Jamii Forum
Jamii Forum ni mtandao wa kijamii wa Tanzania ulianzishwa kama Jambo Forums katika miaka ya 2006. Unafanya kazi chini ya Jamii Forums Company Limited iliyosajiliwa Julai 2008.
Kwa mujibu wa Maxence Melo, Mwasisi-mwenza na mmiliki-mwenza, Jamii Forums imetokana na Jambo Forums iliyokuwa na majukwaa madogo mengi ya mtandaoni kama vile Tanzania Economic Forums, Habari Tanzania, Uchaguzi Tanzania, Jambo Network, Jambo Redio na Jambo Video.
Kusudio kuu la kuanzisha Jamii Forums, kwa mujibu wa Melo, ni kuunda jukwaa ambapo jamii ya kitanzania inaweza kushiriki kwenye mjadala huru kuhusu masuala mbalimbali yanayojitokeza kama vile ya kijamii kisiasa, kiuchumi na ripoti za habari zinazotokea hivi punde.
Kulingana na utafiti wa GeoPoll kuhusu matumizi ya mitandao, uliyodhaminiwa MCT, Jamii Forums ni tovuti ya kwanza kwa habari yenyeXX.XXX% ya hadhira. Kwa mujibu wa Alexa Traffic, ni ya tano miongoni mwa mitandao ya kijamii nchini (Oktoba, 2018). Taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inasema kwamba, mtandao huo una watumiaji 2.4 milioni,walipiaji wa simu za mkononk 2.8 milioni na takribani watu 600,000 wanaotumia mtandao huu wa kijamii kila siku, mwezi Agosti 2017.
Maudhui ya Jamii Forums yanashughulikia habari za kawaida na hutoa fursa ya majadiliano ya masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, michezo na burudani. Licha ya kwenye blog hii, habari zipo kwenye Google Play, Instagram, Facebook, Twitter @Jamii Forums, pamoja na Youtube.
Mwezi Juni 2018, Jamii Forums ilifungiwa kutokana na wamiliki wake kuchelewa kulipa ada ya usajili kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyotakiwa kulipwa kulingana na kanuni mpya ya maudhui ya mtandaoni (Online Internet Regulation). Kwa mujibu wa kanuni hii mpya, wamiliki wa blog/majukwaa ya mtandaoni wana wajibu wa kulipa hadi Tsh 2.1 milioni, pamoja na Tsh 1 milioni kwa ada ya Leseni ya awali kabla ya kuanza kuendesha forums zao. Wanatakiwa pia wataje taarifa za wanahisa wao, uraia wao na mtaji wa hisa.
Kanuni hiyo pia inawataka wamiliki wa blog na waendeshaji wa Forums kujisajili TCRA, kuhakikisha kuwa maoni yanayotolewa na wasomaji wa blog, watumiaji wa Forums ni ya wastani kabla ya kuchapishwa. Aidha wanatakiwa pia kubainisha chanzo cha maudhui.
Melo alieleza kuwa vyombo vya habari kuhusu kufungiwa huko:”Tumelengwa kwa sababu Forum yetu ni mtoa huduma na si mtoa maudhui, kwa hiyo tuliamua kufunga kwa sababu hatuna nafasi yoyote (kwenye kanuni za maudhui ya mtandao)”.
Mwezi Julai 2018, TCRA ilitoa Online Content Services Licence kwa Jamii Forums kwa hiyo iliendelea kutoa huduma baada ya kutimiza matakwa ya kanuni hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya kampuni zenyewe, kampuni inayoendesha shughuli zake iliasisiwa na kumilikiwa na Maxence Melo Mubyazi (51%) na Mike Mushi (49%)
Isa za hadhira
Aina ya umiliki
Binafsi
Maeneo yanayofikiwa
Kimataifa
Aina ya maudhui
Maudhui huru
Kampuni ya vyombo vya Habari
Jamii Media Co. Limited
Muundo wa umiliki
Jamii Forum ni Mtoa Taarifa Mtandaoni iliyosajiliwa TCRA. Katika TCRA, ni Melo tu ndiye aliyetajwa kama mmiliki wa hisa. Kwenye akaunti zao wenyewe pia Mushi anamiliki hisa zilizobaki.
Haki ya kuchagua
Taarifa zisizopatikana
Mmiliki Binafsi
Kundi / Mmiliki Binafsi
Mike Mushi
Muasisi mbia wa Jamii Forums tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 tu. Alianza kusimamia Jamii Forums mara tu alipomaliza shule ya msingi ya Green Acres mwaka 2003. Hivi sasa ni Mkurugenzi na Mkuu wa Ubia wa Biashara na Masoko katika Jamii Media. Amesoma shahada ya Business Administration with Information Technology katika Learn IT kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013.
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
2nd July, 2008
Mwanzilishi
Maxence Melo – ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi (BSc) katika Uhandisi Majengo na amefanyakazi katika kampuni ya ujenzi kabla ya kuanzisha kwa ubia Jamii Forums. Pia ni mwanaharakati wa kidijitali anayehamasisha uhuru wa kutoa mawazo, usalama wa kidijital
Mtendaji Mkuu
Maxence Melo - angalia hapo juu
Mhariri Mkuu
Hakuna taarifa kuhusu chumba cha habari
Mawasiliano
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Isa katika soko
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Idadi ya hadhira kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Aug 30 – Sep 1st, 2018), uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Mitandao ya kijamii, tovuti za kutafuta habari, na tovuti za matangazo hazikuingizwa kwenye uchambuzi wa umiliki.