This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/07/18 at 15:30
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Kanzi data ya Kampuni

Juhudi za kuanzisha kanuni ya usimamizi wa vyombo vya habari mtambuko zimechelewa kuja. Wakati wadau wa vyombo vya habari walikwisha weka mada hiyo kwenye ajenda mwanzoni mwa millennia, serikali imesitisha. Hali hii imeruhusu kampuni chache za vyombo vya habari mtambuko kukua – kama vile IPP Media Ltd, ambayo hivi sasa ni miongoni mwa kampuni kubwa sana za vyombo vya habari Afrika Mashariki au Clouds Entertainment. 

Wakati wingi halisi wa vyombo vya habari mtambuka hauwezi kujulikana kutokana na kukosekana kwa data za soko, baadhi ya kampuni zinatoa huduma maarufu kwenye aina za vyombo vya habari, kiasi kwamba vitakuwa na uwezekano wa kuwatoa washindani au kufikia hatua hiyo baadaye. Kukosekana kwa data za soko kunazuia kuandika na kutekeleza kanuni za vyombo vya habari zenye ufanisi kwa kuwa mamlaka za usimamizi haziwezi kufanya uamuzi unaotokana na hoja na hatua za kisheria . 

Vyombo vya habari vya serikali na IPP Media vinafanyakazi kwa ukamilifu katika sekta zote nne za vyombo vya habari. Sahara Media Group ililazimika kusimamisha shughuli zake cha uchapishaji, na hivi sasa inafanyakazi katika TV, redio na Mtoa Maudhui Mtandaoni.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ