East Africa TV
EATV-East Africa Television (Channel 5) ni chaneli ya televisheni ya burudani kwa saa 24, free – to – air. Ilizinduliwa Julai 2002. Inaendesha shughuli zake kutoka Dar es Salaam, mawimbi ya matangazo yanarushwa kupitia satellite hadi Nairobi na Kampala, ambapo hutangazwa kutoka nchini.
Ripoti ya Media Measurement ya Tanzania ya GeoPoll , kwa kutumia takwimu za watazamaji za robo mwaka ya pili ya 2018 imeiweka East Africa Television (EATV) kuwa na asilimia XX.XXX% ya watazamaji. Kwa hiyo ni ya pili miongoni mwa vituo vyote vya televisheni nchini Tanzania. vipindi vya EATV vinahusu masuala mbalimbali kuanzia Habari, Matukio, Mitandao ya Maisha, Burudani na Masuala ya Kijamii.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesajiliwa kwa jina la East Africa Television na Dkt. Reginald Abraham Mengi na Agapitus Leon Ngumaas kama wanahisa kila mmoja hisa za asilimia 50 percent of the shares.EATV ina redio moja ya East Africa Radio (EA FM). East Africa redio ni redio ya kwanza ya utangazaji kikanda barani Afrika.
East Africa Television (EATV) ni kampuni shiriki ya IPP Group Limited. IPP Group Limited ni kampuni ya utengenezaji, utiaji vinywaji kwenye chupa na kundi la vyombo vya habari inayojumuisha vituo vya Televisheni, redio na magazeti. Wasifu wa kampuni uliyoombwa kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Utoaji wa Leseni (BRELA) unaonyesha kuwa Dkt Reginald Abraham Mengi na Agaptus Leon Nguma ni wanahisa wa IPP Group Limited.
Mengi alizaliwa Tanzania mwaka 1944. Yeye ni mfadhili wa Kitanzania, mwanaviwanda, mmiliki wa vyombo vya habari na mwasisi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Group. Mengi pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu FORBES, amekuwa miongoni mwa matajiri wa Afrika mwenye zaidi ya $400 milioni kwa takwimu za mwaka 2015.
Agapitus Leon Nguma alikuwa katibu wa kampuni na mwanahisa. Alifariki dunia 1 Mei 2018. Alikuwa pia Mkurugenzi wa the Guardian Ltd na Bonite Bottlers Ltd. Kitaaluma ni Mwanasheria.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Free to Air
Kampuni ya vyombo vya Habari
IPP Media Limited
Muundo wa umiliki
East Africa Television (EATV) ni kampuni shiriki ya IPP Group Limited. Ambayo pia inamilikiwa na Dr. Reginald Mengi. Mmiliki wa hisa kwa mujibu wa TCRA., Julai, 2018.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Kundi / Mmiliki Binafsi
Agapitus Leon Nguma
alisoma na kuhitimu kama mwanasheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kujiunga Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kufanyakazi kama Mwanasheria wa Serikali. Hata hivyo, baadaye alijiuzuli katika utumishi wa umma na kujiunga IPP Group ambapo alikuwa Mwanasheria wa Kampuni wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki dunia 1 Mei, 2018.
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
2002
Mwanzilishi
Dr. Reginald Mengi - ni mwanaviwanda wa Tanzania, mmiliki wa vyombo vya habari na muasisi, pia ni Mwenyekiti mtendaji wa IPP Group. Pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania. Katika taarifa za FORBES, Mengi ni miongoni mwa mt
Mtendaji Mkuu
Regina Mengi - Mkurugenzi Mtendaji. Ni binti wa Dkt. Mengi.
Mhariri Mkuu
Nasser Kingu - Mkuu wa Vipindi
Mawasiliano
East Africa TV (EATV)
P.O. Box 4370, Dar-Es-Salaam
Tel.: +255 22 2775915/6
Fax: +255 22 2775915
E-Mail: info@eatv.tv
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).
Muhtasari wa vyombo vya habari
Reginald Abraham Mengi (2018), I Can, I must, I will. ISBN-10: 9781717871749.