This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2024/03/28 at 14:52
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Maxence M. Melo

Maxence M. Melo

Maxence Melo alizaliwa Mei, 1976 katika kijiji cha Kantare mkoa wa Kagera nchini Tanzania. Yeye ni mwanzilishi mwenza na mmiliki mwenza wa Jamii Media Limited inayoendesha tovuti ya Jamii Forums inayokosoa na kuhakiki serikali iliyo madarakani.

Melo ana Full Technician Certificate (FTC) kutoka Dar es salaam Institute of Technology (DIT) na Bachelor of Science Degree katika Civil Engineering kutoka DIT pia, hakupenda kufanyakazi katika taaluma yake ya Teknolojia ya Habari (IT). Baada ya kuhitimu mafunzo yake, alifanya kazi kwenye CSI Company, ni kampuni ya ujenzi, kabla ya kuanzisha kwa pamoja Jamii Forums. Maxence Melo ni mwanaharakati wa kidijiti anayehamasisha uhuru wa kujieleza, usalama wa kidijiti na uhuru wa habari na si mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini Tanzania.

Mbia mwenza na mwanzilishi mwenza Mike Mushi yuko kwenye Jamii Forum tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 tu. Alianza kusimamia jukwaa hilo baada ya kumaliza elimu ya msingi, Green Acres Primary School, 2003. Kwa sasa Mushi ni Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa Ubia wa Biashara na Masoko katika Jamii Media. Kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 alikuwa akisomea Bachelor Degree katika Bussiness Administration with Information Technology katika LearnIT.

Kusudio kuu la kuanzisha Jamii Forums ni kuunda jukwaa ambapo jamii ya kitanzania inaweza kushiriki kwenye mijadala huru ya masuala mbalimbali yanayo jitokeza kama vile ya kujamii, kisiasa na kiuchumi. Tangu kuanzishwa kwake Jamii Media imekuwa ikikabiliwa na shinikizo na vitisho kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo wanasiasa na viongozi wa serikali. Mwezi Februari, 2008, Melo na Mushi walikamatwa na Polisi kwa kuhojiwa kuhusu kushukiwa kujihusisha na shughuli za jinai. Hata hivyo hakuna ushahidi uliopatikana kuthibitisha tuhuma hizo.

Mwezi Desemba 2016, Melo na Mushi walifikishwa mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu na kushitakiwa kwa makosa ya 1) kumiliki jina kikoa la tovuti ambalo halikusajiliwa nchini Tanzania ambapo ni kinyume na “Electronic and Postal Communication Act ya 2010 na 2) kosa la kuzuia uchunguzi wa taarifa nyeti zilizochapishwa na watumiaji (wadokezaji wa taarifa za udhaifu wa serikali iliyo madarakani) kwenye Jamii Website kinyume na kifungu cha 22(2) cha “Cyber Crimes Act” ya 2015.

Hata hivyo, mwezi Juni 2018, Waliachiwa na mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu kwa kutokuwa na kesi ya kujibu kwa kosa la kuzuia uchunguzi na kukiuka “Cyber Crimes Act” 2015. Hadi sasa (Oktoba 2018) wamebaki na kesi mbili za kujibu na zinasubiri kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka.

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ