nje ya studio.
Ni kituo cha biashara cha Free to Air, kinachotangaza kwenye majengo yote yaliyosajiliwa na TCRA. Ni miongoni mwa vituo vinavyoongoza kitaifa vilivyosajiliwa kwa kuzingatia ufikaji, hadhira na mapato ya matangazo. Vipindi vyake husikika kanda yote ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini kupitia masafa ya DIT na DTH.
Star TV ni kituo cha Saba cha TV kinachoangaliwa sana chenye XX.XXX% ya hadhira kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa GeoPoll Media Measurement Service ya 2018. Kituo hiki chenye vipindi hasa vya habari na matukio, pia hutangaza burudani, maigizo, michezo na sitcoms.
Leseni ya Star TV imesajiliwa kwa Sahara Media Group Ltd (SMG) kwa 100% - kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). SMG, iliyokuwa ikiitwa Sahara Communication na Publishing Company Ltd, ilianzishwa mwaka 1992. SMG inaendesha vyombo vitatu vya habari vya Star TV, Radio Free Africa na Kiss FM.
Data za umiliki wa SMG hazikuweza kupatikana katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji wa Leseni (BRELA). Kwa mujibu wa wasifu uliyounganishwa kwenye mtandao, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa SMG hadi sasa ni mwasisi wake Dkt. Anthony M. Diallo, alikuwa waziri katika nyadhifa mbalimbali. Kwa mujibu wa dodoso lililotayarishwa na R & D Manager wa SMG; hakuna utafiti uliyofanywa kutathmini mapato ya matangazo kwa kila kituo cha FTA. Serikali inaipa kampuni hiyo, habari na taarifa, hata hivyo haisaidii sana katika matangazo ya Taifa.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Taifa (husikika ukanda wote wa mashariki, kati na kusini kupitia masafa ya FM na AM)
Aina ya maudhui
Free to Air
Kampuni ya vyombo vya Habari
Sahara Media Group Limited
Muundo wa umiliki
Star TV inamilikiwa na kuendeshwa na Sahara Media Group Limited, ambayo hatimaye ni mali ya muasisi wake Dr. Diallo. Hakuna data zilizopatikanaBRELA.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Kampuni
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
2000
Mwanzilishi
Dr. Anthony M. Diallo - ni mwanasiasa na mwenyekiti wa chama wa mkoa wa Mwanza wa chama tawala cha Chama cha Mapinduzi (CCM). Alikuwa mbunge (1995 - Okt 2010) na kupoteza ubunge kwa mgombea wa upinzani. Alikuwa na nyadhifa mbalimbali katika baraza la Mawa
Mtendaji Mkuu
Dr. Anthony Diallo - angalia hapo juu
Mhariri Mkuu
Victor Chacha - Meneja wa Kituor. Flora Rugashololola - Mhariri wa Habari.
Mawasiliano
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).
Muhtasari wa vyombo vya habari
Research and Planning Manager, Sahara Media Group (September 2018). Media Ownership Monitor Questionnaire Sahara Media Group.