This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/12/11 at 04:28
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Maudhui

Vyombo vya habari vya Tanzania haviishi katika ombwe, bali vinategemea sana muktadha wa siasa, sheria na jamii wan chi. Wingi na aina ya vyombo vya habari nchini Tanzania vimekuwa kutokana na mabadiliko ya historia na siasa katika vipindi vya ukoloni, uhuru, muungano wa sehemu kubwa ya bara ya Tanganyika na visiwa vya mwambao vya Zanzibar, nyakati za ujamaa na kujitegemea, na kuanzishwa kwa mfumo wa siasa ya vyama vingi.

Pia itategemea muundo wa sheria unaohakikisha uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari, na kuhimiza vyombo vya habari – ingawa baadaye vinawekewa sheria na kanuni kali hasa kwa lengo la kujaribu kudhibiti hoja na taarifa mtandaoni. Wakati huo huo, haishughulikii masuala ya wingi (mtambuko) na uwazi wa vyombo vya habari.

Kwa kuangalia hali ya uchumi, matangazo yanayowekwa kwenye utaratibu wenye utata. Vyombo vya habari vya umma kwa kiasi kikubwa vinapata fedha za taifa na kwa njia ya matangazo.

Sifa bainifu za jamii ya Tanzania, kuanzia viwango vya kusoma, kuandika na hesabu hadi tabia za utumiaji  wa vyombo vya habari, kutambua ni vyombo vipi vya habari au aina gani inatawala, na vinavyosemekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa maoni ya watu.

Katika mwongo uliyopita, Tanzania imekabiliwa na mawimbi mengi ya teknolojia mpya, ambayo imebadili namna watu wanavyowasiliana na kutumia habari na taarifa.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ