Clouds Entertainment Co. Limited

Clouds Media Group ni kampuni ya kimataifa na vyombo vya habari mbali mbali na miongoni mwa vyombo vya habari vinavyoongoza katika Afrika Mashariki na kati. Clouds inatetea zaidi sauti inayobadilika, tulivu, inayopendwa, yenye nguvu na ya kipekee (cool, lovable, outrageus, unique, Dynamic, sound), ilianzishwa mwaka 1998 na Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.
Akivutiwa na mandhari ya muziki ya Los Angeles, Kusaga ameungana na mdau wake wa biashara wa muda mrefu, Ruge Mutahaba, walianza kupanga kituo cha redio kwa Tanzania ambacho muda si mrefu kitakuwa Clouds FM. Ilianza na kituo kimoja cha redio chenye chumba kidogo cha Studio. Kuanzia hapo, Clouds imekuwa na kuchanua na kuwa Shirika linaloshughulikia vyombo vyote vya utangazaji kwenye nyanja za usimamizi wa matukio, masoko na dijiti.
Hivi sasa kampuni hiyo inaendesha vituo vya redio; Clouds FM inayojulikana kuwa “Redio ya Watu”, Choice FM kituo cha burudani cha Kiingereza kwa ajili ya wataalamu vijana wa Tanzania waliosoma nchi za nje na sasa wamerudi nchini na coconut FM inayotangaza kutokea Zanzibar.
Kampuni ya Clouds inamiliki vituo tisa vya TV, ikiwemo Clouds TV, 50- Channel cable. DTT TV Network, OTT platform, kampuni ya masoko ya matukio, Ngoma web TV na Gazeti la Kitangoma. Hasa Clouds FM na Clouds TV siku hizi ni vyombo vya habari vinavyosikilizwa na kutazamwa zaidi nchini. Kampuni hii yenye zaidi ya wafanyakazi 300 ina hadhira kubwa Afrika Mashariki na Kati, Mashariki ya Kati na Visiwa vya Caribbean na kufungwa Ofisi Kingston Jamaica.
Hakuna data za Kampuni katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kuna wasifu wa kampuni kwa ajili ya Clouds Television katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Utoaji wa Leseni (BRELLA), kwa mujibu wa taarifa hizo, Alex Mkama anamiliki hisa 25% kama Joseph Kusaga. Clouds Entertainment Limited inamiliki 50% ya hisa.
Ruge Mutahaba hivi sasa bado ni Director of Strategy and Programs Development katika Clouds Media Group.
Aina ya Biashara
Umma
Mfumo kisheria
Binafsi
Nyanja za Kibiashara
Utangazaji, Matangazo ya biashara
Mmiliki Binafsi
Joseph Kusaga - Mkurugenzi Mtendaji. alizaliwa mwaka 1966, Mtanzania. alipenda muziki tangu mdogo. alianza kuendesha matamasha tangu akiwa chuoni akisomea elektoniki, akiwa DJ maarufu na mtayarishaji matamasha.
Alipata wazo la kuanzisha kampuni ya vyombo vya habari wakati alipotembelea USA, alipoungana na mbia wake wa biashara wa muda mrefu Ruge Mutahaba, na kuanzisha mpango wa kituo cha redio kwa Tanzania ambacho baadae kitakuwa Clouds FM.

Judith Violet Kusaga
Mkurugenzi. Amezaaliwa 1955. Mtanzania.
Sheba Martha Kusaga
Mkurugenzi. Amezaliwa 1971. Mtanzania. Ukurugenzi mwingine wa zamani au wa sasa: Choice FM Limited, Clouds Television Limited.
Televisheni zingine
Clouds TV
Clouds TV Rwanda
Clouds TV International
Radio nyingine
Clouds FM
Coconut FM
Choice FM
Chombo cha habari cha kibiashara
Utangazaji
Clouds Television Limited
Clouds FM Limited
Choice FM Limited
Biashara
hakuna
Cloud broadcasts in Rwanda.
Maelezo yote
Mwaka wa kuanzishwa
1998
Mwanzilishi
Joseph Kusaga - developed a passion for music at a very early age. He started to organize events when he was still at the college studying electronics, and became a very popular DJ and event organizer.
He got the idea to start a media company during his visit to the USA, where he connected with his life-long business partner, Ruge Mutabaha, and started to plan a radio station for Tanzania that would later become Clouds FM.
Alex Mkama Kusaga - passed away. Father to Joseph Kusaga.
Waajiriwa
Taarifa zisizopatikana
Mawasiliano
Clouds Media Group
P.O: Box 311513, Dar-Es-Salaam;
Tel.: +255222781445
E-Mail: info@cloudsmedia.co.tz
Namba ya kutambulika
BRELA incorporation n°: 30218
Taarifa za kifedha
Taarifa ya Kifedha
Taarifa zisizopatikana
Faida za uendeshaji
Taarifa zisizopatikana
Utangazaji(jumla ya mapato kwa asilimia)
Taarifa zisizopatikana
Utawala
Bodi ya utendaji + Bodi Maslahi ya utendaji
Company Secretary as of 2016.
Bodi isiyo ya utendaji + Bodi maslahi isiyo ya utendaji
All owners are also registered as company directors.
Watu muhimu wenye ushawishi + watu maslahi wengine muhimu
Ruge - Director of Strategy and Programs Development at Clouds Media Group in Tanzania.
Maelezo ya ziada
Taarifa ya ziada
Company registered at BRELA. No proof of registration at TCRA. Habari Corporation still also available at BRELA. No return of questionnaires.