Law
Katiba ya Tanzania ina muhakikishia kila mtu kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake, pamoja na haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa. Hata hivyo, utekelezaji wa hali hizo za kikatiba zinajadiliwa sana na uhuru wa msingi havipo kwa kiasi kinachotakiwa. Kuanzia 2010, tasnia ya vyombo vya habari imeshuhudia idadi kubwa ya sheria na kanuni katika sekta ya vyombo vya habari na baadhi yake zimepitishwa mwaka 2018. hakuna hata kanuni na sheria hizo iliyoweka suala la umiliki wa vyombo vya habari, umiliki mtambuko au kueleza kwa umma muundo wa umiliki kwenye ajenda.
Matokeo ya kilichotokea hivi karibuni, miongoni mwa mambo mengine ni upataji Taarifa, kanuni ya maudhui, usajili wa mitandao n.k vinajadiliwa sana.
Kupata Habari
Serikali imerekebisha katiba kutoka haki kamili za kudai kupata na kusambaza taarifa mwaka 2005. Mwaka mmoja baadaye marekebisho ya katiba, Serikali imeandaa mswada wa sheria ya Uhuru wa Taarifa ya 2006. Hata hivyo wadau mbalimbali wa vyombo vya habari walikuwa na mawazo kuwa mswada wa sheria haukutimiza ari ya masharti ya katiba na haukuwa tayari kutetea na kutimiza kanuni bora za kimataifa: kupata taarifa kutoka kwenye taasisi za umma na wafichua maovu au udanganyifu mahali pa kazi hawakupewa umuhimu wowote wa kulindwa na kuishia kupewa umuhimu mdogo sana.
Umoja wa kutetea Haki ya kupata Taarifa uliyoongezwa na MCT, ulikuwa mwaka 2007 na kuandaa miswada mbadala miwili ya sheria, The Right to Information Bill, 2007 na Media Services Bill, 2008, kwa lengo la kupanua mawada ya uhuru wa taarifa.
Hatimaye Sheria ya Magazeti yabadilishwa baada ya miaka 40.
Mwaka 1976 Sheria ya Magazeti ilikosolewa sana kwa miaka mingi kwa kuruhusu Waziri wa Habari kufunga magazeti bila ya taarifa na bila ya kuomba radhi- hali iliyojitokeza mara nyingi mwaka 1992, Tume ya Nyalali iliyosababisha kutumika kwa demokrasia ya vyama vingi, na kuhitimisha kuwa sheria ilikuwa kinyume cha katiba. Itachukua miaka 20 mingine kabla sheria ya vyombo vya habari kuelekea kwenye mwelekeo huo.
Sheria iliyobatilishwa na Media Service Act, 2006. Wataalamu na jamii wamekubaliana na ubadilishaji wa Newspaper Act ambayo haikuwa rafiki. Hata hivyo bado wana shuku iwapo Sheria ya 2016 imeonesha “kusaidia au kukwaza” hali ya uhuru wa vyombo vya habari. Shirika la kiserikali la Twaweza limechambua mswada huo na kutaja mambo muhimu yafuatayo:
- Serikali ina udhibiti kamili wa utambuzi wa waandishi wa habari na utoaji leseni kwa magazeti. Hatua hizi zitakuwa na athari ya kuleta taaluma ya uandishi wa habari yote ndani ya udhibiti wa serikali, na hivyo kuzuia sana uwezo wa wahariri wa magazeti na wengine kufanya wajibu wao muhimu wa kukemea maovu.
- Kukatazwa kwa shughuli za vyombo vya habari, ikiwemo sharti la kuuwa vyombo vya habari binafsi visitangaze au kuchapisha habari kama watakavyoelekezwa na serikali na kuweka ukomo wa uhuru wa vyombo vya habari vya umma.
- Maana pana ya kashifu au haribu jina:Taarifa yoyote- hata kama ni ya kweli au maoni. Kinadharia itahesabiwa kuwa ni kashifu au kuharibu jina. Taarifa ni lazima iwe kweli na iliyochapishwa “ kwa manufaa ya umma” Inatarajiwa kuwa serikali ndiyo mwamuzi wa mwisho wa kile kitakacho hesabiwa kuwa “kwa manufaa ya umma”
- Seti ya makosa yasiyoeleweka:Vifungu vya uchochezi vinakwenda zaidi ya kile kinachofikiriwa kuwa ni cha kawaida katika muktadha wa kidemokrasia.
Kanuni kwa maudhui ya Mtandao.
Moja wapo ya sheria ya hivi karibuni ni Electronic and Postal Communications (Online Content) regislations, 2018, inayosimamia mitandao ya kijamii, blogi, vibanda vya intaneti, wanaoweka maudhui mtandaoni, na majukwaa ya mtandaoni. “sheria inakusudia kuzuia” kushuka kwa maadili, kunakosababishwa na mitandao ya kijamii na intaneti. Masharti yanawahusu wakazi wa Tanzania, Watanzania wanaoishi nje ya nchi na wageni wanaoishi nchini Tanzania wanaoendesha blogi na majukwaa ya mtandaoni yenye maudhui kwa ajili ya matumizi ya Watanzania. Kuna hatari nyingi kwa wingi wa vyombo vya habari; ambapo tathmini ya sheria ya MOM pamoja na shirika lisili la serikali la Twaweza vimebaini:
- Vitisho kwa kutotaja jina.Vibanda vya intaneti vitatakiwa kuchuja upataji wa maudhui yaliyopigwa marufuku na kufunga kamera za usalama kurikodi na kufuatilia shughuli za ndani ya kibanda. Vibanda vya intaneti utaratibu.
- Maswala ya dhinia: kwa mujibu wa sheria mpya watumiaji wa mitandao ya kijamii wana majibu na masuuli kwa taarifa wanazochapisha kwenye mitandao ya kijamii, bali pia wanaendesha blogi na majukwaa ya intaneti wanawajibika kwa maudhui yote ya kwenye tovuti zao. Hii maana yake ni kwamba watoa huduma za maudhui wanatakiwa kuwa na taratibu za kutambua vyanzo vya maudhui na kushirikiana na mamlaka (ikiwemo, kwa mfano, itokeapo kuwa mamlaka yanataka kujua utambulisho wa mtumiaji). Kwa maneno mengine iwapo kanuni zitaanza kutumika, kwa mwendesha blogi au mmiliki wa jukwaa kukataa kuchukua taarifa za utambulisho wa mtumiaji, au kukataa kueleza taarifa hiyo kwa mamlaka, litakuwa ni kosa la jinai.
- Adhabu kali zitajenga mazingira ya hofu: Ukiukaji wa masharti haya ni kosa la kupewa adhabu ya faini isiyopungua Tsh 5,000,000 au kifungo cha muda usiopungua miezi 12, au vyote . Hali hii pia inaweza kusababisha kujidhibiti.
Chanzo
Twaweza (2016). The Media Services Bill: help or hinderance? Accessed on: 13. November 2018
Twaweza (2016). Brief Analysis of Media Services Bill 2016. Accessed on 13. November 2018
Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations, 2018
Twaweza (2018). Analysis of Online Content Regulations. Accessed on 13. November 2018