This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2022/07/07 at 01:25
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Mtanzania

Mtanzania ni Gazeti la Kila siku linalochapisha habari na taarifa za matukio katika siasa, uchumi, masuala ya kijamii, burudani na michezo. Toleo la mtandaoni “mtanzania.co.tz”, linajumuisha maoni yote ya mhariri kutoka gazeti la Mtazania lililochapishwa, pamoja na makala ya tovuti tu.

Kwa mujibu wa utafiti wa hadhira wa GeoPoll (2018), Gazeti la Mtanzania ni la 3 miongoni mwa magazeti yanayozingatia zaidi habari na XX.XXX% ya wasomaji. Kampuni inachapisha pia magazeti ya The African, Bingwa, Dimba (Arena), na Rai.

Lilianza kuchapishwa mwaka 1995 na Mtanzania Limited kwa nakala 20,000. Wakati huo ilikuwa inamilikiwa na Habari Corporation Limited, hivi sasa inachapishwa na New Habari (2006) Limited.

Kwa mujibu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) (2018), New Habari (2006) Limited inamilikiwa na wanahisa wawili, Hassan Haidari (hisa 750) na Gulam Abdulrasul mwenye hisa 750 pia. Wakati wanahisa hawafahamiki vizuri kwenye karatasi, bilionea wa kwanza Tanzania na Mbuge wa zamani wa chama tawala CCM, Rostam Aziz, anajulikana kuwa ni mmiliki na muwekezaji, kwa mfano, kwa mujibu wa jarida la IREX na Forbes. Amesema hadharani kuwa amenunua Habari Corporation (HCL), kampuni inayochapisha magazeti mbalimbali na mmiliki wa taasisi ya mafunzo kwa vyombo vya Habari, mamet. Hata hivyo jina lake halipo kwenye orodha ya wanahisa ya Isenegeja iliyowezesha ununuzi huu, wala kwenye ile ya New Habari iliyoundwa kuendesha kampuni hii ya magazeti, ambayo hata hivyo amesema ameinunua. Licha ya hayo, Aziz ana hisa pia kwenye Vodacom Tanzania, pia amepata fedha kutoka kwenye kampuni ya uchimbaji madini kimkataba ya Caspian Mining, Bandari Dar es salaam, milki nyingi za ardhi na majengo Tanzania na Mashariki ya Kati.

Wamiliki wa hisa wanakuwa Wakurugenzi wa Kampuni.

Mwaka 2013, Mtanzania ilifungiwa kwa siku 90 na Serikali kutokana na kuripoti kwa “hemko”

Ofisi rasmi ya kampuni iliyosajiliwa kwa biashara iko Bibi Titi Mohamed Street, Dar es salaam Plot No. 236. Kwa mujibu wa BRELA (2018) kampuni inatakiwa kuhuisha kumbukumbu zake kwenye mfumo wa kujiandikisha kimtandao (ORS)

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

XX.XX%

Aina ya umiliki

Binafsi

Maeneo yanayofikiwa

taifa (bara)

Aina ya maudhui

Maudhui yaliyolipiwa

Taarifa zinazopatikana kiurahisi

Upatikanaji wa taarifa za umiliki kutoka kwa vyanzo vingine, kwa mfano vile vinavyotambulikana kisheria

2 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

New Habari (2006) Ltd

Umiliki

Muundo wa umiliki

Mtanzania inachapishwa na New Habari (2006) Limited inayohusishwa na Rostam Aziz.

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Kundi / Mmiliki Binafsi

Gulam Abdulrasul Chakkar

hajioneshi. Kwa mujibu wa tetesi zilizotangazwa na tovuti ja Jamii Forum kuhusiana na Rostam. Pia anasemekana kuwa miongoni mwa mwanahisa kampuni yenye utata ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS).

50%
Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Sept. 11th 1995

Mwanzilishi

Limeanzishwa na Dimba-Mtanzania-Rai-ambapo Jenerali Ulimwengu alikuwa mwenyekiti. Katika kundi hilo, walikuwepo pia i. Jenerali Ulimwengu ii. Salvatory Rweyemamu iii. Johnson Mbwambo iv. Gideon Shoo v. Shaban Kanuwa.

Mtendaji Mkuu

Hussein Bashe - Mbunge wa CCM. Kabla ya nafasi hiyo amewahi kufanyakazi katika nyadhifa mbalimbali katika chama , kwa mfano Kamati Kuu kama Katibu wa Fedha na Uchumi. Amewahi kufanyakazi na Mwananchi Communication.

Mhariri Mkuu

Absalon Kibanda - ni mwandishi wa habari mkongwe na mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania . Mwaka 2013, alivamiwa na kuteswa na watu watatu wasiojulikana wenye bunduki na vifaa vya chuma vyenye ncha kali. Uvamisi huu unasemekana ulihusishwa na masuala

Watu wengine muhimu

Rostam Aziz - Bilionea wa kwanza Mtanzania na Mbunge wa zamani wa Chama tawala CCM, pia ni mmiliki na mwekezaji.

Mawasiliano

Taarifa zisizopatikana

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ