Njia
Nadharia: Wingi wa vyombo vya habari ni muhimu kwa jamii zenye demokrasia
Wingi wa vyombo vya habari ni kipengele muhimu kwa jamii zenye demokrasia kuwa huru, zinazojitegemea na vyombo vya habari tofauti kuonesha maoni tofauti na kuruhusu ukosoaji kwa watu walio madarakani.
Kwa jumla unaweza kutofautisha wingi wa vyombo vya habari wa ndani unayoonesha jinsi tofauti za kijamii na za kisiasa zinavyoonekana katika maudhui ya vyombo vya habari (kwa mfano: uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kitamaduni, maoni au itikadi tofauti za kisiasa). Wingi wa vyombo vya habari wa nje unahusu idadi na miundo ya wamiliki pia unaojulikana kama “wingi” wa watoa habari.
Hatari ya mawazo mbalimbali husababishwa na wingi/mrundikano wa soko la vyombo vya habari – kinyume cha wingi wa vyombo vya habari –
- Pale ambapo vyombo vya habari vichache vinatumia ushawishi mkubwa kwa maoni ya umma na kuweka vikwazo vya kuingia kwa vyombo vingine vya habari na mitazamo (wingi wa umiliki wa vyombo vya habari)
- Pale ambapo maudhui ya vyombo vya habari ni ya namna moja na yamelenga tu kwenye mada mahususi, watu, mawazo na maoni (wingi wa maudhui ya vyombo vya habari)
- Pale ambapo hadhira inasoma, kutazama na kusikiliza baadhi ya vyombo vya habari tu (wingi wa hadhira ya vyombo vya habari)
Lengo: kujenga uwazi wa umiliki wa vyombo vya habari
Bila kujali kuwa wingi wa vyombo vya habari unajumuisha upeo mbalimbali na hukabiliwa na hatari nyingi, Ufuatiliaji wa Umiliki wa Vyombo vya Habari(MOM) unazingatia zaidi wingi wa vyombo vya habari wan je, na kwa uhakika zaidi katika wingi wa umiliki wa vyombo vya habari kama tishio linaloweza kuathiri wingi wa vyombo vya habari.
Kikwazo kikubwa cha kupambana nacho ni ukosefu wa uwazi wa umiliki wa vyombo vya habari: Je, watu wanawezaje kutathmini kuaminika kwa taarifa, iwapo hawajui ni nani anayetoa taarifa hiyo? Je, waandishi wa habari watawezaje kufanyakazi vizuri iwapo hawajui ni nani anadhibiti kampuni wanayoifanyia kazi? Je mamlaka ya vyombo vya habari yanawezaje kukabili wingi wa vyombo vya habari uliokithiri, iwapo hawajui ni nani anayeongoza vyombo vya habari?
Kwa hiyo, MOM inakusudia kujenga uwazi na kujibu swali la “ni nani hatimaye anadhibiti maudhui ya vyombo vya habari?”
- Kwa kueleza kuhusu mmiliki wa vyombo vya habari muhimu zaidi vya aina mbalimbali za vyombo hivyo, (ikiwemo televisheni, redio, intaneti, magazeti) na washirika wao;
- Kwa kuchambua ushawishi katika mchakato wa kuunda maoni ya umma kwa kuzingatia wingi wa hadhira;
- Kwa kutoa mwanga kuhusu usimamizi wa umiliki na wingi wa vyombo vya habari pamoja na utekelezaji wa sheria za usimamizi.
Maana yake: ukusanyaji wa taarifa na takwimu na kazi ya ugani
Kutokana na njia ya msingi, “MOM” imetayarishwa kama zoezi la uainishaji ili kuunda kanzidata inayopatikana kwa umma na inayohuishwa mara kwa mara yenye kuorodhesha wamiliki wa vyombo vya habari vya umma vyote. Inajenga uwazi kuhusu nani anayemiliki vyombo vya habari, ni maslahi na uhusiano gani walio nao wamiliki hao, ni kwa kiasi gani cha utegemezi walichonacho na ni nani hasa mwenye ushawishi kuhusu maoni ya umma. Kazi ya ugani hailengi kutafuta, ni nani wadau tu, bali kuchunguza ni nani hatimaye anadhibiti vyombo vya habari. Aidha, MOM inatoa uwekaji wa muktadha na uchambuzi wa ubora kwa kutathmini mahitaji ya soko yanayohusika na mazingira ya kisheria katika nchi mbalimbali pia.
Ukusanyaji taarifa na takwimu ulifanywa na timu ya utafiti ya nchini kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na Maripota Wasio na Mipaka (RSF).
Hati: Mwongozo wa Mtumiaji wa Ufuatiliaji wa Umiliki wa Vyombo vya Habari (MOM)
Ukusanyaji wa taaarifa na takwimu ulifanywa kwa kutumia Mwongozo wa Mtumiaji ufuatao na kushughulikia vifungu vifuatavyo:
- Kifungu A “Muktadha” kinatoa taarifa ya awali kuhusu soko la vyombo vya habari na hali ya mazingira yanayovizunguka kama vile mfumo wa usimamizi wa kisheria kuhusiana na masuala ya umiliki, taarifa kuhusu nchi na taarifa na takwimu zinazohusu vyombo vya habari. Sehemu hii inatoa fursa ya kuelewa zaidi matokeo ya sehemu ya sehemu zinazofuata na uwekaji wa muktadha wa hatari zilizokadiriwa kwa wingi wa vyombo vya habari.
- Kifungu B “Soko la Vyombo vya Habari”, aina za vyombo vya habari vilivyo muhimu kwa ajili ya kuunda maoni vinakubaliwa kwa msingi wa ufikiaji hadhira. Takribani vyombo 10 vya habari kwa kila aina – TV, redio, magazeti na intaneti vinachaguliwa.
- Kifungu C “Umiliki”, mmiliki/mdau/mtu mwenye ushawishi kwa chombo cha habari muhimu zaidi wanafanyiwa utafiti. Kampuni kuu muhimu ya vyombo vya habari zinafafanuliwa kiuchumi, (kuhusiana na mapato yao) na zinachunguzwa kuhusu sifa bainifu za umiliki wao.
- Kifungu D “Viashirio” hueleza viashirio vya kutathmini hatari kwa wingi wa vyombo vya habari.
Mwongozo wa Mtumiaji unatayarishwa kwa msingi wa utafiti wa umiliki wa vyombo vya habari uliyopo na wingi wa vyombo vya habari vyenyewe. Viashirio vinachochewa na kuwianishwa na ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (Media Pluralism Monitor) of the Centre for Media Pluralism and Media Freedom [ (CMPF) at the European University Institute (EUI, Florence).