This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2022/08/10 at 06:56
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Uhuru

Gazeti la UHURU ni gazeti la Kiswahili la kila siku linalochapishwa na UHURU   Publications Limited  kamopuni tanzu ya UHURU Media  Group inayomilikiwa na Chama cha Mapunduzi, ambacho  ni muungano  baina ya Tanganyika  African National Union (TANU)  na Afro Shirazi Party (ASD)

UHURU  inajali zaidi hotuba za viongozi wa CCM na viongozi wa serikali, wengi wao ni  makada wa Chama . Habari zake na zake na maoni ya mhariri zinasemekana  kuandikwa kwa mtazamo wa CCM na serikali yake. Limetenga nafasi kuwaelimisha na  kuwaarifu watu kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM na masuala mengine muhimu ya kitaifa, kama vile sera za serikali. Dira ya 2025 ina programu nyingine  za maendeleo.

Badaa ya  kuanzishwa  kwa Azimio la Arusha, waraka rasmi wa siasa ya ujamaa na kujitegemea  1, February, 1967. UHURU limetenga nafasi yake nyingi kusini , miongoni mwa mambo mwengine, itikadi  ya ujamaa kama  ilivyofafanuliwa kwenye Azimio la Arusha na kuanzisha mijadala kuhusu , mada zinazohusiana na maendeleo ya jamii ya kijamaa. Mhariri  wa UHURU , Benjamini Mkapa baadaye amekuwa Rais wa Awamu ya Tatu  wa Tanzania, alisema 1967 kuwa magazeti ya chama  “wakati wote yanatakiwa kuielezea Serikali “ na “kuwaambia watu walioko kwenye  nyadhifa muhimu waachane na mitazamo yao ya kikoloni”.

Historia ya UHURU imeanzia 1954 wakati TANU ilipoanzishwa na kuanzisha gazeti la SAUTI YA TANU,  kuwainganisha watu wa  Tanzania bora katika  harakati zao za kizalendo na kitaifa na kitaifa ya kupata uhuru. Gazeti hili lilihaririwa na Rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere ambaye baada ya uhuru akawa Mwasisi, Rais wa Kwanza  na Baba wa Taifa.

Siku  ya uhuru, 9 Desemba 1961, gazeti  la kihistoria la SAUTI YA TANU limebadilishwa na gazeti la wiki la UHURU ambalo chini ya jina la gazeti kulikuwa na jina dogo la GAZETI LA TANU . Lengo la UHURU ni “kuongoza njia ya uhuru na mshikamaono wa Tanganyika kwa ajili ya harakati za mapambano ya watu wote Duniani “. Katika  maoni yake ya kwanza ya mhariri, gazeti hili lilithibitisha kwamba  ni mali ya TANU wakati  lilipoandika kuwa “Leo ni siku ya shangwe  na Furaha, ni siku ya kuzaliwa  gazeti la UHURU, gazeti la TANU”

Gazeti la UHURU limejiabainisha kuwa ni  “gazeti la raia”na mwelimishaji”. Ni gazeti lenye  jukumu la kujenga taifa jipya la Tanganyika. Ni gazeti la Taifa. UHURU ni gazeti lenu”.

Gazeti la UHURU ni la kisisa kwenye  ripoti na maoni ya mhariri  yake, na huitenga nafasi yake kubwa kwa  mapambano ya kujikomboa ya nchi za Afrika zilizoko chini ya utawala  na mamlaka  ya kikoloni.

Na gazeti hili lina kiwango kikubwa  cha kuwasili wananchi na mhariri wake Joel Mgogo amekiri kuwa  ametenga 90% ya nafasi ya gazeti kuhubiri na kunasihi. Amenukuliwa kusema “kama sifanyi mimi atafanya nani?” Akitoa maoni ya tamko hilo John Condon amesema “Iwapo  Rais Nyerere ni Mwalimu  rasmi wa Taifa gazeti la chama ni mhubiri”Unasihi wote umetokana na uzingatiaji mkubwa uliopewa kwa hotuba za wanasiasa wa TANU na wale  wa Serikali. Kwa hiyo UHURU halikuwa la kibiashara na wala halikukusudiwa kuwa hivyo, lipo kwa ajili  ya kuipa TANU na Serikali yake mahali pa kutolea kauli zake ndani na nje ya nchi”.

Tarehe  7 Aprili , 1967, TANU ilianzisha  gazeti la Kiingereza la kila wiki la The Nationalist lenye sera ya uhariri isiyotofautiana  na ile ya UHURU wa kubadilishwa kuwa la kila siku, mwaka 1964. The Nationalist nalo baadaye lilibadilishwa kuwa la kila siku lakini liliunganishwa  kuwa la kila  siku lakini liliunganishwa  na The Standard Tanzania  26 April 1972 kuwa Daily News baada ya utaifishaji wa standard – Tanzania 5 February 1970. TANU ilianzisha gazeti la MZALENDO tarehe 90 Aprili 1972 kama toleo la Jumapili la UHURU. 

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

XX.XX%

Aina ya umiliki

Binafsi

Maeneo yanayofikiwa

National (mainland)

Aina ya maudhui

Maudhui yaliyolipiwa

Taarifa zisizopatikana

Taarifa za wamiliki wa vyombo vya Habari ambazo hazikupatikana, kampuni zakataa kutoa maelezo au hazikujibu au hazina hifadhi ya kumbukumbu zake

1 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Uhuru Publications Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

Uhuru Publication Limited inamilikiwa na Chama tawala cha CCM. Taarifa za BRELA zimeombwa lakini hazikupatikana

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Mmiliki Binafsi

Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Launched on independence day (December 9th 1961), the sucessor of Sauti ya TANU.

Mwanzilishi

Tanganyika African National Union (TANU) - kilikuwa chama kikuu cha siasa kilichogombea dola katika nchi ya Afrika Mashariki ya Tanganyika (ambayo sasa ni Tanzania). Chama cha TANU kilianzishwa kutoka Tanganyika African Association na Julius Nyerere mwe

Mtendaji Mkuu

Ernest Sungura - Kiongozi mkuu wa Uhuru Media Group. Alianzisha Tanzania Media Foundation (TMF) na alijiuzulu mwaka 2018, wakati akijiunga na chama.

Mhariri Mkuu

Kiondo Mshana - mwandishi wa habari anayefanya kazi na IPP media outlets. Ni mfawidhi wa Uhuru kama mhariri mtendaji

Mawasiliano

Taarifa zisizopatikana

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sep 2018), kuhusu hadira uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Magazeti yenye maslahi maalumu kama vile habari za michezo hayakujumuishwa kwenye uchambuzi wa umiliki.

Muhtasari wa vyombo vya habari

John Condon (2013). Nation Building and Image Building in the Tanzania Press. Journal Of Modern African Studies, Vol 5, pp. 355 -354.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ