This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2022/08/10 at 06:23
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Familia ya Michuzi

Familia ya Michuzi

Michuzi Midea Group inamilikiwa kwa pamoja na Issa Michuzi (50%), Othman Atick Michuzi (10%), Ahmad Issa Michuzi (10%) na kwa mujibu wa data katika Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) (2018) pia Christopher Mtakyawa Makwaia anamiliki (15%).

Muhidini Issa Michuzi anamiliki nusu ya hoisa za kampuni na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji. Yeye ni mwandishi wa habari na mpiga picha Mtanzania. Anafahamika kwa kuanzisha Michuzi Blog miaka ya 2000, miongoni mwa blog za kwanza nchini Tanzania zenye kutoa taarifa muhimu.

Michuzi alikuwa na shauku na kupenda upigaji picha tangu miaka ya 1980, iliyo, lazimisha kujiunga na masomo ya jioni ya mpigaji picha Geothe-Institute, Dar es salaam. Ili kulipia ada yake ya masomo, ameshiriki katika kupiga picha kwenye shughuli nyingi za kijamii, Dar es Salaam zikiwemo klabu za disko. Moja ya picha zake ilichaguliwa kuwekwa ukurasa wa mbele wa DailyNews, gazeti linalo milikiwa na Serikali. Hatimaye aliajiriwa kama mwanagenzi kwa miaka mitatu kabla ya kuajiriwa rasmi tarehe 1 Januari 1990. Mwaka 1992, alijiunga na International Institut fur Journalim, Berlin kwa ajili ya kozi ya juu ya mwandishi habari na upigaji picha. Baadaye alijiunga na Tanzania School of Journalism (ambayo sasa ni Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano na Umma-SJMC) ya Chuo kikuu cha Dar es salaam na kuhitimu mwaka 1996.

Kusudio kuu la kuanzisha blog ni kuwaarifu Diaspora ya Tanzania kuhusu habari zinazohusiana na nchi yao kwa njia ya blog ya picha. Alikutana na Ndesanjo Macha aliyemsaidia kuanzisha blog mwaka 2005, wakati wa mkutano uliokuwa Finland, alikokuwa kwenye msafara wa Waziri wa Mambo ya Nje Jakaya Kikwete. Blog ya kwanza ilianza tarehe 8 Septemba 2005.

Mwaka 2006 alipewa ufadhili wa masomo kuhudhuria kozi maalumu ya upigaji picha kidigitali, Cardiff, Wales na tangu wakati huo amehusiana na DailyNews.

Michuzi ana ndugu wake wawili-Ahmad na Othman ambao pia waendesha blog maarufu nchini Tanzania. Kwa pamoja wanaunda Michuzi Media Group (MMG). Ni kwenye nyaraka zilizotolewa na BRELA ndipo Christopher Mtakyawa Makwaia (15% ya hisa) ametajwa kuwa ni mmliki wa nne. Katika TCRA, ni ndugu wa michuzi tu ndiwo walioorodheshwa kama wamiliki wa hisa.

Hakuna taarifa zilizopatikana kuhusu Christopher Mtakyawa Makwaia.

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ