This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/04/19 at 23:03
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Clouds FM

Clouds FM hujulikana kuwa “Redio ya Watu” ni kituo cha redio cha binafsi kilichopo Dar Es Salaam na kumilikiwa na Clouds Media Group inayoendesha pia clouds TV, Coconut FM na Choice FM katika tasnia ya vyombo vya habari vya kielektroni.

Clouds FM ilianzishwa mwaka 1998 kwa ajili ya burudani, ni miongoni mwa redio zenye hadhira kubwa nchini Tanzania. Katika utafiti wa robo mwaka ya pili wa Geopoll kwa mwaka 2018, kituo hiki kimekuwa cha kwanza kitaifa miongoni mwa vituo 20 kwa wingi wa hadhira / wasikilizaji (XX.XXX %). Utafiti huo pia umeiweka Clouds FM ya kwanza katika kanda zifuatazo: Kati (XX.XXX %), Pwani (XX.XXX %), Ziwa (XX.XXX %) Kusini (XX.XXX %) na Nyanda za juu Kusini (XX.XXX %). Kituo hiki pia ni maarufu sana, Dar es Salaam.

Clouds FM inayotangaza vipindi vyake kwa Kiswahili inasikika na kupokewa vizuri Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya, Pemba, Mara, Tanga na Zanzibar.

Uungaji mkono na kusaidia muziki wa Bongo Fleva tangu mwanzo, matumizi ya masafa ya FM pamoja na programu bora vimesaidia kuongoza katika wingi wa wasikilizaji. Kituo hiki kinamilikiwa na Clouds Media Group ambapo Joseph Kusaga, mjasiriamali maarufu, na mwasisi mwenza, ni mtendaji Mkuu. Kusaga alianza kama DJ na alifanya matamasha na disko nchini kote Tanzania kabla ya kuanzisha kwa ubia C.L.O.U.D.S (Cool, Lovable, Outrageous, Unique, Dynamic, Sound) FM. Tangu kuanzishwa kwa CLOUDS, Kusaga ameendelea kujenga kampuni za vyombo vya habari zenye mafanikio, ukarimu na teknolojia. Mbia mwenzake kwa miaka yote Ruge Mutahaba ambaye bado ni Director of Strategy and Programs Development katika Clouds Media Group.

Hakuna data za kampuni zilizopatikana katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kuna wasifu na kampuni kwa ajili ya Clouds Television katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji Leseni (BRELA), kwa mujibu wa taarifa hizo , Alex Mkama, anamiliki hisa 25% kama Joseph Kusaga. Clouds Entertainment Limited inamiliki 50% ya Hisa.

Taarifa muhimu

Isa za hadhira

Aina ya umiliki

binafsi

Maeneo yanayofikiwa

Taifa

Aina ya maudhui

Maudhui huru

Taarifa zinazopatikana kiurahisi

Upatikanaji wa taarifa za umiliki kutoka kwa vyanzo vingine, kwa mfano vile vinavyotambulikana kisheria

2 ♥

Kampuni ya vyombo vya Habari

Clouds Entertainment Co. Limited

Umiliki

Muundo wa umiliki

Clouds Television Limitedni ni ya kwanza miongoni mwa vituo vya TV na kumilikiwa na Clouds Entertainment Limited, ambayo ni mali ya Kusaga na familia yake. Kwa mujibu wa data za TCRA na BRELA.

Haki ya kuchagua

Taarifa zisizopatikana

Mmiliki Binafsi

Kundi / Mmiliki Binafsi

Alex Mkama Kusaga

ni baba mzazi wa Joseph Kusaga, muasisi wa Clouds Entertainment Limited. Amefariki Afrika Kusini mwaka 2009 na alizikwa Dar es Salaam 7t Novemba 2009. Hadi 2018, bado ameorodheshwa kuwa mmiliki wa hisa.

25%
Kampuni ya vyombo vya Habari
Halisia

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

1998

Mwanzilishi

Joseph Kusaga - alipenda muziki tangu mdogo. alianza kuendesha matamasha tangu akiwa chuoni akisomea elektoniki, akiwa DJ maarufu na mtayarishaji matamasha. Alipata wazo la kuanzisha kampuni ya vyombo vya habari wakati alipotembelea USA, alipoungana na m

Mtendaji Mkuu

Joseph Kusaga - angalia hapo juu

Mhariri Mkuu

Ruge Mutabaha - Mkurugenzi wa Vipindi

Mawasiliano

Clouds Media Group

P.O: Box 311513, Dar-Es-Salaam

Tel.: +255222781445

E-Mail: info@cloudsmedia.co.tz

www.cloudsmedia.com

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Isa katika soko

Taarifa zisizopatikana

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ