Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Chama cha Mapinduzi (CCM) ni muungano baina ya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro- Shirazi Party (ASP), Vyama viwili vya siasa vilivyoongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanzania bara na Zanzibar , mtawalia. Vyama hivyo viliungana tarehe 5 Februari, 1977.
Hivi sasa CCM inamiliki UHURU Media Group (UNG) yenye uhuru Publications Limited (UPL) inayochapisha gazeti la kila siku la Kiswahili la UHURU na toleo lake la Jumapili la MZALENDO na People’s Communication Media inayomiliki Redio UHURU, CCM inatarajia kuwa televisheni mwezi February 2018.
Historia ya CCM kumiliki vyombo vya habari inaanzia 7 Julai 1954 wakati TANU ilipoundwa na mara tu baada ya hapo ilianzisha gazette lake la SAUTI YA TANU lililokuwa linashauriwa na rais wa chama Mwalimu Nyerere ambaye baada ya uhuru alikuwa Rais wa Kwanza na Baba wa Taifa.
TANU ilijaribu kuanzisha gazeti la ligha ya Kiingereza , National Times mwaka 1959 ili kutaka sauti yake isikike kwa wasioongea Kiswahili nchini. Hata hivyo hakukuwa na mtaji wa kutosha kwa ajili ya mradi huo na hivyo kuahirisha. Hata hivyo TANU ilidhamiria kuwa na magazeti ya Kiswahili na Kiingereza . Kwa hiyo siku ya Uhuru 9 Desemba1961, TANU ilizindua UHURU gazeti la wiki na baadaye la kila siku. UHURU limekuwa mbadala wa SAUTI YA TANU . tarehe 30 Aprili, 1972, TANU ilizindua MZALENDO , kuwa toleo la Jumapili la UHURU. TANU ilianzisha gazeti la Kiingereza la Nationalist tarehe 17 April 1967 la kila wiki halafu kila siku. TANU iliunganisha The Nationalist NA The Standard - Tanzania 5, Februari 1970 baada ya kubinafsisha gazeti binafsi. Tanganyika Broadcasting Corporation iliyokuwa na muundo wa kikoloni nayo ili binafsishwa 1 Julai 1965 na kutwa Radio Tanzania Dar Es Salaa na kwa “Sauti “ya Serikali ya TANU.
Kwa hiyo hadi 1970, TANU ilikuwa na vyombo vya habari vilivyodhamiria kutimiza lengo lake kuwaunganisha watu katika ujenzi wa taifa . Hata hivyo, hakukuwa a sera rasmi ya vyombo vya habari baada ya Uhuru zaidi ya TANU na Serikali yake kutumia vyombo vya habari kuimarisha umoja wa kitaifa na kujenga taifa. Ilikuwa baada ya kuzindua Azimio la Arusha 5 Februari 1967, na ushawishi wa TANU uliyoenea, baadaye CCM kwenye vyombo vya habari imetoa athari kubwa TANU iliandaa Semina za mara mbili kwa mwaka, zilizohudhuriwa na watumishi waandamizi wa vyombo vya habari nchini na kupanga hatua zaidi za kuchukuliwa . Mwisho wa hatua hiyo kulikuwa miongozo elekezi ya sera yaliyoshwawishi utendaji wa uandishi wa habari na maudhui. Baina ya semina za mara mbili kwa mwaka, TANU, kupitia wizara yenye dhamana habari na nafasi yao katika ujamaa na kujenga taifa. Utendaji wa vyombo vya habari pia ulishawishiwa na Kamati Kamati ya Vyombo vya habari ya TANU ambayo waziri mwenye dhamana ya utangazaji alikuwa mwenyekiti .. Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wane wa Kamati kuu ya chama, wahariri watendaji wa magazeti ya Serikali na ya Chama, Mkurugenzi na mhariri mkuu wa habari wa Redio Tanzania Dar Es Salaam . Katibu WA Kamati alikuwa Katibu mkuu wa Wizara yenye dhamana ya habari.
Waraka wa Rais, aliyoutoa Rais Nyerere kutokana na wadhifa wake kama mhariri Mkuu tarehe 5 February, 1970 wakati alipotaifisha The Standard Tanzania, imeshawishi kwa kiasi kikubwa utendaji wa vyombo vya habari na maudhui. Ingawa waraka huo ulilenga gazeti moja tu mahususi, kanuni zilizowekwa na miongozo elekezi iliyotolewa ilieleweka kuwa ni sera ya vyombo vya habari kwa sababu imetaja vyombo vya habari vya umma nchini kama chombo cha utumishi wa umma. Inatosha kusema kuwa vyombo vya habari nchini Tanzania wakati wa mfumo wa Chama vilikuwa katika udhibiti mkali wa TANU na baadaye CCM . Tangu kurudishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi nya siasa 1992, ushawishi wa CCM kwa vyombo vya habari umekuwa si wa moja kwa moja kupitia sheria ambazo Serikali yake imezitunga na maagizo yasiyo andikwa.
Biashara
haihusiki
Familia & Marafiki
Maslahi jumuishi ya wanafamilia + Marafiki
haihusiki