Teknolojia
Katima mwongo uliopita, Tanzania imekabiliwa na mabadiliko makubwa ya teknolojia yaliyosbabisha watu kubadili namna wanavyowasiliana, kutumia habari na taarifa. Kama zilivyo nchi nyingine za kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania inakabiliwa na mapinduzi ya simu za mkononi tangu mwaka 2012, wastani wa bei za smartphone zimepungua kwa nusu, Watanznia wengi zaidi wana simu za mkononi na huduma za simu si waya na zinahusika na matumizi mengi ya mtandao. Kuanzia mwaka 2012 mpaka 2017, umaarufu wa matumizi ya mtandao yameongezeka maradufu. Licha ya ongezeko la haraka, 55% ya Watanzania bado hawawezi kupata mtandao kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na utafiti uliofanywa na Pew Research Centre unaonesha kuwa ni 13% tu ya Watanzania wanamiliki smartphone.
Hata hivyo, maendeleo haya si kama yamebadili matumizi ya vyombo vya habari tu bali pia yameshawishi maeneo mengine ya maisha: kwa mfano, zaidi ya Watanzania milioni 20 wanatumia huduma za fedha kwa njia ya simu – njia hii huhamisha fedha kwa kutumia simu ya mkononi – na kuchukua nafasi ya mabenki yaliyozoeleka. Ndiyo maana hasa katika maeneo ya vijijini simu za mkononi ni muhimu sana na si anasa.
Kuanza mapema kutumia mawasiliano ya kidijiti
Utangazaji kwa njia ya simu unaingia katika zama za kidijiti. Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza za Afrika Mashariki kuhamia katika mfumo wa kidijiti na kuzima mitambo yake ya televisheni ya analojia mwaka 2013. Televisheni inayosafirisha mawimbi kidijiti kwa njia ya antenna hupatikana katika miji mingi mikuu. Idadi ya watu wenye uwezo wa kulipia matangazo ya TV ni takribani 2.2milioni. Hata hivyo, ikilinganishwa na redio, televisheni bado ni ghali kwa mtumiaji na mtayarishaji na hukabiliwa na sheria ngumu ya serikali. Hali hii inasababisha kupenya kwa matumizi ya televisheni kusiko na uhakika zaidi na kuacha redio kuwa chombo cha habari cha utangazaji kinachofikiwa zaidi nchini Tanzania. Kihistoria, redio imemuwezesha mmiliki kufikia soko la vyombo vya habari kutokana na kutokuwapo kwa ada ya leseni. Hali ilibadilika mwaka 2018 kutokana na utekelezaji wa the Electronic and Postal Communication Regulations, zilizowataka watangazaji kuwa na leseni za biashara zao za vyombo vya habari na kulipa ada ya mwaka inayoanzia 10$ kwa vituo vidogo vya redio na kufikia 20,000$ kwa utangazaji wa redio kwa nchi nzima, bila ya kujumuisha leseni za awali na ada ya kuongeza muda wa matumizi ya leseni inayotakiwa kulipwa kila baada ya miaka 3 hadi 5.
Mfumo wa Ikolojia na simu za mkononi
Kwa kuangalia wanaotoa maudhui ya kimtandao, mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Google, na Twitter na kampuni zao tanzu za Instagram, WhatsApp, na YouTube ni tovuti zinazotembelewa zaidi, kwa mujibu wa GeoPoll. na tovuti za nchini hufuata.
Vilevile soko la mawasiliano ya simu limetawaliwa na wageni: Kwa jumla mawasiliano ya simu yaliyotawaliwa na kampuni za kigeni ni Halotel, Vodacom, Tigo na Airtel kwa pamoja yana 97% ya malipo ya simu za kuzungumza. Hatimaye, kampuni zao kuu ziko Vietnam, Uingereza, Luxermbourg na India, ingawa baadhi yao zina wanahisa wa nchini.
Vodacom Tanzania Limited, ina 32% ya soko la malipo ya kuzungumza na ina wamiliki wengi. Iliyopo muhimu zaidi ni Vodacom Group Ltd ya Afrika Kusini (49%), kwa kiasi Fulani inamilikiwa na serikali ya Afrika Kusini lakini hatimaye inamilikiwa na kampuni ya Vodafone Group ya London na Mirambo Ltd (26%), kampuni hodhi inayomilikiwa na Rostam Aziz – aliyewahi kuwa tajiri mkubwa Tanzania. Ingawa gazeti la Tanzania la Citizen limeripoti majira ya joto 2018, kuwa Rostam Aziz ana mpango wa kuuza hisa zake kwa serikali ya Afrika Kusini. Kwa kufanya hivyo, kutabaki 11% tu za hisa za kampuni kwa wawekezaji wa Afrika Mashariki.
TiGo yenye 29% ya soko la malipo ya kuzungumza , inamilikiwa na MIC Tanzania Limited, ambayo 100% ya hisa zake ni za Kampuni ya Millicom iliyoko Luxembourg. Mwezi Machi, 2018 TiGO imetangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwa kampuni ya mawasiliano ya simu inayokuwa haraka sana nchini.
Airtel, yenye 27% ya soko la kuzungumza, inamilikiwa naBharti Airtel Limited yenye hisa nyingi za 60%. Asilimia nyingine 40% zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania. Mwaka 2017 serikali imedai kuwa kampuni hiyo inamilikiwa na taifa na Kampuni ya India inayopitisha mawimbi ya sauti, imeidanganya serikali kuhusu hisa. Bharti Airtel imekanusha kukiuka utaratibu wakati wa mkataba iliyoingia kampuni kuwa yenye hisa nyingi kitengo cha Tanzania.
Viettel Tanzania Ltd inayofanyakazi kwa jina la Halotel ina 9% jumla ya malipo ya simu ya kuzungumza. Hatimaye Viettel Tanzania ni sehemu ya Viettel Global Group inayomilikiwa na Serikali ya Vietnam na kuendeshwa na Wizara ya Ulinzi ya Vietnam.
Kiwango Zero vs Kutokuwa na Upande wowote
Airtel, tiGo na vodacom zinawapa wateja wao kifurushi tofauti kidogo kinachojulikana kuwa Free Basics by Facebook”. Kwa kutumia kifurushi hiki, tovuti mbalimbali zilizochaguliwa kama vile Facebook, Twitter, YouTube, Instagram, na WhatsApp hupatikana bure, hali ya kuwa watoa huduma wanalipia gharama za data za watumiaji. Ingawa huduma hii inaonekana bora zaidi kwa wateja, na huwapa upendeleo watu kwenye maeneo maskini, fursa ya kupata tovuti hii, mtindo wa kiwango zero kunaweza kuwa tishio kwa kutokuwa na upande wowote wa mtandao na wingi wa vyombo vya habari kutokana na urahisi wa kupata tovuti zilizochaguliwa.
Watoa huduma ya maudhui mtandaoni wanakabiliwa na matatizo
Ingawa watu wengi wanaweza kutumia maudhui ya vyombo vya habari mtandaoni, watoa huduma hizo wanakabiliwa na matatizo kutokana na seti ya sheria na kanuni mpya zilizotekelezwa na serikali. Tangu mwaka 2015, serikali ya Tanzania imeimarisha vitendea kazi kusimamia maudhui iwapo yanafaa. Kwanza, ilisema watoa huduma maudhui ni lazima wajisajili TCRA na kulipa ada ya mwaka kwa kufanya hivyo. Ada ya leseni ya kuanzia ni $900/1,000,000 na ada ya leseni ya mwaka ya $900/1,000,000 ndiyo inayotakiwa, hali ya kuwa pato la mwaka la mtanzania liko chini ya $900/1,000,000 kwa mwaka. Hii ni sawa na ada kubwa ya kuingia kwenye soko kwa mpaka wakati huo soko la habari la kuingia bure.
Iwapo mtoa huduma za maudhui ni lazima aweze kulipa gharama zake za usajili, bado haiachi kusimamiwa kutokana na Electronic and Postal Communication Regulations. Kwa vyombo vya habari vya Tanzania, vimekosoa vikali matumizi ya kanuni hizi ilikuwa kufungiwa kwa Jamii Forums majira ya joto ya mwaka 2018. Zana nyingine kwenye kitendea kazi itakuwa cybercrimes Act kwa si kama itatumika kufunga tovuti mahususi tu, italeta tishio kwa kulinda data kwa sababu inawataka watoa huduma “kuarifu mamlaka ya uhimizaji sheria kuhusu shughuli yoyote au taarifa, habari husika zinazokiuka sheria na kubainisha mtu anatoa huduma kwa niaba ya nani iwapo ana uelewa sahihi wa taarifa inayokiuka sheria, au shughuli”
Kwa taarifa kuhusu kitendea kazi cha serikali cha kusimamia, angalia katika.
Chanzo
GSMA (2018). The Mobile Economy Sub-Saharan Africa 2018.
TanzaniaInvest (2013). Tanzania Leads East Africa’s Switch to Digital TV. Accessed on 22 October 2018.
Jacob Poushter, Caldwell Bishop, Hanyu Chwe (2018). Social Media Use Continues to Rise in Developing Countries but Plateaus Across Developed Ones. Pew Research Center. Accessed on 22 October 2018.
Mfonobong Nsehe(2018).Tanzania's Former Richest Man Rostam Aziz To Earn More Than $200 Million From Selling Vodacom Shares. Forbes.
Mnaku Mbani (2018). Rostam Aziz exits Vodacom Tanzania. Accessed on 22 October 2018.
Friedrich-Ebert-Stiftung (2015). AFRICAN MEDIA BAROMETER Tanzania 2015.
Tanzania Communications Regulatory Authority (2018). Electronic and Postal Communications Act, Licensing and Regulations
Tanzania Communications Regulatory Authority (2018). QUARTERLY COMMUNICATIONS STATISTICS. Accessed on 22 October 2018.
GeoPoll (2018). Custom study by GeoPoll Print and Online Audience Reach.
Reuters (2017). Bharti Airtel says purchase of Tanzania unit stake had government approval. Accessed on 22 October 2018.
Fumbuka Ng'wanakilala (2014). Viettel to invest $1 billion on 3G telecoms network in Tanzania: officials. Reuters. Accessed on 22 October 2018.
Fumbuka Ng'wanakilala (2018). Tanzania orders all unregistered bloggers to take down their sites. Reuters. Accessed on 22 October 2018.
Daniel Mumbere (2018). Tanzania cyber law introduces $900 fees for bloggers, compulsory passwords. Accessed on 22 October 2018.
Esther Karin Mngodo (2018). Jamii Forum founder speaks out on ‘government shutdown’. Accessed on 22 October 2018.
Hendrik Bussiek (2015). An Assessment of the New Tanzanian Media Laws of 2015.Friedrich-Ebert-Stiftung.
Vodacom Tanzania Limited (2018). Annual Report 2018.
Bharti Airtel Limited(2017). Annual Report 2016–17 p. 268-271.
Millicom (2016). Annual Report 2016.