Transparency
Kwa nini ni muhimu sana kwa wamiliki wa vyombo vya habari kusajiliwa kwa uwazi? Je, kwa nini kila mtu ni lazima ajue kama wamesajiliwa?
Kwa kawaida uwazi ndiyo zana bora zaidi kupambana dhidi ya rushwa na kutoa mwanga kuhusu uwezekano au migongano halisi ya kimaslahi kutokana na mtanzania wa kisheria, wamiliki wanahitajika kuwa rahisi kutafutwa au kufuatiliwa ili kuwawajibisha wao na kampuni zao za vyombo vya habari kwa sababu wao ndiyo wanaostahili kuwajibishwa mahakamani, kwa mfano hili huwajibishwa mahakamani, kwa mfano kwa kesi ya kuchapisha taarifa za kukashifu.
Taaarifa ya kina ya umiliki pia inaruhusu kutathimini wingi halisi au ukiritimba. Iwapo wamiliki wanapofanikiwa kujificha nyuma ya miundo tata ya shirika, inakuwa vigumu kupima ushawishi wao kwa jumla kwenye soko la vyombo vya habari.
Katika vyombo vya habari kuna kipengele kimoja ambacho kinamgusa kila raia. Ni muhimu kwa mtanzania mmoja mmoja kuelewa kuwa” ni nani ndiye mwenye chombo hicho”. Kwa sababu, utakapojua utaweza kuelewa motisha, ajenda na maslahi ya gazeti au chaneli ya utangazaji na utasoma habari, kwa njia tofauti.
Je nini masharti ya sasa ya uwazi?
Uwazi wa umiliki wa kampuni za vyombo vya habari unahakikishwa tu katika wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA) ambako wananchi wanaotaka, wafuate utaratibu wa kuomba wasifu wa kampuni. Taarifa hizo za kampuni ni lazima zikuhishwe kila mwaka, na pia kuhusu muundo wa wamiliki hisa. BRELA ina wajibu wa kuwakumbusha kampuni zisizofuata wajibu wao wa kupeleka taarifa zao. Wakala pia ina wajibu zaidi wa kuchukua hatua dhidi ya kampuni hizo, na kama hapana budi, kuzifutia usajili wan a kuzifungulia kesi za jinai dhidi ya wakurugenzi – wanapoendelea kushindwa kufuata sharia hata hivyo, kusema kweli, taarifa nyingi za kampuni ilizopata timu ya MOM zinaonesha taarifa hizo hazijahuishwa kwa zaidi ya miaka 5, bila ya kuchukuliwa hatua yoyote.
Je, utapata wapi taarifa za umiliki?
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inaruhusu kampuni au watu binafsi kuendesha na au kumiliki chombo cha habari cha utangazaji kwa TV, na redio au mtandaoni kampuni ya vyombo vya habari inataja na wakati mwingine hata kutaja wamiliki wa hisa wanapatikana kwenye tovuti ya TCRA – hata hivyo ni watoa maudhui mtandaoni tu.
Magazeti yanasajiliwa MAELEZO ambako hawana mamla ka ya kuchapisha data za umiliki. Kampuni zote, Pia kampuni za utangazaji ni lazima zisajiliwe kwa wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA). Taarifa za kampuni zenye majina ya wanahisa wakurugenzi waasisi n.k yapokinadharia tu baada ya kulipia ada ya (22,000 Tsh/10$)
Mwaka 2016, Bunge litunga sharia ya Access to Information, inayoruhusu, kuomba taarifa za umma, miongoni mwa nyingine ni taarifa ya umiliki. Sheria inamlazimisha mwenye taarifa kuchapisha kwa ukamilifu baadhi ya taarifa muhimu mara tu wanapozipata, au kuzitoa hata kama hakuna ombi la taarifa ya namna hiyo.
MOM walikagua uhalisia na kutathimini iwapo na namna taarifa za umiliki wa vyombo vya habari vinaweza kupatikana kwa umma, pamoja na kwa kiasi gani inataarifa za kutosha na za kuaminika kwa kiasi gani. Ili kufanya hivyo, tuliomba taarifa za umiliki katika mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), MAELEZO, na Wakala ya usajili waBiashara na Leseni BRELA).