This is an automatically generated PDF version of the online resource tanzania.mom-gmr.org/en/ retrieved on 2023/01/30 at 11:56
Global Media Registry (GMR) & Media Council of Tanzania - all rights reserved, published under Creative Commons Attribution-NoDerivatives 4.0 International License.
Media Council of Tanzania LOGO
Global Media Registry

Freeman Mbowe

Freeman Mbowe

Freeman Mbowe ni mwanasiasa wa Tanzania na Mwenyekiti wa sasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA – Political Party for Democracy and Development). Alichaguliwa kuendelea kama Mbunge anayewakilisha Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hivi sasa anaendelea na siasa kwenye chama hicho hicho cha siasa.

Amehusishwa na kutajwa katika umiliki wa Free Media Ltd inayoendesha gazeti la Kiswahili la Tanzania Daima. Hata hivyo, kwa maandishi, katika Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mke wake Dr. Lillian Mtei ametajwa kuwa mwasisi, mwenye hisa nyingi (75%) na mkurugenzi.

Free Media Limited ni kampuni ya uchapishaji inayohusika na uchapishaji wa magazeti na mmiliki wa Gazeti la Kila Siku la Kiswahili la Tanzania Daima. Akwa mujibu wa www.zoomtanzania.com/biz/tanzania-daima-newspaper, namba ya utambulisho wa biashara ya Free Media Limited ni 486563.

Kwa mujibu wa kiasi cha hadhira kulingana na utafiti wa GeoPoll (2018), gazeti lake, Tanzania Daima ni la 11, lenye 2% ya wasomaji miongoni mwa magazeti 30 yaliyochaguliwa kwenye mradi nchini.

Kampuni ya vyombo vya Habari
Aina za vyombo vya habari
Halisia

Biashara

Nyazifa rasmi

mwenyekiti wa sasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA – Political Party for Democracy and Development) tangu 2004

Familia & Marafiki

Maslahi jumuishi ya wanafamilia + Marafiki

Edwin Mtei

Baba Mkwe. Alikuwa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa Nyerere na alikuwa Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania. Mwaka 1992 Bw. Mtei alijitumbukiza kwa ukamilifu katika siasa za vyama vingi. Alianzisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kufanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba chama hicho kinakua, licha ya kushindwa kwake ubunge wa Arusha mjini katika uchaguzi wa mwaka 1995

  • Project by
    Media Council of Tanzania
  •  
    Global Media Registry
  • Funded by
    BMZ