Tanzanian Broadcasting Corporation

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni shirika la utangazaji la umma pekee Tanzania bara. Shirika hili lilianzishwa kwa mujibu wa Sharia ya Mashariki ya Umma ya mwaka 1992 kutoa huduma ya utangazaji kwa umma kwa njia ya redio na televisheni. TBC inamilikiwa na Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya usajili wa Hazina, kitengo kilichopo ndani ya Wizara ya Fedha, inayomiliki hisa kwa asilimia 100. Nia ya serikali kuitumia TBC ni kuimalisha juhudi za serikali katika ujenzi wa Taifa. Kwa hiyo serikali inatarajia TBC kuwa msemaji kwa niaba kuliko kuwa kusema kwa uhuru na bila ya upendeleo.
Wakati huo huo Seikali inatoa fedha za uendeshaji wa TBC: utafiti uliofanywa umeonesha kuwa takribani asilimia 90 ya mapato yake ya mwaka yanatokana na ruzuku ya Serikali na kuifanya kuwa miongoni mwa vipengele vingi vigumu vinavyoathiri kujitawala na uhuru wa TBC. Asilimia ndogo iliyobaki inatokana na shughuli zake za kibiashara kama vile matangazo na vipindi vinavyolipiwa.
Hii inadhihirisha kuwa wakati TBC ni chombo cha utangazaji cha umma kisheria, kina utegemezi wa kitaifa na kisiasa na kuifanya TBC kujiendesha kwa vitendo kama chombo cha utangazaji cha Serikali.
Kwa mujibu wa Agizo la shirika la utangazaji Tanzania (Uanzishwaji) la 2007, TBC ina sifa bainifu zote za kuwa chombo cha utangazaji cha umma. Kwa mfano imepewa mamlaka ya kuhimiza na kushawishi fikra za Tanzania kwa kutoa vipindi vingi na mbalimbali vinavyoakisi misimamo, mitazamo, maoni, na mawazo, misingi maadili, na ubunifu wa hisani kuonyesha vipaji vya Kitanzania katika vipindi vya elimu na burudani; kutoa habari za aina mbalimbali, taarifa na uchambuzi kwa mtazamo wa Kitanzania na kuendeleza maslahi ya taifa na ya umma. Kuhakikisha uhuru wake wa kujiendesha, Agizo la Uanzishwaji wake linatamka kuwa “kutakuwa na mkataba bania ya TBC na Wizara yenye dhamana ya huduma za utangazaji, kuipa mamlaka TBC kuwa mtangazaji wa umma mwenye jukumu la kutoa huduma kwa wote. Mkataba utahakikisha kuwa TBC katika kutekeleza malengo yake na kutimiza mamlaka yake, matumizi ya uhuru wa kujieleza, ubunifu wa kiuandishi wa habari na utayarishaji vipindi bila ya kuingiliwa na Serikali na Wadau wengine” kama inavyotarajiwa kwa shirika la utangazaji la umma. Kwa mujibu wa wasemaji muhimu, hakuna mkataba baina ya TBC na Waziri, licha ya jitihada za mara nebili zilizofanywa na uongozi wa TBC wa awamu mbili za kuandika rasimu ya mkataba na kuiwasilisha kwa Waziri kwa ajili ya kuiangalia kabla ya kupata nakala ya mwisho ya mkataba. Utafiti umeonesha kuwa uhuru wa kujiendesha wa TBC unaathiriwa zaidi na muundo wake, kujidhibiti na kwa kiasi fulani ushabiki wa kisiasa na sheria.
TBC inaendesha matangazo ya redio na televisheni kwa umma. Matangazo ya televisheni yana chaneli mbili za TBC1, na TBC2, hali ya kuwa matangazo ya redio yana chaneli tatu za TBC Taifa, TBC FM Na TBC International. Kwa kuwa uhuru na utawala wake wa kujiendesha umeminywa, umma una maoni ya kiwango kidogo sana kuhusu TBC kwa sababu wanaiona kuwa ni msemsji wa chama tawala na Serikali yake tu, hasa nyakati za uchaguzi mkuu. Ripoti za ufuatiliaji uchaguzi za ndani na nje ya nchi zimethibitisha kuwa vyombo vya habari vya TBC kuwa mara nyingi vinakipendelea chama tawala na wagombea wake. Kwa mfano wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 TBC ilijaribu kutopendelea upande wowote katika utoaji taarifa wake, na kufanya mtazamaji mmoja kuita tukio hilo kuwa ni mafanikio ya kushangaza na ya kusimamia.
Hata hivyo mafanikio hayo ya kushangaza na ya kusimamia yalimkosesha ajira mtendaji wake mkuu mwisho wa mkatana wake wa kwanza Serikalini.
Historia ya TBC inadhihirisha kwa nini na kwa namba gani iliyoanzishwa kama chombo cha utangazaji cha umma: ni muungano wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam na Televisheni ya Taifa TVT. Mwezi Machi 1955 kituo hicho kilipandishwa hadhi na kuwa idara kamili ya Serikali na kubadilishwa jina kuwa Tanganyika Broadcasting Services na matangazo yake yalipoenea nchi nzima TBS ilibadishwa na kuwa Tanganyika Broadcasting Corporation tarehe 1 Julai, 1956. TBC ilikuwa shirika la umma kwa kufuata mtindo wa BBC. Hata hivyo uhuru wa kujiendesha na kujitawala ulibinywa kwa sababu ililazimika kufanyakazi na kufuatiliwa kwa karibu sana na Serikali ya Kikiloni na kufanya kazi kama msemaji wa Serikali ya Kikoloni.
Mwaka 1965 Serikali ya kizalendo ilipeleka Bungeni mswada wa kuvunjwa kwa TBC na Radio Tanzania Dar es Salaam ilianzishwa kama idara ya Wizara ya Habari, Utangazaji na Utalii. Huduma za matangazo ya Televisheni ya umma yalianza majaribioa yake tarehe 16.Oktoba 1999 na matangazo rasmi yakaanza terehe 15 Machi 2000. Terehe 1 Julai, 2007 Radio Tanzania Dar es Salaam na televisheni ya Taifa (TVT) ziliunganishwa na kuwa Tanzania Broadcasting Corporation.
Aina ya Biashara
Umma
Mfumo kisheria
Shirika la Umma
Nyanja za Kibiashara
Utangazaji na Televisheni
Mmiliki Binafsi
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki TBC kupitia Msajili wa Hazina, idara ndani ya wizara ya fedha. Ina shauku ya umiliki wa vyombo vya habari tangu Mei, 1961 wakati Tanzania Bara ilipopata Madaraka na kutayarisha utaratibu wa utawala tayari kwa uhuru. Inaendesha TSN pia chombo cha utangazaji cha umma cha TBC

Televisheni zingine
TBC1
TBC2
Radio nyingine
TBC Taifa
TBC FM a
TBC International
Digitali nyingine
registered as a Online Content Service at TCRA.
Biashara
hakuna
none
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
1951
Mwanzilishi
Government.
Waajiriwa
452 permanent contract 63
Mawasiliano
Tanzania Broadcasting Corporation;
P.O. Box 9191, Dar-Es-Salaam;
Tel.: +255222860760;
Fax: +255 222865577;
E-Mail: info@tbcorp.org;
Namba ya kutambulika
BRELA incorporation n°: 38167
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
90% of its annual income is derived from Government subsidy
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Utawala
Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji
Dr. Ayubu Rioba - holds the position of Director General at TBC. Hes appointed by the President in 2016. Prior to that position, he worked as a lecturer at at University of Dar es Salaam, School of Journalism and Mass Communication. He is a professional journalist (worked amongst other for the Daily News) and book author. He has a track record as critical columnist on the government, however, since in the current position, he remains silent.
Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji
Ambassador Herbert Mrango- retired civil senior civil servant.
Mr William Kallaghe – National Bank of Commercial
Member. Tanzania Investment Centre
Director. Tanzania Information Services (MAELEZO)
Central Establishment (UTUMISHI)
Bank of Tanzania
Watu muhimu wenye ushawishi + watu maslahi wengine muhimu
President - appoints the CEO/ Director General and Board Chairman.
Minister of Information - appoints the other board members.
Ministry of Finance - confirms annual budget for TBC.
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Company registered at BRELA, profile requested, still pending. Questionnaires were returned.
Vyanzo
Mboya, F, Mkwawa J, Kilimwiko, L (1982). The Functions and Role of the Press in Tanzania. A case study, Diploma Thesis. Tanzania School of Journalism.
Mwaffisi, M (1985). Broadcasting in Tanzania: Case study of Broadcasting System. MA Thesis. University of Washington, Seattle, USA.
Mwaffisi, M (2013). Editorial Independence in Public Broadcasting in Africa: Case of Tanzania Broadcasting Corporation During Multi-party Presidential Elections, 1995-2010. PhD Thesis. University of Dar es Salaam.
Mytton, G, (1976). The Role of Mass Media in Nation-Building in Tanzania. PhD Thesis. Manchester.
TBC (2007). Tanzania Broadcasting Corporation Establishment Order.
Tanzanian Government (1992). Public Corporation Act.