This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/12/11 at 08:09
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Michuzi Blog

Michuzi Blog ni miongoni mwa blogi za kwanza za mtandaoni za Tanzania kuanzishwa na inashughulikia usambazaji wa habari mpya kwa Watanzania na nje ya nchi. Inatumia Kiswahili na mara nyingi hutoa habari kutoka kwa wanasiasa, serikali na jamii kwa jumla. Ilianzishwa mwaka 2005.

Michuzi Blog inashughulikia hasa masuala yanayohusu siasa na miongoni mwa kampuni za matangazo ya mtandaoni ikilinganishwa na blogi nyingine nchini. Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agosti 30 – Sept 1, 2018), Michuzi blog inasomwa na XX.XXX% ya hadhira ya Tanzania na XX.XXX% ya Dar es salaam na Morogoro.

Kwa mujibju wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (2018) Michuzi Blog ni mali ya familia, ambayo Muhidin Issa Michuzi ana 50% ya hisa, Ahmad Issa Michuzi 10%, Othman Adam Michuzi 10 %,na Christopher Mtakyawa Makwaia anamiliki 15%. Haikuelezwa ni nani anamiliki 15% zilizobaki.

Muhidin Issa Michuzi, Mwandishi Mpigapicha alianzisha kampuni na ndugu zake Ahmad na Othman na yeye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu kwa mujibu wa wasifu wa Facebook. Hakuna taarifa kuhusu Christopher Mtakyawa Makwaia. Wanahisa pia wanafanyakazi kama Wakurugenzi kulingana na taarifa za kampuni kutoka BRELA.

Ofisi rasmi ya Kampuni ilisajiliwa na ipo Namanga kwenye barabara ya Alli Hassan Mwinyi, Kiwanja na. 14/13 Kinondoni, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa BRELA (2018), hakuna taarifa ya mapato ya mwaka iliyopelekwa BRELA kwa miaka 5 mfululizo kuanzia 2013 hadi sasa.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

Aina ya umiliki

Binafsi

Maeneo yanayofikiwa

Kimataifa

Aina ya maudhui

Maudhui huru

Taarifa zinazopatikana kiurahisi

Upatikanaji wa taarifa za umiliki kutoka kwa vyanzo vingine, kwa mfano vile vinavyotambulikana kisheria

2 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Michuzi Media Group Co. Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

Michuzi Media Group imesajiliwa kwa watoto wa Michuzi na ni mmiliki wa hisa ambazo hazijitangazi. Kikundi kimesajiliwa kama Mtoa Taarifa Mtandaoni iliyosajiliwa kama kampuni TCRA na BRELA. Kampuni hii haikutoa taarifa zake kwa miaka sita 2013,2014,2015,2016,2017 na 2018 BRELA.

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Mmiliki Binafsi

Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

in the 2000's

Mwanzilishi

Muhidin Issa Michuzi – anamiliki nusu ya hisa za kampuni na ni Menyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu. Ni mwandishi wa habari mpigapicha. Anafahamika zaidi kwa kuanzisha blogi ya Michuzi Blog miaka ya 2000, ni miongoni mwa blogi za kwanza zenye maudhui yenye ma

Mtendaji Mkuu

Muhidin Issa Michuzi - angalia hapo juu

Mhariri Mkuu

Hakuna taarifa kuhusu chumba cha habari

Mawasiliano

P. O. Box 933

DAR ES SALAAM

issamichuzi@gmail.com

Tel: +255717618997

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Audience share based on GeoPoll survey (Aug 30 – Sep 1st, 2018), commissioned by MOM Tanzania. Social networks, search engines and advertising websites were excluded in the ownership analysis.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ