TBC1

TBC 1 ni cheneli ya televisheni ya taifa. Ni televisheni mwenza ya TBC Taifa na imepewa mamlaka ya kutekeleza mamlaka halisi ya kutangazia umma. Kama ilivyo TBC Taifa, asilimia 75 ya vipindi vyake vinatakiwa viwe vya habari na elimu na asilimia 25 tu ndiyo viwe vya burudani. Kwa hiyo malengo makuu ya TBC1 ni kuelimisha na kupasha habari kuhusu masuala makuu ya taifa kama ilivyo katika TBC Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Tanzania Media Measurement ya GeoPoll, kwa takwimu za hadhira za robo mwaka ya pili ya 2018, TBC One ina hadhira ya asilimia XX.XXX% kwa hiyo ni ya tano miongoni mwa vituo vya TV.
Haikusajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Inamilikiwa na Tanzania Broadcasring Corporation ambayo ni chombo cha umma cha utangazaji pekee Tanzania bara. Ni shirika la umma lililoanzishwa mwaka 1992 kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma, kutoa huduma ya utangazaji ya umma kwa njia ya redio na televisheni. TBC inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, na kusimamiwa na Msajili wa Hazina, idara ndani ya Wizara ya Fedha, yenye 100% ya hisa. Lengo la Serikali ni kutumia TBC kuongeza nguvu juhudi za serikali katika kujenga Taifa. Hatimaye, serikali inaitegemea TBC kuwa msemaji wake kuliko kutangaza kwa uhuru wake bila ya upendeleo.
Miongoni mwa matokeo itakuwa ushughulikiaji wa vyanzo vya habari. TBC1 inatumia 57% ya hoja za viongozi/mamlaka kama vyanzo vya habari. Hali hii ilibainishwa na utafiti wa ubora wa vyombo vya habari uliyogharimiwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Imedai kwamba nusu ya habari zake zina muundo bora – hali ambayo ni zaidi ya wastani katika TV Segment. TBCI pia inatumia mtangazaji wa kike katika kila habari ya pili.
Isa za hadhira
XX.XX%
Aina ya umiliki
Umma
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Free to Air
Kampuni ya vyombo vya Habari
Tanzanian Broadcasting Corporation
Muundo wa umiliki
TBC1 inaendeshwa na Tanzanian Broadcasting Corporation inayomilikiwa na Taifa
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Start: October 1999 on trial; official start March 2000 full-time
Mwanzilishi
Serikali. TBC1 ilianzishwa chini ya sheria ya shirika la umma ya mwaka 1992 .
Mtendaji Mkuu
Dr. Ayubu Rioba - ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC. Aliteuliwa na Rais mwaka 2016. kabla ya kuteuliwa alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma (SJMC). Ni mwandishi wa habari mtaalamu (aliwahi pia kufan
Mhariri Mkuu
Dr. Ayubu Rioba - angalia hapo juu
Watu wengine muhimu
Rais - anateua afisa mtendaji mkuu/Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi
Waziri wa Habari - anateua wajumbe wengine wa bodi.
Waziri wa Fedha -anathibitisha bajeti ya Mwaka ya TBC
Mawasiliano
Tanzania Broadcasting Corporation
P.O. Box 9191, Dar-Es-Salaam
Tel.: +255222860760
Fax: +255 222865577
E-Mail: info@tbcorp.org
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).
Muhtasari wa vyombo vya habari
Director General, TBC (October 2018). Media Ownership Monitor Questionnaire TBC.
Director of Radio Services, TBC (September 2018). Media Owner Monitor Questionnaire TBC.
TBC (2007). TBC Establishmend Order.