Clouds TV
Ilizinduliwa mwaka 2010 kama kituo cha TV cha binafsi jijini Dar es salaam na inamilikiwa na Clouds Media Group inayoendesha pia Clouds Redio, Coconut FM na Choice FM. Ni ya nne miongoni mwa vituo vya TV vinavyoangaliwa sana nchini Tanzania yenye XX.XXX% ya hadhira kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll wa robo ya pili ya mwaka.
Ni kituo chenye vipindi vya vijana na ndivyo vilivyofanya kuwa Clouds TV kuwa TV nambari moja katika kipengele cha vijana na kituo cha kwana kuunganishwa kwa ukamilifu na mitandao ya kijamii na kushirikishwa na kila inapotangaza.
Mchanganyiko wa vipindi vya tamthilia zilizotengenezwa nchini na sinema za mapenzi na za matukio halisi na kuchanganya na habari za matukio makubwa na vipindi vilivyotayarishwa kwa uchambuzi wa kina kuhusu mitindo ya maisha imefanya kituo kipendwe zaidi na vijana ambao ni 60% ya Watanzania.
Licha ya habari na matukio, kituo hiki pia kinatangaza vipindi vya aina mbalimbali, kuanzia miziki mbalimbali, vipindi maalumu mijadala na habari za burudani, sinema za mapenzi, burudani na michezo.
Kituo hiki kinamilikiwa na Clouds Media Group ambapo Joseph Kusaga, mjasiriamali maarufu na mwasisi mwenza, ni mtendaji mkuu. Kusaga alianza kama DJ na alifanya matamasha na disko nchini kote Tanzania kabla ya kuanzisha kwa ubia C.L.O.U.D.S (Cool, lovable, Outrageous, Unique, Sound) FM. Tangu kuanzishwa kwa Clouds, Kusaga ameendelea kujenga kampuni za vyombo vya habari vyenye mafanikio, ukarimu na teknolojia.
Taarifa kuhusu Clouds Media Group si rahisi kupatikana; Kampuni hii haikusajiliwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wala namba yake ya uandikishaji ili kupata wasifu wa kampuni katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Taifa
Aina ya maudhui
Free to Air
Kampuni ya vyombo vya Habari
Clouds Entertainment Co. Limited
Muundo wa umiliki
Clouds Television Limitedni ya kwanza miongoni mwa vituo vya TV na kumilikiwa na Clouds Entertainment Limited, ambayo ni mali ya Kusaga na familia yake. Kwa mujibu wa data za TCRA na BRELA.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Kampuni
Mmiliki Binafsi
Kundi / Mmiliki Binafsi
Alex Mkama Kusaga
ni baba mzazi wa Joseph Kusaga, muasisi wa Clouds Entertainment Limited. Amefariki Afrika Kusini mwaka 2009 na alizikwa Dar es Salaam 7t Novemba 2009. Hadi 2018, bado ameorodheshwa kuwa mmiliki wa hisa.
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
2010
Mwanzilishi
Joseph Kusaga - alipenda muziki tangu mdogo. alianza kuendesha matamasha tangu akiwa chuoni akisomea elektoniki, akiwa DJ maarufu na mtayarishaji matamasha. Alipata wazo la kuanzisha kampuni ya vyombo vya habari wakati alipotembelea USA, alipoungana na m
Mtendaji Mkuu
Joseph Kusaga - angalia hapo juu
Mhariri Mkuu
Ruge Mutabaha - Mkurugenzi wa Vipindi
Mawasiliano
Clouds Media Group
P.O: Box 311513, Dar-Es-Salaam;
Tel.: +255222781445
E-Mail: info@cloudsmedia.co.tz
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kiwango cha hadhira kwa mujibu wa ripoti ya viwango vya GeoPoll ya Redio & TV (Aprili – Juni 2018).