IPP Media Limited
IPP Media limited ni miongoni mwa mkusanyiko wa Vyombo vya Habari mkubwa sana Afrika Mashariki na ilisajiliwa 9 Novemba 1999. IPP Media ni kampuni binafsi inayofanya kazi chini ya IPP Group Limited yenye masikani yake jijini Dar es Salaam, Tanzania
IPP Media in magazeti tisa yanayochapishwa kila siku kwa Kiingereza (The Guardian, Sunday Observer, Financial Timems na This Day) na Kiswahili (Taifa letu, Nipashe, Majira, Lete raha). Pia ina vituo vitatu vya Televisheni (ITV, EATV, na Capital Television) na Vituo vitatu vya redio (Radio One, Capital FM na East African Radio) vingi vyao hutumiwa Tanzania. IPP media pia ni mtoa maudhui mpana kwa ajili ya Habari za Afrika Mashariki kwenye mtandao kupitia tovuti yake ya www. ippmedia.com.
IPP Media ni sehemu ya kundi la kampuni binafsi na kuanzishwa na Ndg. Reginald Abraham Mengi tangu miaka ya 1980 katika wadhifa wa mwenyekiti na Managing Partner wa Coopers & Lybrand nchini Tanzania. IPP Group Limited ni kampuni ya utengenezaji utiaji vinywaji kwenye chupa na kundi la vyombo vya habari inayojumuisha Televisheni vituo vya radio na magazeti.
IPP Group ilianza kama kiwanda kidogo cha kalamu kinachoendeshwa kwa mkono jijini Dar es Salaam na sasa kimepanuka na kuwa na uzalishaji bidhaa anuwai na kundi kubwa la kampuni katika Afika Mashariki. Hivi sasa ina vitengo vinne vikuu kama vile Vyombo vya Habari, Vinywaji, (Kilimanjaro Pure Drinking Water, ina uwakala wa bidhaa za vinywaji baridi vya CocaCola, mwagizaji na msambazaji mkuu wa Calsberg wa Pombe Kali) vyombo vya nyumbani na vipodozi, utafiti na uchimbaji wa madini.
Wasifu wa kampuni uliyoombwa kwenye Masjala ya Biashara unaonesha kuwa Mengi ni mwanahisa wa IPP Group Limited pamoja na Agapitus Leon Nguma.
Mengi alizaliwa Tanani mwaka 1944. Yeye ni mfadhili wa Kitanzania, mwanaviwanda, mmiliki wa vyombo vya habari na mwasisi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Group. Mengi pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa Wahasibu FORBES, amekuwa miongoni mwa matajiri wa Afrika mwenye zaidi ya $400 milioni kwa takwimu za mwaka 2015.
Kampuni Mama
IPP Limited
Aina ya Biashara
Binafsi
Mfumo kisheria
Kampuni ya dhima yenye kikomo
Nyanja za Kibiashara
Utengenezaji, utiaji vinywaji kwenye chupa na vyombo vya habari (ikiwemo televisheni na redio, vituo vya redio na magazeti)
Mmiliki Binafsi
ni mwanaviwanda wa Tanzania, mmiliki wa vyombo vya habari na muasisi, pia ni Mwenyekiti mtendaji wa IPP Group. Pia ni Makamu wa Rais wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania.
Agapitus Leons Nguma
alikuwa katibu wa kampuni na mwanahisa. Amefariki dunia 1 Mei 2018. Alikuwa pia Mkurugenzi wa the Guardian Ltd.na Bonite Bottlers Ltd. Kitaaluma ni Mwanasheria.
Magazeti mengine
The Guardian
The Guardian on Sunday
Nipashe
Nipashe Jumapili
Financial Times
This Day
Kulikoni
Alasiri
Taifa Letu
Lete Raha
Sema Usikike
Televisheni zingine
ITV
Capital TV
East Africa TV
Radio nyingine
Radio One
Capital FM
East Africa Radio
Digitali nyingine
ippmedia.com
guardian.co.tz
Chombo cha habari cha kibiashara
The Guardian Limited
Online Content Provider
Independent Television (ITV) Services-www.itvpopote.com
Media
IPP Media Limited
Biashara
all businesses operate at least regional.
Food & Beverages
Bonite Bottlers - Franchise for Coca Cola carbonated soft drinks brands
Mining
IPP Resources - mines gold, uranium, copper, chrome and coal)
IPP Minerals and Prospecting - mining, cutting, faceting and polishing of stones including Tanzanite, Ruby, Sapphire, Emerald and Alexandrite.)
Households & Beauty
number of brands including REVOLA. Manufactures and distributes under license the GIV Beauty Soap from “PT. Wings Surya (Indonesia).
TESA ULTRA WASHING POWDER
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
1999
Mwanzilishi
Dr. Reginald Mengi - see above
Waajiriwa
Taarifa zisizopatikana
Mawasiliano
Haidery Plaza Building,
Ali Hassan Mwinyi Road/ Kisutu Street, 7th Floor
Dar es Salaam.
Namba ya kutambulika
BRELA incorporation n°: 38275
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Utawala
Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji
Taarifa zisizopatikana
Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji
Taarifa zisizopatikana
Bodi ya usimamizi + Bodi Maslahi ya usimamizi
Taarifa zisizopatikana
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Company profile available at BRELA. Registered at TCRA. No return of questionnaire.
Reginald Abraham Mengi (2018), I Can, I must, I will. ISBN-10: 9781717871749.