This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/04/19 at 12:55
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Jamii Media Co. Limited

Jamii Media Co. Limited

Kwa mujibu wa taarifa iliyoombwa kutoka wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) tarehe 14 Septemba 2018, Jamii Media Company Limited ilisajiliwa tarehe 2 Julai,2018. Imesimamiwa chini ya Mkurugenzi MaxenceMelo (Mkurugenzi Mtendaji) na Mike Mushi. Kampuni hii pia inaendesha mtandao maarufu wa kijamii unaojulikana kama Jamii Forums.com.

Kusudio kuu la kuanzisha Jamii Forums ni kuunda jukwaa ambapo jamii ya kitanzania inaweza kushiriki kwenye mjadala huru kuhusu masuala mbalimbali yanayojitokeza kama vile ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Maudhui ya Jamii Forums yanashughulikia habari za kawaida na hutoa fursa ya majadiliano ya maswala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, michezo na burudani.

Kulingana na utafiti wa GeoPoll kuhusu matumizi ya mitandao iliyodhaminiwa na MCT, Jamii Forums ni tovuti ya kwanza kwa habari yenye 5.5% ya hadhira. Kwa mujibu wa Alexa traffic, ni ya tano miongoni mwa mitandao ya kijamii nchini (Oktoba, 2018). Taarifa ya kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inasema kwamba mtandao huu una watumiaji 2.4 milioni, walipiaji 2.8 milioni wa simu za mkononi na takribani watu 600,000 wanaotumia mtandao huu wa kijamii kila siku, mwezi Agosti 2017.

Kampuni hii ilianzishwa na sasa inamilikiwa na Maxence Melo na Mike Mushi.

Tangu kuanzishwa kwake kampuni ya Jamii Media imekuwa ikikabiliwa na shinikizo na vitisho kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa na viongozi wa serikali. Hali hii pia ilionekana mwezi Februari, 2008 wakati wamiliki wake walipokamatwa na polisi kwa kuhojiwa kuhusu kushutumiwa kujihusisha na shughuli za jinai. Hata hivyo hakuna ushahidi uliopatikana kuthibitisha tuhuma hizo.

Jamii Media ilifungua kesi ya kikatiba mwaka 2016 mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya jeshi la polisi kuiomba mahakama kutangaza kuwa mamlaka ya Jeshi la Polisi kuomba taarifa binafsi kwa mtu anayetumiwa kufanya makosa kwa mujibu wa kifungu cha 32 na 38 cha “Cyber Crime Act 2015” ni kinyume na katiba. Mwezi Machi 2017, mahakama kuu ilitangaza kuwa masharti ya sheria ni ya kikatiba.

Mwezi Desemba 2016, Melo na Mushi walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Kisutu na kushitakiwa kwa makosa matatu ya jinai: Kumiliki jina la tovuti ambalo halikusajiliwa nchini Tanzania ambapo ni kinyume na “Electronic and Postal Communication act ya 2010” na kosa la kuzuia uchunguzi wa taarifa nyeti zilizochapishwa na watumiaji (wadokezaji taarifa) kwenye Jamii Website kinyume na kifungu cha 22(2) cha “Cyber Crimes Act” ya 2015 mwezi Juni 2018, waliachiwa na mahakama ya Hakimu Mkazi kwa kutokuwa na kesi ya kujibu kwa makosa ya kuzuia uchunguzi na kukiuka “Cyber Crime Act” ya 2015. Hadi sasa (Oktoba, 2018) wamebaki na kesi mbili za kujibu na zinasubiri kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka.

Taarifa muhimu

Aina ya Biashara

Binafsi

Mfumo kisheria

Kampuni ya dhima yenye kikomo

Nyanja za Kibiashara

Jamii Forum TCRA kama Mtoa Huduma ya Maudhui Mtandaoni.

Umiliki

Mmiliki Binafsi

Maxence M. Melo

ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi (BSc) katika Uhandisi Majengo na amefanyakazi katika kampuni ya ujenzi kabla ya kuanzisha kwa ubia Jamii Forums. Pia ni mwanaharakati wa kidijitali anayehamasisha uhuru wa kutoa mawazo, usalama wa kidijitali na uhuru wa habari na si mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini Tanzania.
Mike Mushi – Muasisi mbia wa Jamii Forums tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 tu. Alianza kusimamia Jamii Forums mara tu alipomaliza shule ya msingi ya Green Acres mwaka 2003. Hivi sasa ni Mkurugenzi na Mkuu wa Ubia wa Biashara na Masoko katika Jamii Media. Amesoma shahada ya Business Administration with Information Technology katika Learn IT kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013.

51%

Mike Mushi

muasisi mbia wa Jamii Forums tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 tu. Alianza kusimamia Jamii Forums mara tu alipomaliza shule ya msingi ya Green Acres mwaka 2003. Hivi sasa ni Mkurugenzi na Mkuu wa Ubia wa Biashara na Masoko katika Jamii Media. Amesoma shahada ya Business Administration with Information Technology katika Learn IT kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013.

49%
Vyombo vya habari
Other Media Outlets

Digitali nyingine

jamiiforums.com

Halisia

Chombo cha habari cha kibiashara

Huduma za Maudhui Mtandaoni / Mitandao ya Kijamii

Jamii Media Co. Limited

Biashara

Ni biashara ya vyombo vya habari tu

Hakuna

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

2nd July, 2008

Mwanzilishi

Maxence Melo – ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi (BSc) katika Uhandisi Majengo na amefanyakazi katika kampuni ya ujenzi kabla ya kuanzisha kwa ubia Jamii Forums. Pia ni mwanaharakati wa kidijitali anayehamasisha uhuru wa kutoa mawazo, usalama wa kidijitali na uhuru wa habari na si mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini Tanzania.
Mike Mushi – Muasisi mbia wa Jamii Forums tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 tu. Alianza kusimamia Jamii Forums mara tu alipomaliza shule ya msingi ya Green Acres mwaka 2003. Hivi sasa ni Mkurugenzi na Mkuu wa Ubia wa Biashara na Masoko katika Jamii Media. Amesoma shahada ya Business Administration with Information Technology katika Learn IT kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013.

Waajiriwa

Taarifa zisizopatikana

Mawasiliano

Jamii Media Co. Limited

P. O. Box 4203

DAR ES SALAAM

maxence@jamiiforums.com

Tel:+255 758525253

Namba ya kutambulika

BRELA Incorporation N°66333

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Utawala

Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji

Taarifa zisizopatikana

Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji

Taarifa zisizopatikana

Bodi ya usimamizi + Bodi Maslahi ya usimamizi

Taarifa zisizopatikana

Watu muhimu wenye ushawishi + watu maslahi wengine muhimu

Taarifa zisizopatikana

Maelezo ya ziada

Taarifa zisizopatikana

Taarifa za wamiliki wa vyombo vya Habari ambazo hazikupatikana, kampuni zakataa kutoa maelezo au hazikujibu au hazina hifadhi ya kumbukumbu zake

1 ♥

Taarifa ya ziada

Company is available at BRELA, was requested, however, not released due to a pending court case. Registered at TCRA (only one shareholder mentioned). No return of questionnaires.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ