Global Publishers & General Enterprises Limited
Global Publishers & General Enterprises Limited ni kampuni binafsi iliyosajiliwa na kushughulikia uchapishaji wa magazeti ya kila siku nchini Tanzania. Kampuni inamiliki magazeti sita ya Amani, Championi, SpotiXtra, Ijumaa, Risasi na Uwazi yenye wito wa “Kampuni ya Magazeti Pendwa”. Magazeti yote yanatumia Kiswahili. Kampuni hii pia inamiliki Online Television inayojulikana kama “Global TV Online”
Maudhui ya magazeti ya Global Publishers & General Enterprises Limited yanahusu siasa, watu mashuhuri, hadithi fupi, burudani, michezo na umbeya, ni mambo yanayosababisha kuwa na aina ya uandishi wa habari za kusisimua za udaku.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (2018), kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Limited inamilikiwa na Joachim Lusana Buyobe kwa 100%. Buyobe pia anamiliki Geita online TV kwa 100%. Hakuna taarifa zaidi kuhusu Buyobe.
Kwa upande wake Eric James Shigongo anaonesha kuhusika kwa karibu na kampuni. Anatajwa kuwa ni Ofisa Mtendaji Mkuu, Mkurugenzi na Msimamizi wa Global Group – wakati mwingine huwa ni mmiliki wa tovuti nyingi. Pia huwa anaitaja kampuni kwenye facebook yake. Nafasi yake haifahamiki kwa sababu wasifu wa kampuni yake haukupatikana katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kampuni hiyo haikujibu maswali ya mahojiano.
Shigongo amejipatia umaarufu kama mjasiriamali, mwandishi wa vitabu na msemaji. Amezaliwa Mwanza kwenye fukwe za ziwa Victoria, amekuwa na uthubutu wa mambo mengi, ikiwemo vyombo vya habari, hoteli, kilimo, milki na uendelezaji ardhi na majengo.
Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (2018), kuhusu kiwango cha wasomaji, Global Publishers & General Enterprises Limited inachapisha magazeti pendwa Tanzania kama vile Champion (XX.XXX%) (ni la 5 kwa wasomaji) pamoja na Risasi na Ijumaa, yenye XX.XXX% kila moja (nafasi ya 13 na 14) kati ya magazeti 28 ikiwemo magazeti makuu yanayochapishwa nchini.
Aina ya Biashara
Binafsi
Mfumo kisheria
Kampuni ya dhima yenye kikomo
Nyanja za Kibiashara
Global Publishers & General Enterprises Limited imesajiliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutoa huduma za magazeti na huduma mtandaoni.
Joachim Lusana Buyobe
Raia wa Tanzania hajionyeshi. Pia anamiliki Geita online TV kwa 100%.
Magazeti mengine
Amani
Risasi
Ijumaa Wikienda
Sporti-Extra
Uwazi
Championi
Ijumaa
Digitali nyingine
globalpublishers.co.tz
youtube.com/user/uwazi1/
Chombo cha habari cha kibiashara
Mchapishaji Magazeti
Global Publishers & General Enterprises Limited
Huduma za Maudhui Mtandaoni
Global Publishers and General Enterprises Limited
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
1998
Mwanzilishi
Abdallah Mrisho Salawi hakuna taarifa zaidi kuhusu mwasisi mwenza.
Eric Shigongo - ni mjasiriamali, mwandishi wa vitabu na msemaji. Alizaliwa Mwanza, kwenye fukwe za ziwa Victoria, ana kampuni mbalimbali zikiwemo vyombo vya habari, hoteli, kilimo, uendelezaji milki na nyumba. Ni mwandishi maarufu anayeandika hadithi mfululizo kwenye magazeti na riwaya.
Waajiriwa
Taarifa zisizopatikana
Mawasiliano
Global Publishers & General Enterprises Limited;
P. O. Box 7534, Dar-Es-Salaam;
Namba ya kutambulika
BRELA Incorporation N°38971
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Utawala
Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji
Taarifa zisizopatikana
Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji
Taarifa zisizopatikana
Bodi ya usimamizi + Bodi Maslahi ya usimamizi
Taarifa zisizopatikana
Watu muhimu wenye ushawishi + watu maslahi wengine muhimu
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Kampuni imesajiliwa BRELA. Wasifu umeombwa bado haujajibiwa.Imesajiliwa TCRA. Madodoso hayakurudishwa