Millardayo.com
Millardayo.com ni miongoni mwa tovuti ya habari nchini Tanzania inayoendeshwa na kumilikiwa na Millard Afrael Ayo na ndugu yake. Tovuti hiyo imeanzishwa mwaka 2012 na Ayo na kuipa jina lake.
Kuanzishwa kwa Millardayo.com kumechangiwa zaidi na Issa Michuzi, mwendesha blog mkubwa nchini Tanzania, na Ambwene Yesaya ambaye ni mwanamziki maarufu nchini Tanzanian na rafiki mkubwa wa Ayo. Walimshauri aanze blog kuhusu visa na habari alizokuwa akizitangaza Clouds FM radio kwa kuwasaidia wale waliokosa kusikiliza redio.
Millardayo.com ilitajwa kama njia ya pili maarufu kupasha habari kwenye utafiti uliyogharimiwa na MCT (Aug/Sep) wa GeoPoll kuwa na hadhira ya XX.XXX%. Pia kwa mujibu wa Alexa Traffic, Millardayo.com ilikuwa ya 19 (Oct 2018). Maudhui ya Millardayo.com yanahusu habari za kawaida kama vile za nchini, kanda na kimataifa, habari za burudani, kijamii, kisiasa na habari za maisha ya watu binafsi (umbeya)
Hivi sasa Millard Ayo inasimamia na kuajiri zaidi ya wafanyakazi 13 wanaofanyakazi kama waandishi na wapiga picha. Licha ya blog hii (Millardayo.com), habari zinaweza kupatikana YouTube, Google Play & Apple Store, Facebook Twitter @millardayo na Instagram zenye wasomaji 3.9 milioni.
Mwaka 2012, Millardayo.com ilishinda tunzo mbili kutoka nyota wa Africa na Vodacom kuwa tovuti bora zaidi Tanzania.
Blog hiyo inaendeshwa chini ya Ayo TV TZA Company Limited iliyoanzishwa na kumilikiwa na Millard Afrael Ayo (anamiliki hisa 900) na Ivan Ayo (anamiliki hisa 100).
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Kimataifa
Aina ya maudhui
Maudhui huru
Kampuni ya vyombo vya Habari
AYO TV TZA Company Limited
Muundo wa umiliki
Millardayo ni Mtoa Taarifa Mtandaoni iliyosajiliwa TCRA, imeanzishwa na kumilikiwa kwa ubia na Millard A. Ayo.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Kundi / Mmiliki Binafsi
Ivan Ayo
ndugu yake Millard A. Ayo.
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
2012
Mwanzilishi
Millard Afrael Ayo - alizaliwa tarehe 16 Januari, 1986 nchini Tanzania. Alianza kufanyakazi kama mtaalamu wa vyombo vya habari na kuanzisha kwa ubia blogi yake iliyojipatia tuzo. Bado anaendelea kufanyakazi na Clouds Media kama mtangazaji.
Mtendaji Mkuu
Millard Afrael Ayo - angalia hapo juu
Mhariri Mkuu
Hakuna taarifa kuhusu chumba cha habari
Mawasiliano
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
AIdadi ya hadhira kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Aug 30 – Sep 1st, 2018), uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Mitandao ya kijamii, tovuti za kutafuta habari, na tovuti za matangazo hazikuingizwa kwenye uchambuzi wa umiliki.