This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/28 at 22:16
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Mwananchi

Gazeti la MWANANCHI liliandikishwa kwa Msajili wa Magazeti 20 April 2000 na 27 Mei 2000 nakala ya gazeti ikitoka kiwandani. Kwa sasa MWANANCHI ni gazeti la Kisahili linaloongoza kwa idadi ya Wasomaji, kwa mujibu wa utafiti wa watumiaji wa vyombo vya habari wa GeoPOll kwa robo mwaka ya pili ya 2018.

MWANANCHI ina magazine na vijarida vya kuchomoa kuhusu mada mbalimbali na kwa siku tofauti za wiki. spotiMikiki ni kijarida cha michezo kinachochapishwa kila Jumatatu na kijarida cha Uchumi kinacholenga habari za uchumi, matukio na masuala ya kiuchumi na huchapishwa kila Alhamisi. Jungukuu ni kijarida cha masuala ya kijamii kinachochapishwa kila ijumaa, wakati Starehe ni kijarida cha michezo kinachochapishwa kila Jumamosi. Siasa hulenga uchambuzi wa matukio ya karibuni ya siasa na habari za uchunguzi na huchapishwa kila Jumanne na Maarifa – ni jukwaa la wanafunzi na Waalimu na huchapishwa kila Jumatano. Fahari ni kijarida maalumu cha kuchomoa kinachowalenga wasomaji wa kike na makala kiuhusu mitindo ya mavazi, nakshi au pambo la mandhari, urembo, hadithi fupi, uhimizaji malezi n.k na huchapishwa kila Jumapili.

Gazeti la MWANANCHI huchapishwa na Mwananchi Communication Limited. Magazeti mengine yanayochapishwa na kampuni hiyo ni pamoja na MWANANCHI JUMPILI ambalo ni toleo la Jumapili la MWANANCHI na MWANASPOTI, toleo la michezo la mara mbili kwa wiki na gazeti la burudani lililoanzishwa 12 Februari, 2001. MCL pia huchapisha matoleo mawili ya magazeti ya Kiingereza ya THE CITIZEN, na toleo la Jumapili la THE SUNDAY CITIZEN.

Mwananchi Communication Limited ilianzishwa mwaka 2001 wakati Balozi Ferdinand Ruchinda alipoungana na Rostam Azizi kuianzisha. Kabla ya hapo, Balozi Ruhinda, mwaka 1999 ilianzisha kampuni ya mawasiliano ya Media Communications Limited ambayo baadaye ilikuwa Mwananchi Communication Limited.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

Aina ya umiliki

Binafsi

Maeneo yanayofikiwa

Taifa (bara)

Aina ya maudhui

Maudhui yaliyolipiwa

Uwazi hafifu

Upatikanaji wa taarifa za wamiliki kutoka kwenye kampuni/chaneli

3 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Mwananchi Communications Limited

Nation Media Group Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

MCL inachapisha kama kampuni tanzu ya National Media Group inayoendeshwa na Aga Khan Foundation na kugharimiwa kupitia Aga Khan Development Fund. Mabadiliko ya umiliki ya hivi karibuni hayajaoneshwa BRELA ambako Aziz na Ruhinda wameoneshwa kama wanahisa. Wanahisa wa sasa kwa mujibu wa MAENDELEO (Juni 29, 2018).

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Kundi / Mmiliki Binafsi

Jeangir Kermalzi Bhalov

Raia wa Tanzania. Anamiliki hisa nyingi kwa taarifa ya 2018.

51%
Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Registration 2000, Launch 2001

Mwanzilishi

Aziz Rostam - ni mwanasiasa, mfanyabiashara na miongoni mwa Watanzania tajiri sana. alijiuzulu nyadhifa zote za CCM mwaka 2011. Ruhinda Ferdinand – Alikuwa Balozi wa Jamhuri ya watu wa China. Ni mwanachama wa chama tawala.

Mtendaji Mkuu

Francis Majige Nanai - ana zaidi ya miaka 12 ya uongozi mwandamizi katika mauzo, masoko, na usimamizi kwa jumla . Alijiunga na Mwananchi Communications Limited Ofisa Mkuu Mwendeshaji Agosti mwaka 2013 kabla ya kuteuliwa kuwa nafasi aliyonayo hivi sasa mwe

Mhariri Mkuu

Bakari Machumu -Mhariri Mtendaji, Frank Sanga - Mkuu wa Ubunifu wa Maudhui, Damas Kanyabwinya - Mhariri.

Watu wengine muhimu

Kwa mujibu wa wasifu wa kampuni kutoka BRELA , wamekuwa wakurugenzi tangu Oktoba mwaka 2018:

Mawasiliano

Mwananchi Communications Limited (MCL)

P.O Box 19754, Dar es Salaam

Tel.: +255754780647

Fax: +255222224875

www.mwananchi.co.tz

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa ya ziada

Kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll (Agost 30 – 1 Sep 2018), kuhusu hadira uliyodhaminiwa na MOM Tanzania. Magazeti yenye maslahi maalumu kama vile habari za michezo hayakujumuishwa kwenye uchambuzi wa umiliki.

Muhtasari wa vyombo vya habari

Managing Editor, Mwananchi (October 2018). Media Ownership Monitor Questionnaire Mwananchi.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ