This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2022/08/10 at 07:28
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

John B. Mahega

John B. Mahega

John Benard Mahega, ni Mtanzania, Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpekuaji Media inayoendesha Blogi ya Mpekuzi Huru. Blogi ya Mpekuzi Huru ni ya Tanzania inayotoa Habari za Brudani, Habari za Siasa, Umbeya wa Wattu Mashuhuri na Taarifa mbashara za hivi karibuni. Mtandao wake wa facebook ulianzishwa mwaka 2009.

Mahega haonekani kabisa hadharani. Wasifu wake wa Linkedin nao unatoa taarifa chache sana; hata hivyo alianza kufanyakazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Mpekuzi, mwaka 2012. Mafunzo kwa Vitendo Tanzania Telecommunication Company Limited (TTCL) yametajwa. Ana Shahada ya kwanza katika Uhandisi wa Simu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), mwenzi wake wa biashara na mmiliki mwenza ni Hellen.

Elibariki Mcharo mwenye 10% ya hisa na hakuna taarifa zaidi zinazomuhusu Hellen. Wasifu wa Kampuni hiyo haupo kwenye Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ