Michuzi Media Group Co. Limited
Michuzi Media Group Company Limited ni miongoni mwa blogi za kwanza nchini Tanzania zinazoshughulika na usambazaji wa habari mpya Tanzania na nchi za nje. Inatumia Kiswahili na mara nyingi hutoa habari kutoka kwa wanasiasa, serikali na jamii kwa jumla. Ilizinduliwa mwaka 2005.
Kwa mujibu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (2018), Michuzi Blog ni mali ya familia ambapo Muhidin Issa Michuzi ana 50% ya hisa, Ahmad Issa Michuzi 10%, Othman Adam Michuzi 10% na Christopher Mtakyama Makwaia anamiliki 15%. Haikuelezwa ni nani anayemiliki 15% zilizobaki.
Muhidin Issa Michuzi , mwandisgi mpiga picha alianzisha kampuni na ndugu zake Ahmad na Othman nay eye ni Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu, kwa mujibu wa wasifu wa facebook. Hakuna taarifa kuhusu Christopher Mtakyawa Makwaia. Wanahisa pia wanafanyakazi kama wakurugenzi kulingana na taarifa za kampuni kutoka BRELA
Michuzi Blog inashughulikia hasa masuala yanayohusu siasa na miongoni mwa wakala za matangazo ikilinganishwa na blog nyingine nchini. Kwa mujibu wa utafiti wa utumiaji wa vyombo vya habari wa GeoPoll (Agosti 30 – Sept 1, 2018), Michuzi blog inasomwa na 1% ya hadhira ya Tanzania na 2% ya Dar es salaam na Morogoro.
Ofisi rasmi iliyosajiliwa Namanga kwenye Barabara ya Alli Hassan Mwinyi , kiwanha Na. 14/13 Kinondoni, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa BRELA (2018), Hakuna taarifa ya mapato ya mwaka iliyopelekwa BRELA kwa miaka 5 mfululizo kuanzia 2013 hadi sasa.
Aina ya Biashara
Binafsi
Mfumo kisheria
Kampuni ya dhima yenye kikomo
Nyanja za Kibiashara
Michuzi Media Group Co. Limited imesajiliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutoa huduma mtandaoni. Kampuni ya Michuzi Media Group pia imesajiliwa TCRA kama Mtoa Huduma za Maudhui Mtandaoni
Mmiliki Binafsi
Muhidin Issa Michuzi – ni Ni mwandishi wa habari mpigapicha. Anafahamika zaidi kwa kuanzisha blogi ya Michuzi Blog miaka ya 2000, ni miongoni mwa blogi za kwanza zenye maudhui yenye maana. Aliajiriwa kama mwandishi wa kujitolea kwa miaka 3 Daily News kabla ya kuajiriwa rasmi tarehe 1 Januari, 1990
Digitali nyingine
issamichuzi.blogspot.com
Chombo cha habari cha kibiashara
Mtoa Huduma Mtandaoni /Mitandao ya Kijamii
Michuzi Media Group Co. Limited
Biashara
Ni biashara ya vyombo vya habari tu
Hakuna
Maelezo yote
Mwanzilishi
Muhidin Issa Michuzi – anamiliki nusu ya hisa za kampuni na ni Menyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu. Ni mwandishi wa habari mpigapicha. Anafahamika zaidi kwa kuanzisha blogi ya Michuzi Blog miaka ya 2000, ni miongoni mwa blogi za kwanza zenye maudhui yenye maana.
Waajiriwa
Taarifa zisizopatikana
Mawasiliano
Michuzi Media Group Co. Limited
P. O. Box 933
DAR ES SALAAM
Tel: +255717618997
Namba ya kutambulika
BRELA Incorporation N°90165
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Utawala
Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji
Director
Director.
Director
Director.
Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji
Taarifa zisizopatikana
Bodi ya usimamizi + Bodi Maslahi ya usimamizi
Taarifa zisizopatikana
Watu muhimu wenye ushawishi + watu maslahi wengine muhimu
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Company profile available at BRELA and TCRA. No return of questionnaires.