This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/09/15 at 17:41
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Econet Media Tanzania Limited

Econet Media Tanzania Limited

Econet Media Limited ni kampuni ya  dhima yenye kikomo iliyosajiliwa Tanzania, Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Septemba 2010 kama chombo cha utangazaji.

Kampuni hii ina vituo viwili: TV1 Tanzania na Kwese TV, vyote ni vituo vya televisheni vya “Free to air”. Tovuti zao ni www.tv1.co.tz na www.kwese.co.tz. Ni sehemu ya kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu ya kimataifa – Econet Wireless Group –yenye shughuli na uwekezaji katika zaidi ya nchi 15.

Econet Media Ltd imeingia katika soko la vyombo vya habari la Tanzania wakati kampuni yake tanzu ya burudani ya African Telecoms Group, Econet Wireless iliyoingia mkataba na kununua Viasat 1- ambayo mpaka wakati huo ilikuwa inaendesha TV1- mwaka 2016. Kabla ya hapo, Viasat 1 ilikuwa inamilikiwa na Modern Times Group (MGT) - kampuni ya burudani ya Sweden iliyokuwa pia inadhibiti Modern African Productions (MAP) na hisa nyingi katika Trace Africa.

Hivi sasa, Econet Media Ltd, ina hisa 49% za TV1. Raia wa Zimbabwe, Strive Masiyiwa ni Mwasisi na Mwenyekiti Mtendaji wa Econet. Biashara zake ni pamoja na nishati jadidifu, vyombo vya habari na ukarimu. Hisa zilizobaki zinamilikiwa na raia wa Tanzania, Dkt Wilbert Basilius kapinga (41%) na Dkt Gideon Kaunda (10%)

Dkt Gideon H Kaunda ni “Corporate Lawyer na Communications na Transport Specialist” mwenye uzoefu mkubwa wa huduma za uendelezaji mradi na mshauri wa sheria. Hivi sasa ni mwenyekiti wa Pangaea Arbitrator kutoka International Court on Aviation and Space Aviation (IASA). Ni mjumbe wa Bodi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ambaye ni mwenyekiti  wa kamati ndogo ya Huduma za Wananchi na kujenga Uwezo.

Dkt Wilbert Basilius Kapinga ni bingwa wa sheria ya kampuni, sheria ya fedha , shughuli za kibenki, ubinafsishaji, mawasiliano ya simu na sheria ya ushindani wa biashara na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 ya miamala na miradi kwenye maeneo hayo.

Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Econet Media Limited/Kwese ni Joseph Hundah, aliyeacha kazi Modern Times Group kwa ajili ya wadhifa katika Econet.

Kampuni haijatoa taarifa tangu 2015, 2017 na 2018. Kampuni imejaza fomu za mabadiliko za kisheria kuonesha baadhi ya mabadiliko ingawa fomu hizo pia hazijasajiliwa kutokana kutofuata utaratibu.

Namba ya utambulisho wa ulipa kodi ni 110-803-982 na mtu wa kuwasiliana ni Kaimu Meneja Mkuu. ECONET ina wafanyakazi 70.

Taarifa muhimu

Kampuni Mama

Econet Media Limited

Aina ya Biashara

Binafsi

Mfumo kisheria

Kampuni ya dhima yenye kikomo

Nyanja za Kibiashara

Econet Media Tanzania imesajiliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni na kufanyakazi kama mtangazaji kwa njia ya televisheni. Licha ya kazi hiyo, Econet Group inafanya biashara katika nishati jadidifu, mawasiliano kwa njia ya simu, huduma za fedha, ukarimu, bima, biashara kwa njia ya mtandao, elimu, utiaji vinywaji kwenye chupa na mifumo ya malipo

Umiliki

Kampuni

Econet Media Tanzania Limited

Strive Masiyiwa ni Mzimbabwe , ni Muasisi na Mwenyekiti Mtendaji wa Econet. Anapendelea pia biashara ya nishati jadidifu , huduma za fedha, vyombo vya habari na ukarimu.

49%
Econet Media Tanzania Limited

Mmiliki Binafsi

Dkt Wilbert B. Kapinga

yeye ni mwanasheria wa Mkono & Co Advocates, amebobea katika sheria ya kampuni, sheria ya fedha, ubinafsishaji, sheria ya mawasiliano ya simu na ushindani,na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 kuhusu miamala ya miradi katika maeneo hayo.

41%

Dr. Gideon Kaunda

Dr Kaunda alikuwa ni Mwanasheria wa Kampuni, na Bingwa wa Mawasiliano na Uchukuzi mwenye uzoefu mkubwa katika huduma za utayarishaji miradi na ushauri wa sheria. Zamani alifanyakazi kama Principal Assistant Counsel and Legal Advisor katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa miaka minane (1969-1977), baada ya hapo aliteuliwa kuwa Mwakilishi wa Serikali ya Tanzania kwenye Council of the Internation Civil Aviation Organisation (ICAO) kwa kipindi cha miaka sita.
Dr Kaunda alijiunga tena na serikali mwaka 1984 na kufanya kazi mbalimbali za ushauri elekezi katika PTA (COMESA), Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, kabla ya kuazimwa kwenda kufanya kazi kama Special Assistance to the Chief Executive Officer of Alliance Air
Dr Kaunda rejoined the Government in 1984 and took up various consultancy assignments with the PTA (COMESA), The World Bank, The European Union, among others, prior to being seconded as Special Assistance to the Chief Executive Officer of Alliance Air.

10%
Vyombo vya habari
Other Media Outlets

Televisheni zingine

TV1

Digitali nyingine

tv1.co.tz

Halisia

Chombo cha habari cha kibiashara

Utangazaji kwa njia ya Televisheni

Econet Media

Biashara

hakuna

Biashara zifuatazo zinaendeshwa chini ya kampuni mama:

Telecom

Econet Wireless International (Mauritius, Lesotho, South Africa, Botswana, Zimbabwe, Burundi, Nigaria, UK, China)

Hospitality

East Africa DataCentre

Finance Services

Liquid Telecom Payment Solutions

E-Commerce

Cassava Fintech

Insurance

Cassava Fintech

Renewable energy

Solarway (United Arab Emirates, Portugal)

Education

Ruzivo (Zimbabwe)

Telcom

cumii technologies

Agriculture

Drone Africa

Game Monitoring

Drone Africa

Mapping and Surveying

Drone Africa

Maelezo yote

Mwaka wa kuanzishwa

Missing Data

Mwanzilishi

Strive Masiyiwa - Anapendelea pia biashara ya nishati jadidifu , huduma za fedha, vyombo vya habari na ukarimu.

Waajiriwa

70

Mawasiliano

Missing Data

Namba ya kutambulika

Tax ID 110-803-982
BRELA Incorporation N°126003

Taarifa za kifedha

Taarifa ya Kifedha

Taarifa zisizopatikana

Faida za uendeshaji

Taarifa zisizopatikana

Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)

Taarifa zisizopatikana

Utawala

Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji

Christopher David Wadman

Director. South African National.

Maelezo ya ziada

Taarifa zinazopatikana kiurahisi

Upatikanaji wa taarifa za umiliki kutoka kwa vyanzo vingine, kwa mfano vile vinavyotambulikana kisheria

2 ♥

Taarifa ya ziada

Company profile available at BRELA. No proof of registration at TCRA. Contradictory to information provided by company itself.

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ