Dr. Anthony Diallo
Dkt. Anthony Diallo, ni mwanasiasa na mbuge wa zamani, ni mwasisi wa Sahara Media Group Limited, kampuni ya vyombo vya habari inayoendesha Star TV, Radio Free Africa na Kiss FM, na makao yake jijini Mwanza. Hakuna data za umiliki wa Sahara Media Group kwenye Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), tovuti nyingi zinamtaja Diallo kuwa ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo.
Dkt. Diallo, ambaye hivi sasa ni Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Mapinduzi CCM) wa Mkoa wa Mwanza alikuwa mbunge anayewakilisha jimbo la Ilemela mkoani Mwanza kuanzia mwaka 1995 hadi Oktoba 2010, alipopoteza kiti hicho kwa mgombea wa Chama cha Upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ametumikia nyadhifa mbalimbali katika baraza la mawaziri kuanzia mwaka 2000 hadi 2008. Alikuwa naibu wa Waziri wa Biashara na Viwanda, Naibu Waziri wa Maji na Mifugo na Waziri wa Maliasili na Utalii.
Dkt. Diallo anashughulikia biashara-mtandao (e-Business), Serikali-mtandao (e-Government) na utekelezaji wa mifumo. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika Nyanja za utengenezaji bidhaa, ununuzi na kupanga uzalishaji.
Kabla ya kujiunga kwenye biashara ya vyombo vya habari, mwaka 1992, Dkt Diallo alikuwa mwasisi mwenza wa DM investment Co. Ltd, miongoni mwa kampuni kubwa zaidi za uhandisi na utengenezaji bidhaa nchini.
Kampuni iliyofungwa mwaka 1994 ilitengeneza Bidhaa za Sahara za vyombo vya umeme, mashine za kilimo, injini za dizeli za “single stroke” na mitambo ya viwandani kwa ajili ya viwanda vya uchakataji wa bidhaa za kilimo.
Dkt Diallo alizaliwa 25 Desemba, 1956 ana shahada ya kwanza ya Sayansi (BS – eB) katika biashara mtandao (e-Business) kutoka Chuo Kikuu cha Phoenix, Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha NewCastle, Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Kitaifa kutoka Chuo Kikuu cha Phoenix (MM-I), na Shahada ya Uzamivu katika Usimamizi wa Biashara (BDA) kutoka Chuo Kikuu cha NewCastle (2008).
Pia ana stashada ya Uzamili katika Usimamizi wa Teknolojia kutoka Maastricht School of Management, NL na Mhitimu wa Advanced Management Program wa Harvard Business School, Boston, USA (1994).
Biashara
HISTORIA YA AJIRA
UZOEFU WA SIASA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Member of National Executive Council(MNEC) 2002 To Date
DM Investments
Managing Director: 1992
General Manager: 1982
Project Manager: 1979
General Health
Sales Officer: 1978
Mwanza Chemist
Managing Director: 1973 - 1975
Mwananchi Dispensary
Dispensary Assistant: 1971 1972
Roman Catholic
Mission Clerk: 1969
Ministry of Livestock Development
Minister 10/17/2006 - 2/8/2008
Ministry of Natural Resources and Tourism
Minister 1/1/2006 - 10/16/2006
Ministry of Water and Livestock
Deputy Minister: 2001 - 2005
Ministry of Industry and Trade
Deputy Minister: 2000 - 2000
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
District Political Committee Member 1995 To Date
Parliament of Tanzania
Member of Parliament of Tanzania: 1995 - 2010