This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2022/10/04 at 20:12
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Government

Government

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki Tanzania Standard Newspaper Limited (TSN) na Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) ambapo inamiliki 99% ya hisa kwenye TSN na 100% ya mtawalia , hali ya kuwa mhariri mtendaji anamiliki 1% zilizobaki katika TSN. TSN iliundwa tarehe 5 Februari 1970, wakati serikali ilipotaifisha Tanganyika Standard NewsPaper Limited iliyokuwa inamilikiwa binafsi. TSN inachapisha DailyNews na toleo lake la Jumapili la SundayNews.

TBC imeunganisha Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Televisheni ya Taifa (TVT) tarehe 1Julai 2004. Matangazo ya redio kwa umma yalianzishwa na serikali ya kikoloni ya Mwingereza, 1 Julai 1951 wakati ilipoanzishwa kituo cha Radio cha Sauti ya Dar es Salaam. Kituo hicho kilibadilishwa jina na kuitwa Tanzania Broadcasting Services (TBS) mwaka 1955 wakati matangazo yake yalienea nchi nzima. TBC ilibadilishwa jina na kuwa Tanganyika Broadcasting Corporation mwezi Julai,1956. Serikali ya kikoloni ya Mwingereza iliitumakukidhi maslahi yake ya kikoloni. Serikali ya wananchi iliyokuwa madarakani baada ya uhuru, ilitaifisha TBC tarehe 1 Julai,1965 na kuibadili jina kuwa Radio Tanzania Dar es Salaam.

Matangazo ya Televisheni kwa Umma yalianzishwa Oktoba 1999. Baada ya Uhuru Serikali haikuanzisha televisheni kwa sababu iliamini kuwa televisheni ni ghali kuianzisha na kuiendesha kwa hiyo itaanzishwa tu kama zana ya maendeleo na si alama ya hadhi au ufahari. TVT iliunganishwa na RTD na kuwa TBC mwaka 2002 kabla ya kubadilishwa jina kuwa TBC Julai 2007.

Shauku ya Serikali katika kumiliki vyombo vya habari inaanzia Mei,1961 wakati Tanzania bara ilipopewa Serikali ya Ndani ya Madaraka, iliyotayarisha utaratibu wa utawala kabla ya uhuru. Miongoni mwa uamuzi wake wa kwanza ni kubadili jina la Idara ya Uhusiano ya kikoloni, kuwa Idara ya Habari ya Tanganyika (TIS) ambayo hivi sasa ni Idara ya Habari Tanzania (TIS) maarufu kwa Kiswahili kuwa MAELEZO. Idara ya Habari ya Tanganyika mpya iliyoanzishwa iliwekwa moja kwa moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,na wakati huo Waziri Mkuu alikuwa Nyerere akawa mfawidhi wa sekta ya Habari. Pia ilianzisha jarida la Habari la kila mwezi la Kiswahili lijulikanalo kuwa NCHI YETU.

Kati ya 9 Desemba, 1961- wakati nchi ilipopata uhuru na 5 Februari 1967 wakati Tanu ilipozindua Azimio la Arusha, waraka rasmi wa mpango wa sera ya Serikali ya Ujamaa na Kujitegemea – wakati huo serikali haikuwa na sera ya wazi kuhusu vyombo vya habari, licha ya kutumia vyombo vya habari kufanya mabadiliko kuhusu ujenzi wa Taifa. Maeneo matatu ambayo serikali imekusudia katika ujenzi wa Taifa utakaoleta mchango chanya ni uunganishaji Taifa, maendeleo ya uchumi, jamii na kuhifadhi na kukuza utamaduni.

Baada ya kupitishwa kwa Azimio la Arusha, athari ya Serikali kwa vyombo vya habari imezidi kushawishiwa chamba cha TANU kilochoiweka madarakani. Serikali kwa kushirikiana na TANU ilichukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa vyombo vya habari navyo vinajituma kwa dhati kufanikisha azimia ya serikali. Hatua hizo ni pamoja na kupanga na kuendesha semina mbalimbali kwa watumishi wa vyombo vya habari ambapo walipewa mihadhara kuhusu jukumu la vyombo vya habari katika kujenga ujamaa na kujenga Taifa, kuwakutanisha watumishi wa vyombo vya habari vya TANU/CCM na vinavyomilikiwa na serikali ambavyo walitakiwa kuhudhuria mafunzo ya miezi 3 hadi 9 ya itikadi kwenye vyuo vya itikadi vya chama. Wakati wa mafunzo haya watumishi walifahamishwa itikadi na falsafa ya chama na hivyo kupata dhana ya sita ya nini kichapishwe na nini kisichapishwe na kujenga kiwango kikubwa cha kujidhibiti.

Serikali ilitilia mkazo hatua hizi za ushawishi wa Chama kwa kutunga sheria zisizokuwa rafiki kwa uendeshaji wa vyombo vya habari kwa ufanisi na mafanikio. Sheria hizo ni pamoja na; Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970, Sheria ya Magereza ya 1967, Sheria yaUtumishi wa Upelelezi na Usalama ya 1996, Sheria ya Bodi ya Filamu na Maigizo ya Jukwaani ya 1976 na Sheria ya Magazeti ya 1976 ilitanguliwa 2016.

Marekebisho ya kiuchumi na kisiasa yaliyoanzishwa Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1992, na baadae marekebisho ya sheria ya vyombo vya habari yamesababisha sura mpya ya vyombo vya habari vya Tanzaniailiyohakikisha kuwapo na sheria zilizolegeza masharti ya udhibiti wa serikali kwa vyombo vya habari. Vyombo vya habari binafsi viliruhusiwa na kufanya vyombo vya habari vya umma na binafsi vifurahie zaidi uhuru wa vyombo vya habari kuliko zamaza mfumo wa chama kimoja cha siasa.

Hata hivyo tangu 2015 uhuru huu umepunguzwa kwa kutungwa sheria zisizo rafiki kabisa kwa ufanyaji kazi wa vyombo vya habari nchini. Miongoni mwa sheria hizi ni Cybercrime Act ya 2015 (sheria ya makosa ya Kimitandao), Statistics Act ya 2015 (Sheria ya Takwimu), Access to Information Act 2015 (Sheria ya Upataji Habari) na Media Service Act ya 2016 (Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari).

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
Halisia

Biashara

haihusiki

Familia & Marafiki

Maslahi jumuishi ya wanafamilia + Marafiki

haihusiki

Maelezo ya ziada

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ