This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2022/07/06 at 23:48
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Daily News

Daily News huchapishwa na Tanzania Standard Newspapers Ltd inayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye hisa za asilimia 99 na Mhariri Mtendaji ana hisa za asilimia 1. Mhariri Mkuu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhariri Mtendaji ni Ofisa Mtendaji Mkuu na mtu wa kuwasiliana naye.

Kwa mujibu wa ripoti ya Tanzania Audience Measurement ya GeoPoll, iliyofadhiliwa na MCT, Daily News si gazeti linalosomwa zaidi kwa lilivyokuwa zamani, kwa hiyo halimo kwenye Kumi Bora. Hata hivyo kutokana na umaarufu wake wa kihistoria na ni lazima lisomwe na viongozi wenye kutoa msimamo na watoa uamuzi katika idara na wakala za serikali, limeingizwa kwenye uteuzi. Daily News lilitioka mtamboni tarehe 5 February, 1970 wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipotaifisha Tanganyika Standard Newspapers Limited na gazeti lake la The Standard (Tanzania). Daily News ni muungano wa Standard (Tanzania) na The Nationalist lililotoka kiwandani tarehe 17 Aprili, 1964. The Nationalist lilikuwa gazeti la kila siku la Kiingereza lililomilikiwa na chama cha siasa cha Tanganyika African Nation Union (TANU) kilichoongoza harakati za mapambano ya uhuru Tanzania bara na kutawala nchi mpaka 5 Februari, 1977 wakati kilipobadilishwa jina kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nab ado kipo madarakani hadi sasa.

Hata hivyo, historia ya Daily inaanzia nyuma zaidi hadi 1 Januari, 1930 wakati toleo la kwanza la Tanganyika Standard lilipotoka kiwandani. Kuanzia mwaka 1930 hadi 1967 Tanganyika Standard ilichapishwa na East Africa Consolidated Holdings ambayo baadaye ilitwaliwa na kampuni ya biashara ya Uingereza ya London-Rhodesia (LONRHO). Tarehe 7 Novemba, 1954, Sunday News lilitoka kama toleo la wiki la Tanganyika Standard.

Tanganyika Standard lilibadilishwa jina na kuitwa The Standard (Tanzania) baada ya muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tarehe 5 Februari 1970 Serikali ilitaifisha The Standard (Tanzania) na tarehe 16 Januari, 1976 The Standard Tanzania iliunganishwa na The Nationalist kuunda Daily News.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

XX.XX%

Aina ya umiliki

inamilikiwa na serikali

Maeneo yanayofikiwa

National (mainland)

Aina ya maudhui

Maudhui yaliyolipiwa

Uwazi hafifu

Upatikanaji wa taarifa za wamiliki kutoka kwenye kampuni/chaneli

3 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Tanzanian Standard Newspaper

Umiliki

Muundo wa umiliki

Daily News inachapishwa na Tanzania Standard Newspapers Ltd inayomilikiwa na serikali.

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Mmiliki Binafsi

Kundi / Mmiliki Binafsi

Managing Editor

mhariri mtendaji, ameteuliwa na serikali

1%
Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

April 26th 1972

Mwanzilishi

Serikali - limetaifishwa na lilikuwa binafsi na kumilikiwa na Tanzania Standard.

Mtendaji Mkuu

Tuma Abdallah -alichaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TSN kama Kaimu Mhariri Mtendaji mwezi Agosti, 2018. Amekuwa TSN kwa zaidi ya miaka 23 na amekuwa na nyadhifa mbalimbali katika Uhariri Mwandamizi ikiwemo Mhariri, Mhariri wa habari, Mhariri msaidizi, M

Mhariri Mkuu

Pudenciana Temba - amefanyakazi na TSN tangu aanze ajira

Watu wengine muhimu

Rais- anateuwa Mhariri Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi.

Mawasiliano

Tanzania Standard(Newspapers) Ltd

Daily News Building

Plot No. 11/4 Nelson Mandela Expressway

P.o.Box 9033

Phone: 073-2 923559

Email: info@tsn.go.tz

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sep 2018), kuhusu hadira uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Magazeti yenye maslahi maalumu kama vile habari za michezo hayakujumuishwa kwenye uchambuzi wa umiliki.

Muhtasari wa vyombo vya habari

Acting Managing Editor, Daily News (October 2018). Media Ownership Monitor Questionnaire Daily News.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ