This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/10/13 at 16:23
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Kanuni imekosewa

Dhana ya “Kanuni ya vyombo vya habari“ inautata nchini Tanzania. Tangu nchi ipate uhuru, kanui daima imekuwapo kwa maana ya kudhibiti na kupunguza soko, hata kushawishi maudhui ya vyombo vya habari. Kwa mfano wakati wa kuelekea kwenye Azimia la Arusha mwaka 1967. Rais Nyerere alieleza maoni yake kuwa uhuru wa kujieleza ni lazima uwe na mpaka kwa maslahi ya malengo muhimu zaidi kwa kuwa unaweza kuathiri sera mpya iliyoanzishwa ya ujamaa kutokana na hali hiyo wahariri walipata taabu sana kuzindua magazeti huru muda mrefu magazeti na majarida huru yalipewa ruhusa ya kusajiliwa yalikuwa yadini: Kubanwa kwa vyombo vya habari binafsi kulibadilika tu wakati ambapo hata mfumo wa siasa ulipobadilika kwa kwa kuanzisha mfumo wa vyama vingi, 1992. 

Hakuna ulinzi kabisa

Kwa upande mwingine kwa lengo la kulinda soko lenye ushindani na hai, ambalo wingi wa vyombo vya habari, hujadili kwa uwazi wingi wa mawazo na mitazamo, haijatokea. Hadi leo, kanuni za ulinzi zinazokataza wingi wa umiliki  na ukiritimba kwa mfano  kwa kuzuia uunganishaji au uamuzi zaidi ya ukomo Fulani uliyowekwa na havipo. Hususani .

Kupinga kanuni za vyombo vya habari mtambo. 

Mwaka 2001, wadau wa vyombo vya habari walipendekeza, hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya umiliki  mtambuko pia katika  wingi wa nvyombo vya habari, kutokana na waraka wa sera uliyotayarishwa na Serikali. Ni mojawapo ya mapendekezo matatu ambayo Serikali imekataa kuyaingiza kwenye sera ya vyombo vya habari – baada ya mapendekezo ya kubadili kampuni za vyombo vya habari vya umma na katika kuhimiza usawa wa kijinsia katika vyombo vya habari. 

Mwaka 2009, Serikali hatimaye ilichukuwa hatua. Wakati huohuo baadhi ya kampuni za vyombo vya habari kama vile IPP Media wametumia fursa ya kuwekeza kwenye vyombo vya habari na vimepanuka haraka kwa sababu kanuni zilikuwa na upungufu. Kutokana na kukabiliwa na changamoto hiyo Serikali ilipendekeza baadhi ya marekebisho kwenye sera ya Taarifa na utangazaji kusimamia umiliki wa vyombo vya habari mtambuko: wamiliki wa vyombo vya habari vuwajibike huchagua iwapo ni chombo cha habari cha kielektroniki au gazeti. Kwa wale ambao tayari wanamiliki vyote, pendekezo la rasimu ya Sera ni kwamba ni lazima waamue sekta moja kwa kipindi cha miaka mitano  sababu rasmi ya Serikali kwa pendekezo hilo la sera kuhusu umiliki wa vyombo vya habari ilikuwa ni kuwazuia wamiliki wa vyombo vya habari kutumia vyombo vya kupendelea biashara zao au maslahi ya kisiasa.

IPP media uliona kuwa imelenga kwa uonevu na wamiliki wa vyombo vya habari kwa jumla walipinga pendekezo hilo. Serikali iliendelea na rasimu yake lakini kwa kukosa uwazi. Baadhi ya wadau wa vyombo vya habari waliorodheshwa kama washiriki wa mkutano ambapo marekebisho yaliandikwa – bila ya kuelewa kuwa mkuatano umefanyika. Licha ya kutoridhishwa na uaratibu huo, wadau wa vyombo vya habari pia walikataa pendekezo la Sera. Hatimaye rasimu ya mapendekezo iliachwa  kutokana na wimbi hilo. 

Baadaye: Sheria ya udhibiti wa maudhui  mtandaoni inaondoa uhuru wa kujieleza.

Hakuna mipango yoyote ya kujaza upungufu wa sheria na kanuni. Badala yake, hivi karibuni Tanzania imetia saini kuwa sheria kanuni mpya ya kushangaza inayosimamia mitandao ya kijamii na blogi. Kanuni hiyo inajulikana kuwa ni Electronic and Postal Communication (Maudhui ya mtandaoni) Regulations 2017 imeanza Marchi 2018. Miongoni mwa mabadiliko hayo ni ada ya leseni itakayotozwa kwa watanzania wanaoendesha vituo vya redio mtanaoni na tovuti za video (TV) hali hii inaweka vikwazo vya kuingia kwa wahusika wapya na kukiuka wingi wa mtandao. 

Chanzo

(i) The Tanzania Communications Regulatory Authority Act 2003
(ii) The Electronic and Postal Communications Act, 2010
(iii) The Electronic and Postal Communications (Licensing) Regulations 2018
(iv) The Electronic and Postal Communications (Radio Communication and Frequency Spectrum) Regulations, 2018
(v) The Electronic and Postal Communications (Digital and other Broadcasting Networks) Regulations, 2011
(vi) The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations, 2018
(vii) The Electronic and Postal Communications (Radio and Television Broadcasting Content) Regulations, 2018

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ