This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/10/13 at 16:52
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Kudhibiti Hoja na Takwimu

Jinsi Sheria ya Takwimu inavyozuia utafiti huru na uandishi wa habari

“Sheria ya Takwimu ya 2015 haizuii au kumkataza mtu yeyote kuchakata na kutayarisha taarifa ya kitakwimu, hata hivyo wafanye hivyo baada ya kushauriana na NBS kwa ushauri wa kiufundi na kuhakikisha kuwa wanafuata njia zilizowekwa na viwango.” 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu, ina mamlaka ya kushirikiana na wadau katika kuchakata, kutayarisha na kusambaza takwimu rasmi pamoja na kutoa maelekezo kwa mtu mmoja mmoja, taasisi na wakala wanaotaka kufanya utafiti wa kitakwimu utakaotoa takwimu rasmi.”

Wakati nukuu hizi kutoka kwenye kijarida cha NBS cha Agosti 2017, zinaonesha kama vile ni msaada uliyokusudiwa, kwa lugha ya kawaida ina maana kuwa: kila mtu yuko huru kufanya utafiti – lakini ataruhusiwa tu kuzungumzia kuhusu matokeo au kuchapisha data baada ya kupata idhini rasmi kutoka kwa NBS.

Kampuni ya Utafiti wa Soko imefungwa kwa miezi kadhaa.

Je, inakuwaje iwapo hufuati utaratibu huu? Kampuni ya utafiti wa soko, GeoPoll, mtoaji taarifa za data za kila siku za hadhira ya TV, Redio na Magazeti barani Afrika kwa siku moja tu, imelazimika kuona cha mtema kuni.

Mwezi Agosti, 2017, GeoPoll ilichapisha matokeo yake kiwango cha utangazaji wa TV nchini Tanzania bila ya kuidhinishwa. Mkurugenzi mkuu wa NBS alisema yafuatayo, “NBS inapenda kuuarifu umma kwa jumla na wale wadau wanaotaka takwimu, kuwa takwimu zilizotayarishwa na GeoPoll Company kuhusu wasikilizaji wa redio na watazamaji wa TV si takwimu rasmi kwa sababu kampuni hiyo imeshindwa kufuata mbinu na viwango vilivyotajwa kwenye Sheria ya Takwimu ya Tanzania Na. 9 ya 2015”

Matokeo yake ni kwamba, uchapishaji data za hadhira bila ya idhini umesababisha kufungwa kwa muda kwa shughuli za GeoPoll nchini Tanzania.

Tarehe 19 Aprili 2018, mkutano wa pamoja uliitishwa na kuhudhuriwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa GeoPoll, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watumishi wa Wizara, Wawakilishi wa NBS, na mjumbe kutoka GeoPoll. Matokeo yake ni kwamba hadhi ya GeoPoll, kama kampuni iliyosajiliwa Tanzania na kupewa leseni imethibitishwa, na GeoPoll imechapisha taarifa kwa vyombo vya habari, “Serikali ya Tanzania Imeidhinisha GeoPoll kufanya Huduma za Utafiti nchini Tanzania” (April 25, 2018).  

Mwezi Septemba, 2018, Sheria ya Takwimu ilifanyiwa marekebisho (angalia hapo chini) na kusababisha kuboreshwa kwa baadhi ya vipengele vyenye matatizo, kwa mujibu wa Twaweza. 

Je MOM imeathiriwa Vipi?

Kama ilivyo kwenye nchi nyingine, MOM ilikusanya, kuthibitisha na kuchanganua seti kubwa ya data kuhusu soko la vyombo vya habari nchini Tanzania. MOM huchagua vyombo vya habari muhimu zaidi kulingana na kiwango cha hadhira – kwa kuwa vyombo vya habari vyenye kiwango kikubwa cha hadhira ni vile vinavyopendwa na vyenye ushawishi kuhusu maoni ya umma. Nchini Tanzania, GeoPoll ilitumiwa kama chanzo kikuu cha data kamili na za kuaminika za hadhira.

Hata hivyo tumebaini kuwa, licha ya marekebisho yaliyofanywa katika Sheria ya Takwimu (angalia hapa chini), uchapishaji wa data za hadhira unaweza pia kuangukia katika kuzuiwa – kwa kweli kwa mujibu wa Kifungu cha 24B. Wakati masharti ya sheria yanaelekea hayako wazi sana na uzoefu wa masharti hayo katika utekelezaji wake uliyopo, MOM imeamua kuomba idhini rasmi kutoka NBS. Maombi yalitumwa kwa njia ya baruapepe wiki ya 45, juhudi za kufuatilia kupitia simu, na fax, wiki ya 46. Kwa mujibu wa NBS itatoa ushauri ndani ya wiki moja, mara tu baada ya kupokea nakala ya ripoti iliyochapwa, kutokana na taarifa ya muda mfupi, kikundi cha utafiti kimeendelea kusubiri tu kwa ajili ya idhini rasmi na wakati tunasubiri, tuliamua kutokutoa data za hadhira kwenye tovuti. Idadi itachapishwa – kama ilivyo kwenye miradi ya MOM katika nchi 15+ nyingine – mara baada ya NBS kujibu. Kwa kuwa data zote zipo na zimechanganuliwa kwa kina, mwenendo na mielekeo bado inaonekana kwenye matokeo yetu, pamoja na kwenye sehemu ya kiashirio cha hatari.

Bila ya kujali jibu la NBS, haina budi kuzingatiwa kuwa tabia hiyo isiyo ya kawaida ya kudhibiti ubadilishanaji wa umma wa data za utafiti, husababisha hatari ya kiwango cha juu kwa uhuru wa kujieleza, kuzuia utafiti wa kisayansi uandishi wa habari za data kitaalamu.

Je, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ni nini? (NBS)

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanzishwa kama Taasisi ya Umma inayojitolea kwa mujibu wa Staticst Act, 2015 na ina madaraka na mamlaka ya kutoa takwimu rasmi kwa serikali, jumuiya ya wafanyabiashara na umma kwa jumla. Sheria pia inaipa NBS mamlaka ya kuwa chombo cha kuratibu ndani ya mfumo wa Taifa wa Takwimu (NSS) kuhakikisha kuwa kunatayarishwa takwimu bora rasmi. Kabla ya kutungwa kwa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, NBS ilikuwa miongoni mwa wakala za utendaji za serikali, iliyoanzishwa 26 March, 1999, Chini ya Executive Agencies Act, 1997.

Rais anamchagua Rais kwa kushauriana na Waziri mwenye dhamana – kama alivyo Mwneyekiti wa Bodi. 

Historia ya Sheria ya Takwimu ya 2015

Sheria ya Takwimu ya 2015 ilitungwa mwaka 2015 kuanzishwa na kuratibu National Statistical System. Athari zinazoweza kumtokea yeyote anayetumia au kufanya kazi zinazohusu takwimu chini Tanzania, kama vile taasisi za utafiti vyombo vya habari na vyama vya kiraia zimelaumiwa na umma. Tunaweza imetaja baadhi ya changamoto muhimu:

  • Kutokuwa na uhakika wa nani anayeruhusiwa kukusanya takwimu na kunahitajika idhini gani.
  • Vikwazo kwa wanaotoa tahadhari ya masuala mbalimbali bila ya kulindwa kokote kwa maslahi ya umma.
  • Makatazo makali kuhusu uchapishaji au kueleza taarifa yoyote yenye maudhui ya kitakwimu. Inakuwa ukiukaji wa sheria (i) kuchapisha au kutangaza taarifa za “uongo”za takwimu na (ii) kuchapisha au kutangaza taarifa za takwimu "zitakazoweza kupotosha ukweli”. 
  •   Adhabu kwa wale watakaopatikana na hatia ya makosa kwa mujibu wa sheria hiyo zilikuwa kali mno, kusema kweli hazikuwa na kikomo.

Sheria hiyo imepuuza ukweli kuwa migogoro inayohusu takwimu ni sehemu muhimu sana ya mijadala ya kisomi na kisera, na inaonesha kuwataka wale wanaotayariha au kuchapisha takwimu kuomba idhini ya NBS kabla ya kufanya hivyo.  

 “The written Laws Miscellaneous Amendments Act No. 3 of 2018” yaani marekebishobalimbali ya sheria, yanashughulikia baadhi ya changamoto hizo.

Je, kumetokea mabadiliko gani kwa Sheria ya marekebisho No. 3 ya 2018?

Sheria ya Takwimu ilirekebisho wakati Bunge lilipopitisha THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO.3) ACT, 2018, Tarehe 10 Septemba Masharti manane yalirekebishwa: Vifungu vya 3.17.18. 19, 20, 22, 24A na 37.

Kwa mujibu wa Twaweza, Marekebisho haya yameleya mabadiliko mazuri/ chanya kwa jumla. Itatoa kwa mfano uwazi zaidi kuhusu zisizorasmi zilizoelezwa kuwa “taarifa za kitakwimu” katika kifungu 22(b) taarifa za za kitakwimu zinaelezwa kuwa “any organized quantitative or qualitative informantion obtained from different sources through censuses, surveys or administrative data“, ambayo itatumika kwa mfano wa Media Ownership Monitor.

Masuala makuu

  1. Kabla ya kusambaza, kuchapisha au kutangaza takwimu rasmi, mtu yeyote ni lazima apate idhini ya NBS. Mtu kwenye matokeo tofauti na takwimu zilizosambazwa na NBS atashauriana na NBS kabla ya kutangaza matokeo hayo kwa umma. (Section 24A)
  2. Marekebisho hayo yamkataza/kumpiga marufuku mtu yoyote kusambaza au kutangaza kwa umma taarifa zozote za kitakwimu bila ya idhini ya mtakwimu mkuu. Taarifa za kitakwimu zinazokusudiwa kukosoa kupotosha au kudharau Takwimu Rasmi ni marufuku kuchapisha. (Section 24B)
  3. Marekebisho hayo yanatoa kosa la jinai la jumla kwa mtu yeyote atakayechapisha au kusababisha kuchapishwa au kutangazwa kwa takwimu zozote rasmi au taarifa ya kitakwimu bila ya idhini ya kabla ya Mtakwimu Mkuu. Matokeo yake ni faini isiyopungua Tsh. 10 Millioni (10,000,000) au kifungo cha muda usiyopungua miaka mitatu (3) au vyote viwili (Section 37 ammended by section 29 of the Act No. 3 of 2018 by deleting subsection 4,5 and 6 of Principle Act and by substituting subsection 4 of Section 37 with new meaning yani kufuta baadhi ya vifungu na kuandika kingine kwa maana mpya
  4. Cheo cha “Mkurugenzi Mkuu” kimefutwa na kubadilishwa na “Mtakwimu Mkuu”ambaye ni mtendaji Mkuu wa NBS. (Section 21 (a) of the Act No. 3 of 2018).
  5. Tafsiri ya neno “Takwimu Rasmi” imepanuliwa kumaanisha takwimu zilizotayarishwa, kuthibitishwa, kukusanywa na kusambazwa na au kwa mamlaka ya NBS na pia kufafanuliwa zaidi kumaanisha taarifa yoyote ya idadi au bora iliyotayarishwa na kupatikana kutokana vyanzo mbalimbali kwa njia ya mwafaka, utafiti au data za kiutawala. (Section 3 ammended by section 22 of Act No. 3/208)
  6. Mtakwimu Mkuu amepewa madaraka na mamlaka ya kuanzisha, kurekebisha au kukatisha ukusanyaji wa takwimu rasmi unaofanywa kwa utafiti ay mwafaka (censuses). Hakuna mtu, Taasisi ya Serikali ya wakala itakayoidhinisha kuanza ukusanyaji wa takwimu rasmi kwa njia ya utafiti au consuses isipokuwa kwa idhini ya Mtakwimu Mkuu. (Section 24 of the Act. No. 3/2018 Ammended section 18 of Principle Act, 2015)
  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ