Timu
MOM Timu
KAJUBI DIOCLES MUKAJANGA ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari la Tanzania (MCT). Kajubi amekuwa ripota, mhariri, mkufunzi wa vyombo vya habari na mchapishaji. Aidha, ni mshairi na mwandishi wa riwaya. Kwa takribani miongo miwili, amekuwa katika uongozi wa mashirika ya waandishi wa habari na kuwa kiongozi wa Media Institute of Southern Africa – Tanzania Chapter (MISA-Tan), the Association of Journalists and Media Workers (AJM), na MCT. Kajubi alikuwa rais wa World Association of Press Councils (WAPC). Mwaka 2016/2017 alishirikiana kuandika kwa pamoja na washauri wawili wa kimataifa, makala ya mradi kwa ajili ya Tanzania Media Fund (hivi sasa Foundation), na kufanikiwa kuzindua Mfuko huo. Ameandika au kuchangia katika vitabu 14 vikiwemo vitabu vya mafunzo kwa waandishi wa habari, maisha, mashairi na riwaya. Kajubi ni mtetezi mkereketwa wa uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari. Ni katibu wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Kamati zake zote.
MS. PILI MTANBALIKE ni Meneja wa Programu katika Baraza la Habari Tanzania (MCT). Ni mwandishi wa habari mkongwe mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 akifanyakazi katika nyadhifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na nje ya vyombo vya habari. Alianza kazi yake ya uandishi wa habari kama ripota mwaka 1982 katika Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA). Baadaye alijiunga na UNICEF mwaka 1992 alikofanyakazi katika Kitengo cha Vyombo vya Habari na Mawasiliano. Mwaka 1998 alijiunga na UNDP kama Mtaalamu wa Mawasiliano katika the National Multi sectoral HIV/AIDS Programme inayotekelezwa na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP). Alijiunga na MCT mwaka 2001 kama Ofisa wa Programu. Ms. Mtambalike ni miongoni mwa wanachama waasisi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania na kukitumikia kama Katibu Mkuu kuanzia mwaka 1992 mpaka mwaka 2000. Ni Mwanaharakati wa Haki za Binaadamu na ametumikia Bodi mbalimbali ikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) na Sikika, shirika lisilo la kiserikali linalofanyakazi ya kuboresha ushiriki wa raia, uwazi na uwajibikaji katika sekta ya afya. Pia alikuwa Mjumbe wa Bodi ya the Federation of African Media Women in the SADC Region. Hivi sasa anafanyakazi katika Bodi ya Tanzania Media Foundation (TMF) ambayo inatekeleza programu mbalimbali na kufadhili waandishi mmoja mmoja na vyombo vya habari kuhusu habari za kiuchunguzi na maslahi ya umma. Ms.Mtambalike pia amekuwa mwandishi mwenza wa vitabu viwili, kimoja katika Maadili ya Vyombo vya Habari na kingine kuhusu JInsia na Vyombo vya Habari. Vile vile aliandika vitabu viwili vya watoto, kimoja “Tuimbe na Kucheza”, kitabu cha Kiswahili cha watoto cha nyimbo za michezo, na kingine ni “Wimbo wa Sandina” kinachohusu ajira za watoto wa kike. Ms.Mtambalikeameandikia sana vyombo vya habari vya Tanzania na Kimataifa kwa kusisitiza zaidi masuala ya upendeleo katika haki za binadamu, jinsia na vyombo vya habari na maendeleo.
OLAF STEENFADT ni Mkuu wa Mradi wa MOM kwa Waandishi Wasio na Mipaka. Kwa miaka mingi amekuwa akishiriki katika kutoa ushauri na kufundisha kuhusu wingi wa vyombo vya habari, hasa katika ushirikiano wa maendeleo. Nyadhifa za mashirika ya kimataifa na taasisi zisizo za serikali zimemsaidia hasa kufanya kazi Ulaya ya KUsini Mashariki na chi za Kiarabu. Aliwahi kufanya kazi ARD na ZDF katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo, mtangazaji wa redio na televisheni, mwandishi wa habari za uchunguzi, mwandishi wa ndani na nje ya nchi pamoja na utayarishaji wa muundo na masoko ya kipindi. OLAF anafundisha historia ya vyombo vya habari, sera ya vyombo vya habari na sheria katika vyuo vikuu vya Ujerumani na Ulaya.
DR. MAURICESAMWILU MWAFFISI ni Mhadhiri wa Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma katika St. Augustine University of Tanzania, Kituo cha Dar es salaam. Amefanya kazi za uandishi wa habari na usumamizi wa vyombo vya habari katika vyombo vya habari vya binafsi na vya umma, vyombo vya habari vya elektroni na magazeti. Alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari za Redio Tanzania Dar es salaam, alipopandishwa cheo kuwa Mhariri Mkuu wa Habari Msaidizi. Alihamishiwa Tanzania School of Journalism ambako alifanya kazi kwa miaka 13 ambapo miaka 7 kati ya hiyo, alikuwa Mkuu wa Chuo hicho. Alifanyakazi katika IPP Media Group na kuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Habari na Matukio katika ITV/Redio One. Alikuwa pia Mhariri Mtendaji na Muasisi wa The Democrat, gazeti la kiingereza la kila wiki. Aliwahi kufanyakazi nyakati mbili tofauti kama Ofisa Habari Mkuu na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Tanzania (Maelezo). Alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Televisheni ya Taifa (TVT) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania wakati RTD na TVT zilivyounganishwa. Amestaafu katika utumishi wa umma mwaka 2017 baada ya kufikia umri wa lazima wa kustaafu. Baada ya kustaafu alifundisha Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kwa miaka sita kabla ya kuhamia St. Augustine University of Tanzania. Dr. Mwaffisi ameandika riwaya mbili za Distant Destination and Black Mercenaries. Amemwoa Mariam na wana watoto watatu.
GEORGE T. MASOUD is the Managing Partner at GMT ATTORNEYS and advocate of the High Court of Tanzania (and Courts subordinate there to except for the Primary court), Notary Public and Commissioner for Oaths, specializing in Research, Court work in all matters of Criminal and Civil Nature (Litigations), Labour disputes, Commercial law, Business and Human Rights, and Environmental Law. Worked with NSSF, Legal and Human Rights Centre for four years on the Corporate and Environmental unit. His experience includes provision of advice in Labour matters, Human rights and business, developing new business and the necessary requirements and regulations. He has also occasionally acted as company secretaryto some private companies.
Between 2013 to 2016, Mr. George had a stint with Legal and Human Rights Centre at which he gained a valuable experience on the area of Human Rights and Business.
Training and short couses attended
Research Techniques and Report Writing Skills, (2013) conducted by Legal and Human Rights Centre, Capacity building Skills by Legal and Human Rights Centre, (2014), Litigation skills and Prosecution Skills by National Social Security Fund, (2011/2013), Data Collection and Analysis ( Conducted by TRAFFIC and USAD), Human Rights Public Interest Litigation and Security Management ( Conducted by Tanzania Human Rights Defenders Coalition) and Postgraduate Diploma in Legal Practice at Law School of Tanzania (2013).
Publications
Coordinated the publication on Human Rights and Business Report-2014/2015 (prepared by Legal and Human Rights Centre), Assistant Researcher on Corruption and Whistleblowers Protection Report-2014 (prepared by Legal and Human Rights Centre) and Coordinated the Publication on Human Rights and Business Report-2015/2016 (prepared by Legal and Human Rights Centre).
Professional Memberships include: the Tanganyika Law Society and the East Africa Law Society and East Africa Law Society.
VINCENT MPEPO was born in Songea Town, Ruvuma Region. He is Assistant Lecturer in the Department of Journalism and Media Studies, Faculty of Arts and Social Sciences of the Open University of Tanzania. He teaches journalism and mass communication courses in undergraduate, diploma and certificate levels. He also supervises dissertation at undergraduate levels.
Mpepo is working with the Open University as Assistant Examination Officer, Faculty of Arts and Social Sciences. His research interests are on social media and communication. Vincent Mpepo graduated in 2017 Master of Arts in Mass Communication and first degree at School of Journalism and Mass Communication of the University of Dar es salaam in 2012.
LISA-MARIA KRETSCHMERni Mkuu wa Utfiti na Mratibu wa Mradi wa MOM duniani. Kama Meneja wa Mradi, Lisa pia ana wajibu wa utekelezaji wa mradi wa MOM nchini Tanzania.
Zamani alikuwa akifanya kazi katika uwanja wa Haki za Binaadamu na Uimarishaji, miongoni mwa shughuli nyingine alikuwa akifanyakazi katika Shirika la Maendeleo la Ujerumani (giz) na Mbunge wa Bunge la Ujerumani. Mwaka 2011, alisaidia mradi wa utafiti wa kimataifa kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika migogoro katika Ludwig-Maximilians-University Munich. Uzoefu wake huu unachangia kufanya kazi za MOM kama ilivyokuwa katika nyadhifa zake kwenye idara za mawasiliano na mashirika (ya kibiashara & yasiyo ya kibiashara) ili kuongeza uelewa kuhusu kero za haki za binaadamu. Amesoma mawasiliano ya kisiasa, uandishi wa habari na uchumi katika Germany (LMU Munich, FU Berlin), Uholanzi, Denmark na Israeli.
LUKAS BLANK anafanyakazi kama mwanagenzi kwa ajili ya MOM. Anasomea Uandishi wa Habari Mtandaoni katika University of Applied Sciences Darmstadt, katika Uandishi wa Kimataifa na Ulaya. Wakati wa mazoezi yake ya kila siku ya uanagenzi katika magazeti ya nchini na majarida ya jiji, amepata uzoefu wa kazi za uandishi wa habari. Hivi sasa ni mwandishi wa habari wa kujitegemea na huandikia zaidi vyombo vya habari vya nchini vya Darmstadt, Ujerumani.
Baraza la Habari Tanzania (MCT)
MCT ni chombo huru, chakujitolea na kinachojisimamia chenyewe. Kilianzishwa miaka ya 1990 kama chombo kisichokuwa cha kisheria na mbadala wa matarajio ya serikali kuhusu usimamizi na udhibiti wa vyombo vya habari. Tangu wakati huo, dhamira ya MCT ni kujenga mazingira yanayowezesha vyombo vya habari imara na vinavyozingatia maadili vinavyochangia zaidi kwenye jamii ya haki na demokrasia. Kwa kufanya hivyo ina...
- ... inahamasisha na kulinda uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari.
- ... inahimiza tasnia ya vyombo vya habari Tanzania kufuata viwango vya hali ya juu vya taaluma na maadili
- ... inahakikisha uwajibikaji wa vyombo vya habari
- ... na inahimiza uendelezaji wa wataalamu wa vyombo vya habari
Vilevile, MCT inatoa na kutengeneza vijarida, makala na ripoti kuelezea hali halisi ya vyombo vya habari nchini Tanzania.
Reporters Without Borders
Waandishi wasio na mipaka (Reporter Sans Frontières, RSF) ilianzishwa Montpellier (France) mwaka 1985 na waandishi wa habari wane. Imesajiliwa nchini Ufaransa kama shirika lisilo la kibiashara na lina hadhi ya ushauri katika Umoja wa Mataifa na UNESCO RSF inatetea uhuru wa vyombo vya habari, inasaidia vyombo vya habari vinavyojitegemea na kuwalinda waandishi wa habari walio hatarini duniani kote. Dhamira yake ni ...
- Kuendelea kusimamia mashambulizi ya uhuru wa habari duniani kote;
- Kulaani mashambulizi yoyote ya aina hiyo kwa vyombo vya habari
- Kufanyakazi kwa kushirikiana na serikali mbalimbali kupambana na udhibiti na sheria na kubana uhuru wa habari.
- Kuwasaidia kwa hali na mali waandishi wa habari waliohukumiwa pamoja na familia zao
- Kutoa msaada wa hali na mali kwa waandishi wa habari za vita ili kuhimarisha usalama wao.
Tangu mwaka 1994, kitengo cha Ujerumani kinafanyakazi sana jijini Berlin. Ingawa kitengo cha ujerumani kinafanyakazi kwa karibu na Sekretarieti ya Kimataifa ya mjini Paris kutafiti na kutathmini uhuru wa vyombo vya habari duniani, inajitegemea kwa fedha na uendeshaji. Kwa wajibu huo, imeomba ruzuku kutoka federal German Ministry for Economic Cooperation and Development – ili kugharimia mradi wa MOM.