Vyombo vya Habari
Redio, kwa mujibu wa Afrobarometer 2017, ni chanzo cha kukimbilia kupata habari za hivi karibuni. Asilimia 45 ya wasikilizaji hufuata redio kila siku, 26% mara chache kwa wiki. TV (23%/13%), Intaneti (8%/7%), Mitandao ya Kijamii (8%/7%) na Magazeti (5%/10%) wanafuata kulingana na umbali. Data za hivi karibu zilizochunguza tabia za utumiaji mpana, kwa mfano pamoja na matumizi ya kutumia vyombo vya habari kwa burudani na michezo, hazipo. Data za hivi karibuni za aina hiyo, zilikusanywa na Ipsos, ni za mwaka 2014 na zinathibitisha hali hiyo – redio ilitumiwa mara kwa mara zaidi na magazeti yalikuwa ya mwisho.
Utafiti huo huo unaonesha kuwa takribani theluthi moja ya Watanzania wamesema kuwa vyombo vya habari vinawapasha habari wapiga kura na kushawishi uchunguzi wa viongozi. Wachache wamejibu kwa 10% wanaona kuwa vyombo vya habari vinafichua uongozi mbaya. Usikivu mbaya ulikuwa nab ado ni tatizo kwa vituo vingi vya redio na televisheni. Habari, michezo na muziki ni vivutio vikubwa kwenye vyombo vya habari vingi.
Imani kwa vyombo vya Habari inapungua lakini bado ni thabiti
Imani kwa vyombo vya habari inategemea sana aina ya chombo cha habari. Asilimia ya raia wenye imani kubwa kwa taarifa kutoka TV na Redio ni kubwa sana, kwa 69% na 64%, mtawalia. Matangazo redioni au kwenye TV yanawavutia sana watu kuliko taarifa inayojadiliwa kwenye mikutano ya hadhara (22%) au karibu na mawasiliano ya kijamii (13%). Magazeti yanaaminiwa zaidi na moja ya sita ya Watanzania. Taarifa inayopitia kwenye mitandao ya kijamii ni la mwisho, kwa 6% tu wanayoiamini. Licha ya kupungua kwa viwango vya imani kwa vyombo vya habari wengi wao wanaamini katika kutendewa haki kwa vyombo vya habari. Kwa mfano, wanapendekeza ni lazima serikali ithibitishe adhabu yoyote kwa makosa ya maudhui, mahakamani (54%). Na raia kwa upande wao wangependa magazeti wanayochapisha habari za uongo au za upotoshaji yaombe radhi na yachapishe masahihisho (62%) kuliko kufungiwa au kutozwa faini (38%)
Kiwango cha Juu cha Wingi wa Hadhira kwenye magazeti, Redio na TV
MOM inaonesha kuwa wingi wa vyombo vya habari upo kwenye sekta tatu; magazeti, redio na TV; Kiwango cha juu cha wingi wa hadhira kinabainishwa wakati kampuni nne za juu kwa pamoja zinafikia zaidi ya 50% wingi wa hadhira.
Hali hii imejitokeza kwenye magazeti ambapo kampuni nne za juu zina hadhira ya XX.XXX % ya wasomaji ikiwemo Mwananchi Communications Limited inayoongoza kundi hilo. Kiwango cha juu cha wingi kipo pia kwenye TV, ambapo wamiliki wane wa juu wanawakilisha hadhira ya XX.XXX%. Kwa TV na Redio, IPP Media Group, Clouds Entertainment pamoja na Tanzanian Public Broadcasting (TBC)inayomilikiwa na serikali, vina nafasi imara kwenye soko. Ingawa soko la redio lina wingi na aina mbalimbali, inaonyesha kiwango cha juu cha wingi wa hadhira kwenye wamiliki wane wanaoongeza soko kwa pamoja wanaotoa XX.XXX% ya wasikilizaji wa habari. Wingi wa hadhira kwenye sekta ya mtandao ni kiwango cha chini, ina XX.XXX% tu.