This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/07/18 at 17:24
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Mlinzi aliyepooza – wakati vyombo vya habari vinaponyamaza

Vyombo vya habari Tanzania vinalalamika kuhusu kukosa uwazi kwa sekta ya umma na sekta binafsi mhimu. Wanasema kuwa wanapata shida kupata taarifa zenye maslahi kwa umma katika sekta mbili. Mradi waMOM unaonyesha kuwa vyombo vya habari vyenyewe havina uwazi, na kufanya uwe vigumu kwa wakati kupata taarifa zenye masilahi kwa umma kuhusu sekta ya vyombo vya habari.

Taarifa za msingi hazikutolewa 

Kutoka kampuni 21 zilizoulizwa ni kampuni 3 tu ndizo zilizojibu kampuni nyingi za vyombo vya habari hazikurudisha madodosa yetu kabisa na hata hizo chache zimejibu tu baada ya wiki tatu za ufuatiliaji wa mara kwa mara unaochosha. Kati ya hizo chache hawakujibu maswali kwa usahihi au baadhi ya maswali haykujibiwa kabisa hali hii ilishangaza sana kwa sababu maswali yenyewe hayahusu mada nyeti, ni ya kawaida tu: yamehusu kujua wenye hisa na watu wengine muhimu kwenye kampuni, Tarehe ya usajili BRALA, TCRA au idadi ya habari, MAELEZO mwanzo wa shughuli na idadi ya watumishi. Maswali yanayogusa kuhusu maswali ya fedha yalikuwa ni hiari kujibu- na kusema kweli hakuna hata kampuni moja ya vyombo vya habari iliyorudisha madodoso imejibu seti hiyo ya maswali.  

Si ruhusiwi kijibu maswali haya

Kila watafiti walipofuatisha madodoso kwa maafisa waandamizi kwenye kampuni ni za  vyombo vya habari walijibiwa kuwa taarifa iliyoombwa haiwezi kutolewa kila ya idhini ya maofisa watendaji wakuu au wamiliki wa vyombo vya habari moja kwa moja. Viongozi hao wa ngazi za juu ni hawakuweza kufikiwa kwa kila kinachoonekana kuwa ni umangimeza iliyopo kwenye kampuni za vyombo vya habari, kuvipoozesha vyombo hivyo kutolea ndani wakati baadhi ya maofisa walikuwa tayari kujadili taarifa na watafiti, kwa sharti kwamba majina yao yasitajwe wala wasinukuliwe. 

Wasemaji rasmi wa kampuni mara nyingi wako kwa viongozi wa ngazi za juu. Kwa upande wa IPP, hata mmiliki wake Dkt Reginald Mengi anatajwa kuwa msemaji ambaye kinadhana ni lazima athibitishe mawasiliano yanayohusu kampuni, zake. 

Ushawishi upande mmoja – kokosa usalama kwa upande mwingine.

Uzoefu huu unaonesha kiwango Fulani cha ushawishi wa wamiliki wa vyombo vya habari. Wakati hjukidhibiti si rahisi kuelewa, kwa hali hii kimahitaji angalau tahadhari ya hali ya juu kuwasiliana taarifa ya msingi kabisa ni dhahiri hali hii maweka alama kubwa ya kuuliza kuhusu vyombo hivyo vya habari vitakuwa wazi kiasi kutoa taarifa nyeti kabisa. 

Kokosa usalama kuhusu ni uhuru wa namna gani kutenda ndani ya mazingira ya kazi kunaweza kuhusishwa na usalama wa ajira waajiriwa na waandishi wa habari kwenye sekta binafsi mara nyingi wainaishi kwa hofu kuwa ajira zao zinaweza kusitishwa wajkati wowote. Masharti mikataba na nafasi mara nyingi ni chache ni kweli kwamba waanddishi wa habari wanaogopa kufukuzwa kazi iwapo itabainika kuwa wametoa taarifa bila ya ridhaa ya mmiliki. Hali kadhalika katika sekta ya umma, hofu ya jumla ya uhusiano wenye uhyasama na ofisa mtendaji mkuu inaweza kuonekana kiwango cha majibu ya vyombo vya habari ni takribani sifuri 

Kiwango cha uwazi kinapatikana kwa kila chombo cha habari kwenye taarifa zao katoka tovuti ya MOM. Matokeo ya vyombo vya habari 36 vilivyochanganuliwa na kuulizwa ni kama ifuatavyo. 

Levels of Transparency

Wazi zaidi maana yake kampuni/chaneli inatoa taarifa ya kuleta matokeo na kwa ukamilifu kuhusu umiliki wake, data zinakwisha mara kwa mara na kubakiwa kwa urahisi nchini Tanzania hakuna kampuni iliyyokuwa na uwazi zaidi. 

Uwazi wa kimyakimyani pale ambapo baada ya kuombwa data za mmiliki zinapatikana kwa urahisi kutoka kwenye kampuni/ chaneli ni kampuni tatu tu –kampuni zinazomilikiwa na Serikali za TBC na TSN – Pamoja na mwananchi communication Limited. Kwa kuwa zina idadi ya vyombo vya habari, tumepata taarifa za 22% ya vyombo vya habri. Hata hivyo taarifa hizo zilipatikana baada ya ufuatiaji wa kuchosha na zilikuwa zinatofautiana na taarifa rasmi. 

Data zinapatikana kwa umma maana yake data za umiliki zinapatikana kwa urahisi kutoka vyanzo vingine, kwa mfano masifali za umma n.k

Nchini Tanzania, data zilipatikana kwa umma kwa vyombo vya habari vingi (64%) katika BRELA hata hivyo ubora wa taarifa rasmi za kampuni haukuwa mzuri na kuwa na sehemu zisizojazwa. Data mara nyingi kwa kawaida zinakuwa zimepitiwa na wakati, na mabadiliko ya umiliki hayakuwa yameingiziwa. 

Data hazikupatikana maana yake umiliki wa data haupatikani kwa umma, kampuni/ chanel zinakataa kutoa taarifa au hazijibu hakuna kumbukumbu za umma zilikuwapo kwa 15% ya vyombo vya habari, hakukuwa na data BRELA inga ni lazima kusajili hapo kama kampuni na hata kama tumelipia – kazi kuwapo – taarifa ya kampuni.

Kuficha sana– maana yake ni kwamba licha ya kutopatika kwa data sahihi, umiliki umefichwa, kwa mfano, kwa kampuni za uongo n.k 

Tukio la nmana hii halikuthibitishwa nchini Tanzania. Hata hivyo, wakati mwingine kampuni za vyombo vya habari zimeorodhesha wenye hisa tofauti na wale waliowakilisha kampuni kwa umma. Hii ni hali iiliyokuwa kwa Rostom Aziz, anayeonekana kama mmiliki wa New habari (2006)- lakini wamiliki wa hisa wengine wanaoonekana kwenye karatasi. Tukio jingine la kusisimua ni mwanasiasa wa CHEDEMA Freeman Mbowe ambaye Mkwewe Dkt Lilian Mtei ndiye mmiliki wa hisa nyingine za free media Ltd. Kama daktari wa matibabu anayefanyakazi Hospitali, hawezi kuwa na muda wa kutosha na utaalam wa kushughulikia kampuni “yake” ya vyombo vya habari, wakati mume wake angefurahi zaidi.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ