Mwananchi Communications Limited
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Tanzania, ambaye pia ni Msajili wa Magazeti nchini, Mwananchi Commmunications Company inamilikiwa na Nation Media Group of Kenya (49%) na Bhalo Jehangir Kermali Bhaloo (51%). Mpaka hivi karibuni, kutokana na matokeo ya dodoso lililojazwa na kampuni yenyewe, Nation Media Group iliwahi kumiliki 99% ya hisa na Linus Githai 1%. Umiliki wa wageni umezidi ukomo cha kisheria cha 49% kilichosababisha mabadiliko ya hivi karibuni katika umiliki.
Mkurugenzi Mtendaji wa MCL ni Francis Majige Nanai na Mkurugenzi Mkuu ni Bakari Machumu.
Kampuni hii inachapisha MWANANCHI, gazeti la Kiswahili la kila siku linaloongoza nchini Tanzania na toleo la Jumapili la MWANANCHI JUMAPILI, na MWANASPOTI, linalotoka mara mbili kwa wiki la michezo na burudani lililoanzishwa 12 Februari 2001. Magazeti ya Kiingereza ni THE CITIZEN na toleo lake la Jumapili la THE SUNDAY CITIZEN. Kampuni pia inachapisha vijarida/magazine nyingi kwa kiingereza na Kiswahili. Machapisho ya kampuni yalikuwa yakichapwa kwa mkataba mpaka 2005, wakati iliponunua mtambo wa uchapishaji uliotumika kutoka Australia.
Historia ya Mwananchi Communications Limited inaweza kufuatiliwa kuanzia mwaka 1999 wakati Balozi Ferdnand Ruhinda alipoanzisha kampuni ya mawasiliano, Media Communication Limited na Aprili 2001 alipoanzisha kampuni mpya aliyoiita Advertising Agency & Public Relations. Hata hivyo, mwaka huo huo (2001) jukumu la uchapishaji lilihamishwa kutoka Media Comminication Limited kwenda kwenye kampuni mpya ya uchapishaji iliyoanzishwa, Mwananchi Communications Limited iliyoanzishwa na balozi Ruhinda kwa ubia na Rostam Aziz. The National Media Group of Kenya ilinunua hisa nyingi. Desemba mwaka 2002 na MCL ikawa kampuni tanzu nchini Tanzania.
Makao yake makuu yapo Kiwanja Na. 34/35 Tabata Relini, Mandela Road, Dar es Salaam, Tanzania.
Kampuni Mama
Nation Media Group Limited
Aina ya Biashara
Binafsi
Mfumo kisheria
Kampuni ya dhima yenye kikomo
Nyanja za Kibiashara
Mwananchi Communications Limited and Mwanaspoti Nwspaper imesajiliwa TCRA kama mtoa huduma ya maudhui mtandaoni, Malezo na BRELA
Kampuni
Kwa mujibu wa BRELA, Kampuni ya Kenya ya National Media Group (NMG) inamiliki 60% ya hisa. Taarifa hii inawezekana imepitwa na wakati kwa sababu umiliki wa kigeni umepunguzwa kwa mujibu wa wawakilishi wa kampuni. NMG inaendeshwa na Aga Khan Foundation na His Highness Aga Khan.
Jeangir Kermalzi Bhalov
Raia wa Tanzania. Ana hisa nyingi kwa mujibu wa mwaka 2018.
Magazeti mengine
Mwananchi
Mwananchi Jumapili
The Citizen
Sunday Citizen
Mwanasporti
Digitali nyingine
mwananchi.co.tz
mwanaspoti.co.tz
Chombo cha habari cha kibiashara
Mchapishaji Magazeti
Mwananchi Communications Limited
Huduma za Maudhui Mtandaoni
Mwananchi Communications Limited
Gazeti la Mwanasporti
Biashara
Ni biashara ya vyombo vya habari tu
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
Registration 2000, Launch 2001
Mwanzilishi
Aziz Rostam - ni mwanasiasa, mfanyabiashara na miongoni mwa Watanzania tajiri sana. alijiuzulu nyadhifa zote za CCM mwaka 2011.
Ruhinda Ferdinand – Alikuwa Balozi wa Jamhuri ya watu wa China. Ni mwanachama wa chama tawala
Waajiriwa
326
Mawasiliano
Mwananchi Communications Limited (MCL);
P.O Box 19754, Dar es Salaam;
Tel.: +255754780647;
Fax: +255222224875;
Namba ya kutambulika
TAX ID 100-895-803
BRELA Incorporation N°41222
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Utawala
Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji
Francis Nanai
Stephen Gitagama
James Kinyua
Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji
Leonard Mussusa
Hanif Jaffer
Wangethi Mwangi
Abdu Simba
John Ulanga
Bodi ya usimamizi + Bodi Maslahi ya usimamizi
Taarifa zisizopatikana
Watu muhimu wenye ushawishi + watu maslahi wengine muhimu
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Wasifu wa Kampuni BRELA umepitwa na wakati (mgongano kuhusu umiliki wa mgeni). Kurudishwa kwa dodoso na hati ya leseni ya Maelezo