TBC2

TBC2 ni idhaa ya televisheni ya kibiashara ya Tanzanian Broadcasting Corporation (TBC).
Kwa mujibu wa ripoti ya Tanzania Media Measurement ya GeoPoll, kwa takwimu za hadhira za robo mwaka ya pili ya 2018, TBC2 ina hadhira ya XX.XXX%. hii ina maana kuwa ya 10 miongoni mwa vituo vya TV vya habari.
Kutokana na amri ya kuanzishwa kwa Tanzania Broadcasting Corporation ya 2007, TBC imepewa mamlaka ya kuwa na aina nne ya vyombo vya habari hasa utangazaji kwa umma, huduma za utangazaji wa kibiashara, huduma ya utangazaji kwa jamii na aina nyingine za shughuli za utangazaji kadri Waziri mwenye dhamana ya Utangazaji atakavyoona.
Katika mahojiano ya ana kwa ana (13/09/2018), Director of Radio Services amesema kuwa hivi karibuni TBC itaanza kuondoa vipindi vya biashara katika TBC Taifa na TBC1 ili ziweze kumakinikia zaidi vipindi vya masuala ya maendeleo ya taifa na matukio katika kuimarisha juhudi za serikali za ujenzi wa taifa. Director of Radio Services amesema vipindi vya biashara hivi sasa katika vituo viwili hivyo ama vinafutwa au kurekebishwa, kuvunja mikakati ya muda wa matangazo na kuondoa matangazo kwenye idhaa hizo. Hata hivyo maudhui ya TBC2 ni ya kuburudisha zaidi kuliko kuwa ya bishara.
TBC2 inamilikiwa na Tanzania Broadcasting Corporation, idhaa pekee ya utangazaji wa umma, katika Tanzania bara. Pia ni shirika la umma lililoanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1992, kutoa huduma ya utangazaji ya umma kwa njia ya redio na televisheni. Ni chombo cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusimamiwa na Msajili wa Hazina, idara ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango, yenye 100% ya hisa. Hatimaye, Serikali inatarajia kuwa msemaji wake kuliko kutangaza kwa uhuru wake bila ya upendeleo.
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Umma
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Free to Air
Kampuni ya vyombo vya Habari
Tanzanian Broadcasting Corporation
Muundo wa umiliki
TBC2 inaendeshwa na Tanzanian Broadcasting Corporation inayomilikiwa na Taifa.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Missing Data
Mwanzilishi
Serikali
Mtendaji Mkuu
Dr. Ayubu Rioba - ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC. Aliteuliwa na Rais mwaka 2016. kabla ya kuteuliwa alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma (SJMC). Ni mwandishi wa habari mtaalamu (aliwahi pia kufan
Mhariri Mkuu
Dr. Ayubu Rioba - angalia hapo juu.
Watu wengine muhimu
Rais - anateua afisa mtendaji mkuu/Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi
Waziri wa Habari - anateua wajumbe wengine wa bodi.
Waziri wa Fedha - anathibitisha bajeti ya Mwaka ya TBC
Mawasiliano
Tanzania Broadcasting Corporation
P.O. Box 9191, Dar-Es-Salaam
Tel.: +255222860760
Fax: +255 222865577
E-Mail: info@tbcorp.org
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).
Muhtasari wa vyombo vya habari
Director General, TBC (October 2018). Media Ownership Monitor Questionnaire TBC.
Director of Radio Services, TBC (September 2018). Media Owner Monitor Questionnaire TBC.
TBC (2007). TBC Establishmend Order.